Najuta kuzaliwa kwenye familia ya kilokole

Najuta kuzaliwa kwenye familia ya kilokole

Faza 99

Member
Joined
Sep 17, 2019
Posts
38
Reaction score
69
Mimi ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto 6, baada ya Dada na braza me nilifuatia. Faza etu ni pastor wa kanisa Fulani la kilokole na ni mcha mungu katika kweli kabisa ya mungu in short familia nzima ni ya kilokole ya kiimani sana. Katika kulelewa kwetu tumekuzwa katika misingi ya kiimani, kama kawaida ya familia za kilokole zilivyo.

Nikiwa std 5 ghafla nilijikuta naichukia mienendo na misingi ya kidini. Ikawa nafosiwa na nguvu ya familia kwenda kanisani, kuabudu na kuhudhuria maombi mbalimbali kwa masimango na kelele za kutosha ingawa moyoni nilkuwa sitaki kabisa. Kila kitu nikawa napingana nacho hapo maskani nikajichukia kwanini nilizaliwa kwenye hii familia. Ulkuwa ni utumwa kwangu niliona kama nipo gerezani. Faza alitumia nguvu kubwa kunirejesha kwenye msingi nisipotee ila wapi. Alijua pengine makundi yananipotosha ila sikuwa hata na rafiki.

Nilipoanza kidato cha kwanza niliamini ndo utakuwa mwisho wa shida zote maana ningekua mbali na familia.Faza alizingua nisipelekwe boding kuhofia ningepotea jumla maana dalili zote za kupotea zilishaonekana.basi nikanunuliwa bike ya go and return home hapo ndo wazee waliona sahihi ili wawe karibu na Mimi.nikawachukia wazee wangu Nikaichukia shule na mwisho mwa mwaka wa kwanza nikafanya michakato ya kutoroka ikatiki nikaacha shule nikatambaa home bila kuaga. Niliandika ujumbe mfupi kwa faza kumuaga nikauweka kwenye bible yake niliamini atauona maana ndo kitabu anachokisoma mda wote. Hapo nilkuwa na umri wa miaka 13 tu. Nikatimkia majiji ya watu na kuanza maisha yangu nikiwa huru kabisa.

Ilipita miaka 13 bila ya kuwa na mawasiliano na ndugu yeyote. Nishakuwa mtu mzima sasa nimepambana sana kweli nimepitia mengi nimehaso vya kutosha na nimefikia Levo nzuri tu kimaisha. Mapema mwaka huu February nikaamua niende home kwa wazee wangu, nimewakumbuka sana ila kikubwa zaidi kwenda kujenga kajumba ka kufikia. Nilpokelewa home fresh ingawa nilkuta familia imehamia kijiji kingine kwa ajili ya shughuli zake faza za kihubiri maana ni pastor mkubwa tu. Familia ilifrahi kuniona baada ya muongo mzima maana walkuwa wakiniombea miaka yote niwe salama na kweli maombi yalijibiwa.

Raundi hii nilkuwa rafu zaidi kichwani nina dredi mwili mzima umejaa tattoo nilkuwa sifananii na yeyote katika familia hiyo sio kaka wala sista ingawa wana familia zao.madogo kuniita kaka hawawezi naonekana mhuni sana. ilkuwa ni aibu kubwa kwa familia ya pastor kuwa na kijana wa dizaini yangu. Hiyo ndo life style yangu ninavyoishi. Kibaya zaidi kwao napiga dumu ( bangi) faza alinikuta siku moja nikiwa nanyonya moto kuweka akili sawa. Faza alinihusia niachane na mambo ya kidunia niishi katika kweli ya mungu nilimjibu siwezi kuacha hayo maswala ndo maisha yangu na ndo sababu ya Mimi kwenda kuishi mbali nao kuepusha kero. Mzee analia sana akifa atamjibu nini mungu wake juu yangu je shetani amepata ushindi kwenye hii vita? Kila mtu na moyo wake aniachie msalaba wangu nilmjibu hivo.

Sifanani siendani wala sichangamani na yeyote katika familia hii ya kilokole najuta kwanini nilizaliwa kwenye hii family. Nimesharudi Dar baada ya kutimiza kile kilichonipeleka home licha ya aibu yote nimejenga nyumbani nzuri tu na nimepewa heshima yake. Mi ni mhuni mwenye akili ya maisha. Yote ya yote faza kafarijika kuona nimefikia hatua nzuri kimaisha ingawa kichwani elimu sifuri maana kuna washikaji wa rika langu bado wanaishi na kula makwao ilhali Mimi nina mji wangu dar watu wananipa kodi ya pango. Namwamini mungu wangu ila hiyo life style yangu.
 
Wat a gwan rastaman.

Kuna mawilo tu duniani.
1)Kuishi kwa kujifurahisha na kukosa baraka na ufalme wa Mungu

2) Kuishi kwa kutopenda wala kufuata mambo ya kidunia na kujiwekea hazina yako kwenye uzima wa milele.

Hakuna kitu cha katikati hapo,ni moja tu kati ya mawili.

Enjoy maisha uliyoyachagua Bro.
 
Wat a gwan rastaman.

Kuna mawilo tu duniani.
1)Kuishi kwa kujifurahisha na kukosa baraka na ufalme wa Mungu

2) Kuishi kwa kutopenda wala kufuata mambo ya kidunia na kujiwekea hazina yako kwenye uzima wa milele.

Hakuna kitu cha katikati hapo,ni moja tu kati ya mawili.

Enjoy maisha uliyoyachagua Bro.
Nakubali faza
 
"Nikiwa std 5 ghafla nilijikuta naichukia mienendo na misingi ya kidini"

Majibu yote yako hapo, Itafutie ufumbuzi hio sentensi.

Vyote ni sababu ya kusudi lillo ndani yako na "ushuhuda" wa mzee wako.
 
Back
Top Bottom