Najuta kutembea na wallet! Sitorudia kuweka pesa kwa wallet kamwe!

Hela zinakaa kwenye mfuko wa shati, mnawekaje kwenye wallet na ni 2026 hii?
 
Unakaa na wana halafu huwatoi hata kidogo,wakati wanajua upo njema,umekosea sana ungewatoa kidogo,wasinge fanya hilo mkuu,jamaa huwa wanaridhika na pesa ndogo sama hata wekundu mmoja tu ungeatosha.
Mjini wanakuja nawapokea mm na michongo mimi ndo nawapa ,na huwa nawa cash out mara kibao tu wacha maneno
 
Sheria ya wallet ukiwa unatembea ndo inatakiwa uweke mfuko wa nyuma ila ukiwa unakaa chini au umepanda gari wallet unatakiwa uweke mfuko wambele wa suluali ukifuata hii hautojuta mimi siwezi kabisa kutembea bila wallet kabisa unawekaje wallet nyuma alafu umekaa huoni unakaa tako moja juu
 
Mateso mie sitaki hata kutumia
 
Huu ujinga Bado ulikuwa nao?
 
Msiisingizie wallet wazee, mi tangu nimeanza kupata pesa zangu mwenyewe huwa natumia wallet na haijawahi kunipa hasara yoyote, hao Wanao ndo miyeyusho tu
 
Ujinga wallet ni heshima kwa mwanaume ukitoa hela local kwenye mifuko unaonekana local sana sasa kadi za NIDA na za Bank unatunzawapi
Kuna siku utatoa milio
 
Msiisingizie wallet wazee, mi tangu nimeanza kupata pesa zangu mwenyewe huwa natumia wallet na haijawahi kunipa hasara yoyote, hao Wanao ndo miyeyusho tu
Vina muda
 
Kuna hawa wanaojaza wallet mpaka ticket za treni za mwaka jana,
Risiti za ATM kibao kwanini usiweke nyumbani kama unatunza kumbukumbu?
Miaka na miaka wallet imejaa takataka
Unajua ni ukilema huo imagine unakaa kwenye bus au gari lako kila leo na huitoi mfukoni sasa hayo makalio yataacha kufa ganzi
Maana kama sio ganzi wanaitoaje mfukoni bila kuhisi? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Unakuja kuzeeka unaanza kuchechemea hujui sababu
 
Mimi swala la wallet ni
Miaka ya nyuma nilikua mpenzi mkubwa wa wallet hasa kipindi nipo shule o level na a level ila kiukweli kwa life ya kipindi iko kishule shule wallet ilitokea kunigharimu sana mara wallet imepotea na ilikua ya senti zangu za kudunduliza mara sijui wallet nimeiweka wapi ukizingatia mda huo kuna sehemu natakiwa niende basi kuna mda nikawa napandwa na hasira... ila uo mchezo wa kutembea na wallet nilikuja kuacha nilivoingia chuo na ata baada ya kumaliza chuo.. japo kwa sasa nina wallet lakini sijawai kutembea nayo nimeiweka tu ndani kama kihifadhio cha vitambulisho vyangu, kadi zangu za benki na baadhi ya risiti
 
Mie nimeokoka now sitaki Waleti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…