Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Atasurvive tu sasa afanyaje kwani Mungu asamehi?Mungu Akupe mtihani wa kutoka nje ya ndoa?? Labda miungu.
kukubali dhambi na kuichukia ni hatua nzuri ya kutambua kosa mbele ya Mungu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Atasurvive tu sasa afanyaje kwani Mungu asamehi?Mungu Akupe mtihani wa kutoka nje ya ndoa?? Labda miungu.
Kusamehe sawa, lakini kusema hilo jaribu kapewa na Mungu, ni kuendekeza au kuhalalisha makosa...Atasurvive tu sasa afanyaje kwani Mungu asamehi?
kukubali dhambi na kuichukia ni hatua nzuri ya kutambua kosa mbele ya Mungu.
Yani mume wake alizaa nje.Uko sahihi katika hili Niko Kwenye mahusiano na mwanamke anaepitia hali km hii nimejitahidi kumkwepa kadri ya uwezo wngu baada ya kugundua alianzisha mahusiano hya baada ya kukutwa na hyo changamoto. kinachoshindikana kwke ni kuvunja tu ndoa c unajua ndoa za kikristu
😆😆Mtihani huo kwa wanaume si unajua kuchepuka ni kawaida ,sasa jaribu limemshinda kapata tatizo ..Na hilo tatizo ni mapito ya kidunia atakuja kusahau.Kusamehe sawa, lakini kusema hilo jaribu kapewa na Mungu, ni kuendekeza au kuhalalisha makosa...
Zaidi ya kwako, hata chakula shida, wake zao ndo bread winners. Hata kuwalea hao ndugu zetu wa nje hawawezi, hawana chochote, kumekauka kau....Kiliwatokea kama mimi hivi
Ndio mumewe alizaa nje ya ndoa na alimleta mtt akiwa na miaka zaidi ya tisaYani mume wake alizaa nje.
Pole sana, siku jaribu kumtoa out na mkiwa huko mweleze namna unavyo umia kwa tendo lako baya, pia msifie jinsi alivyo mke bora na ni yeye pekee unayemtegemea kama msaidizi wa familia kwa faida ya watoto wenu na jinsi unavyo umia kumkosa.Kaka kinachoniuma ni ule ushirikiano wa mwanzo ambao ulikuwa unaleta matunda kwenye familia , yani mafanikio makubwa , tulikuwa na ndoato kubwa Safi sana, Amini bro tulinunua kiwanja ili baadae tushishe mjengo mmoja.
Hayo yote yamekatika kaka,
Kupambana najitahidi sana mimi binafsi coz mimi ndio Baba wa famialia.
Ila kokosa ushirikiano hata wa mawazo kutoka kwa mke inaniuma sana.
Maana niliona mwanzoni mawazo yake na ushirikiano wake ulivyokuwa na mafanikio.
PoleHabari,
Ngoja nianzia mbali kidogo mpate kuelewa mke wangu ni mtu wa aina gani. Na ilikuwaje mpaka nikazaa nje.
Mimi na mke wangu tulikutana kwenye kongamano la injiri kipindi namaliza chuo yeye alikuwa anasoma chuo kingine tofauti na chetu.
Ni mtu mpole sana niseme ukweli, na anavaa mavazi ya heshima sana, Nilitengeza nae urafiki mpaka kuingia kwenye mahusiano. Niseme ukweli kipindi bado sijamuoa alikuwa ni mtu wa kupenda maendelea sana tena maendeleo ya kushirikiana.
Nilikaa nae kwenye mahusiano kama miaka 6 hivi kisha baadae tukaamua kufunga ndoa takatifu. Nikili kuwa kipindi tupo kwenge uchumba au niseme urafiki nilikuwa sijawahi mgusa kabisa kwani alikuwa ni mtu mpole sana. Mimi nilikuwa na michepuko yangu.
Kipindi tumeanza ndoa yetu, mke wangu yeye wala hakuwa Mchoyo mshahara wake yeye na pesa zake zingine alikuwa anaweka mezani, kitu hiki kilipelekea mpaka mimi kumuamini mke wangu na mimi nikaanza kuweka pesa mezani na kujadili nini cha kufanya tupate maendeleo katika familia yetu itakayokuja.
Mke wangu yeye ni mtu wa kuchakarika sana, na alikuwa anapenda kufanya sana biashara za kushirikiana na mimi mume wake. Kusema ukweli tulikuwa tunainuka kiuchumi kabisa maana nilikuwa naona hali inabadilika katika ndoa yetu hasa kiuchumi,
Nilipanga mengi sana na mke wangu , nilijivunia kuwa nae sana, niliona nimepata, japo ndo kipindi kile ilikuwa still changa.
Sasa baada ya mwaka 1 na miezi 2 mke wangu alibeba ujauzito wangu, ujauzito ule tangu dalili zilipoanza ulikuwa unamsumbua sana mpaka kutafuta mfanyakazi kusaidia kazi. Baada ya miezi kama 4 hivi ya ujauzito, sisi wanaume si unajua bwana kikombe kilijaa maji maana ni miezi kadhaa sijakutana na wife sababu ni ujauzito wangu ule. Nilikuwa navumilia tuu.
