Najuta kutembea na wallet! Sitorudia kuweka pesa kwa wallet kamwe!

Najuta kutembea na wallet! Sitorudia kuweka pesa kwa wallet kamwe!

Habari wakuu.

Leo mida ya mchana hivi nilikuwa om ,nikasema nitoke kiaina nikawacheki wana kijuweni, si unajua wana wa kitaa kuonana mpaka wikiendi,so nikapita ATM 🏧 Nikatoa kama laki 2 hivi nikatia kwa walet mfuko wa suruali ya jeans tena wa nyuma nikasema nipite kwa wana pale ,kijiwe nongwa , niwape hai ,nikawakuta wanawangu wawili kwenye bench, walivyoniona ,salam shangwe kama zote ,

Si nikaa pale mwanangu, kwenye lile bench ,aiser tukapiga story pale wee ,nikasema nisepe, nikaamka kwenda dukani kununua mazaga ya om kufika dukani pale ,kuingiza mkono mfukoni walet haipo,nakahisi pale nilipokuwa nimekaa na wanangu kwenye lile bench itakuwa imendondoka pale nikarudi pale kama umeme kufika pale wanangu hawapo !,

Nimewapigia simu kuwauliza simu zao zote wawili hawapatikani 😪😪😪 niliwatafuta mno baada niliwapata na niliwakuta ,wapo sehemu wanakunywa na shangwa juu !sikutaka hata kusemesha maan hawakuniona pale niliondoka kinyoge sana ila sitokuja kuweka pesa kwa walet never
🙆😅
 
Wallet nnayotumia mimi tracker
Hivi huko nyumbani hazipo

Ova
 
Mwaka 2004 nikiwa darasa la sita nilipoteza walett iliyokuwa na shilingi elfu 12 ,mbaya zaidi ilikuwa siku ya kuamkia sikukuu ya pasaka ...kuanzia hapo sijapwahi kumiliki wallet.
Sitaki hata kusikia kuhusu waleti
 
dah boarding kwa moto, shuleni kwetu sijui watu walikuwa wananusa hela? hata ukiweka hela kukiwa giza tiii ukaificha chini kabisa ya tranka ukaibana na nguo, still unakuta siku ya pili hela imeibwa, jumlisha huo ugeni i feel you huo mwezi ulivyokuwa
Bora mtu achukue ambaye hata sijui sasa hawa ni wanangu haswa wakiwa na shida nawasaidia usingizi nakosa
 
Mimi nilikuwa nasoma day nilipofika form three nikahamishiwa boarding. Nimefika bwenini na ushamba wangu naweka hela kwenye tranka na funguo naweka chini ya mto. Siku moja narudi tranka limefunguliwa wamenibebea elfu hamsini yangu kama ilivyo. Niliteseka ule muhula sitasahau, ukichanganya na ugeni sina hata rafiki hali ilikuwa mbaya zaidi
Aiser pole
 
Binafsi nikivaa jeans ziwezi toboa bila 50 flan kwa wallet insue ni Moja Kuna Wana masnich kinouma usipime Yani ni hatari
Nimejifunza mbona kwa njia ngumu
 
Tatzo hutoagi ganji kwa wana,ndio maana hawakurudisha
Dah wana wanakuja mjini hapa mie ndo nimewapokea na kuwapa michongo ya mjini mpaka wanatambulika na watu , tena kwa roho safi unsongea nini ww
 
Siku nyingine weka mifuko tofauti, Mimi Falsafa yangu ni kuwa sichanganyi vitu vyangu muhimu sehemu moja, iwe pesa au chochote kile cha muhimu Sana kwangu...Mifuko ya jeans ni minne, Mifuko miwili ya nyuma yote weka pesa halafu maliza na wa kushoto...suruali zangu za jeans zote zina vifungo Mifuko ya nyuma, Kadi ya benki mfuko wa mbele kushoto, simu mfuko wa kulia mbele, funguo ya gari mfuko wa mbele...kabla Hela sijaitoa mfukoni Jua ishahesabiwa kitambo na sinaga mambo ya keep chenchi wala kutoa ofa, Kila mmoja ale pesa zake...
Umenifundisha mkuu now sites sitembei na makorokoro sim banking unyama
 
Hao siyo marafiki bali ni genge la wahuni :3Heading:
Tamaa now hata kuniangalia usoni wanaona aibu ,nimekutana naona tena mida narudy om niwapa mpaka hai ,kiroho safi wao ndo wanaona aibu ,namuachia mungu watanitafutaga tu
 
Nina miaka zaidi ya 20 natumia wallet sijawahi hata kuidondosha kwa bahati mbaya tena naiweka mfuko wa nyuma ya suruali au jeans, nipo sensitive sana hata ikikaa vibaya najua haijakaa vzuri sehemu yake. Hata nilewe kiasi gani siwezi dondosha wallet. Mambo mengine ni umakini tu
 
Nina miaka zaidi ya 20 natumia wallet sijawahi hata kuidondosha kwa bahati mbaya tena naiweka mfuko wa nyuma ya suruali au jeans, nipo sensitive sana hata ikikaa vibaya najua haijakaa vzuri sehemu yake. Hata nilewe kiasi gani siwezi dondosha wallet. Mambo mengine ni umakini tu
Usitukane mamba siyo dudu baya lakini kabla hujavuka moto kamwe komaaaa
 
Ukiweka laki 2 kwenye wallet si itakuwa imetuna sana...

Anyway siku nyingine jifunze kuhifadhi pesa kwa kuzitawanya sehemu tofauti tofauti...

Ukivaa jeans, weka mifuko ya mbele haswa kile kipocket kidogo...
Kuna jamaa yangu wa Kigamboni aliikunja 20,000 zile elfu kumi mbili muundo kama wa sigara (roller) akaweka kwenye hiko ki_pocker cha jinsi. kuingia kwenye pantoni mpaka anatoka kufanya manunuzi kwenye yale maduka pale Kigamboni hana hata mia.
 
Back
Top Bottom