Hayo uliyoafanya kwanza ni makosa ya kibinadamu.
Kitendo pekee cha kujuta kufanya kosa, ndivyo ustaarabu unavyoelekeza kufanya na Mungu anapenda.
Ungama na kujuta dhambi hiyo kwa Mungu, ndiye atakayekusamehe na kuendelea kukubariki, si binadamu.
Kusema uende kwa jamaa ukaombe msamaha, hilo jambo halifai maana jamaa ataona hiyo ni gia ya kumpoza, ndipo ghadhabu na hasira zake zitapanda maradufu.
Hakikisha unapomuungamia Mungu wako, hilo jambo usilirudie kamwe, si kwa hao tu, bali kuingilia ndoa yoyote usije kufanya tena.
Mambo ya hawara yako na ndoa yake, wala usisumbuke kuvifuatilia, iachie dunia itaamua mustakabali wao, wewe endelea na mambo yako mengine.