Najuta sana kuharibu ndoa ya huyu jamaa. Nitumie mbinu gani kumuomba msamaha?

Duh wewe
 
Hayo uliyoafanya kwanza ni makosa ya kibinadamu.

Kitendo pekee cha kujuta kufanya kosa, ndivyo ustaarabu unavyoelekeza kufanya na Mungu anapenda.

Ungama na kujuta dhambi hiyo kwa Mungu, ndiye atakayekusamehe na kuendelea kukubariki, si binadamu.

Kusema uende kwa jamaa ukaombe msamaha, hilo jambo halifai maana jamaa ataona hiyo ni gia ya kumpoza, ndipo ghadhabu na hasira zake zitapanda maradufu.

Hakikisha unapomuungamia Mungu wako, hilo jambo usilirudie kamwe, si kwa hao tu, bali kuingilia ndoa yoyote usije kufanya tena.

Mambo ya hawara yako na ndoa yake, wala usisumbuke kuvifuatilia, iachie dunia itaamua mustakabali wao, wewe endelea na mambo yako mengine.
 
Nashukuru kwa nasaha zako mkuu..nimeuchukua huu ushauri wako
 
Hizi comments za humu zinafurahisha sana. Eti wanaume wote walio comment hapa kasoro mzabzab hawajawahi kabisa kula mke wa mtu, leo wana mkana mwenzao. Maajabu haya

Kama ni wasaliti na wana comment hivyo; then kwa mtu mmoja mmoja mwenye Tabia hiyo anatakiwa ajue kwamba ni hatari sana na hata wanaofanya hivyo sio jambo wanalolifurahia!
 
Acha kulalamika mwamba kakuachia umuoe maana kaona mnaiba iba sasa ndo muda wenu wa kufaidi mapenzi kwa raha zenu.
Wanawake huwa hawajifunzi, mwanaume atakupenda ukiwa kwenye ndoa yako ukiachika hata yeye hakutaki tena.
Kama amem-cheat mumewe tafsiri yake ataku-cheat na wewe. Mwanaume gani anayajielewa yupo tayari kuoa malaya? πŸ˜‚
 
Hizi comments za humu zinafurahisha sana. Eti wanaume wote walio comment hapa kasoro mzabzab hawajawahi kabisa kula mke wa mtu, leo wana mkana mwenzao. Maajabu haya
The issue kwangu mie ni kwamba ushakula mke wa mtu, ameshaachika eti anajifanya anajutia mara anasema namba ya yule mwanamke hana. So angekuwa nayo inhekuwaje? He is not sorried for what he did kula tunakulaga lakini haya majanga ayakitokea unapaswa kuwajibika . Sasa anataka kuomba msamaha wa nini jamaa keshamuambia amuie yeye so its for him to decide sio kujifanya anajutia wakati anajua umalaya waliokuwa wqnaufanya. Take responsibility na ashukuru hajaliwa .
 
Kama ni wasaliti na wana comment hivyo; then kwa mtu mmoja mmoja mwenye Tabia hiyo anatakiwa ajue kwamba ni hatari sana na hata wanaofanya hivyo sio jambo wanalolifurahia!
Leo wote ni watakatifu wanamshangaa mwenzao kwa kufanya upuuzi
 
Ni kawaida kujuta baada ya madhara kutokea.
 
Jamaa kafanya jambo la maana sana huwezi kaa na mke msaliti.
Kwa kweli inauma sana kuharibu maisha ya watu angalia watoto wa huyo dada hapo wataishi maisha ya shida kisa nyege zako za muda.
Halafu bado kila siku mnashinda visiting na makanisani,kusali ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…