Sasa karibu na office yetu kulikuwa na kampuni moja hivi inaagiza vitu china na kuuza, mara nyingi vitu vya home nilikuwa nanunua pale. Kulikuwa na mdada mmoja nilizoeana nae, yeye alikuwa anapokea wageni na kuwaonyesha bidhaa. Kipindi cha ujauzito mazoea yaliongezeka mpaka kubadilisha namba na yule dada. Niseme tu ukweli kuwa niliomba sexy kwake, mimi kwangu kisingizio ni hali ya mke wangu. Nilianza kukutana naye maeneo ya nyumba za wageni tulikuwa tunatumia kinga. Mchezo humu uiliendela mpaka mke wangu anajifungua.
Mimi nikaona mahusiano na mchepuko yameisha tayari kwa sababu mke wangu ashajifungua tayari, nilisitisha mahusiano na mchepuko.
Ila kumbe mke wangu alikuwa anamshono ulitokana na kujifungua . Home na alianza kukalia maji yaliyochanganywa na dettol. Lakini baada ya mwezi mmoja alikuwa still anaumia wakasema anakinyama kimeota kwa hio arudi hospital akashonwe tena, mimi daaa.
Siku namsindikiza hospital nilipanga tena kukutana na mchepuko wangu. Nilivyomuacha hospital mke wangu jioni nilikutana na mchepuko wangu yule kwenye bar moja hivi. Sasa kipindi tunaondoka tukajikuta kunanyanduana kwenye gari kusema ukweli sikutumia kinga kabisa.
Nilimpeleka mpaka sehemu yeye aliposema nimuache, si kujua maisha anayoishi wala kwao sikujui.
Mke wangu baada ya kushonwa tena na kurudi home, mimi niliendelea kukutana na mchepuko kwa mwezi mmoja.
Siku moja aliniambia siku zangu sizione , daaa maneno yale nilishituka sana .
Nikamwambia mimi ni mume wa mtu akasema sawa ila ninahisi ni mjauzito. Mimi daa kusema ukweli hamu naye ilikata kabisa, nikaacha kukuatana nae tena. Nilifikili anatania ila siku zinavyoenda tumbo linatoka nje.
Mke wangu alivyopona tuliendela na maisha huku mchepuko anaujauzito wangu.
Maisha na mke wangu yalikuwa mazuri sana na mafanikio, mchepuko nilikuwa namtumia pesa za kumsaidia tuu, baada ya kujifungua hata mtoto sikwenda kumuona nilikaa kama miezi 5 hivi sikwenda hata kwao.
Mke wangu alikuwa hajui kabisa, mimi na mke wangu tulipanga vingi sana kuhusu maisha yetu, na mafanikio yalikuwa yanatimia kabisa kwani nilikuwa nayaona haya mlangoni na mengine yanangia kabisa.
Siku moja nikasema ngoja nikamuone kwake huko.
Aisee yule dada kumbe anaishi maeneo ya uswazi kabisa , yani ni mtahani kwa waswahili kabisa, waswahili wenyewe wale, nyumba mbanano hata pikipiki haipiti, mimi daa ndo nimezaa na huyu, niliumia sana tena sana ndo mwanzo wa kuanza kujuta, binti anaishi na mama yake tuu, na mama yake ni mswahili kweli kweli, yani hata home wakimuona watanishangaa sana.
Niliondoka na kurudi home namawazo sana huku mke wangu hajui, nilikaa kimya kama 2 years huku maisha na mke wangu yanaendela tukiwa tunakuwa kabisa kimaisha, mke wangu alibeba ujauzito mwingine , sikuchepuka kabisa, alifanikiwa kujifungua.
Baada ya miaka 2 tangu mke wangu ajifungue mtoto wa 2, mtoto wa mchepuko alikuwa miaka 4.
Mimi niliona daa sio vyema mtoto wangu kabisa yule aishi kule kwenye mazingira yale ya mtaani tena uswazi.
Kuna siku moja nilikaa mpaka 3 night kwa niliezaa nae. Daa mazingira ni hovyo sana na kelele nyingine, watu wanapita dirishani wanatukana matusi, maisha ya uswazi mnaelewa jamani.
Mimi niliona ngoja nimshirikishe mother, nipokee ushauri mama aliniambia ni kweli kama mazingira sio mazuri mchukue tuu ila atapata kuzoeana na wenzie mapema. Ila alinisisitiza sana kutengeza kwanza vizuri na mke wangu kuepuka madhara baadae. Niliongea mpaka na viongozi wa dini, kusema ukweli walinikaripia sana kwa sababu ni uzinzi nilifanya. Wakaniambia tuu ni damu yako ongea na mke wako tuu.
Mimi niliamua kwenda kufunguka kwa mke wangu, Nilitanguliza msahama na majuto kwa wife. Niliongea nae sana kuhusu mtoto wa nje na kuacha mahusiano na mama mtoto na ishu ya kumchukua mtoto tukae nae. Mimi sikufukilia madhara yatakayo tokea baadae sikufikilia hilo.
Mke wangu yeye alijibu tuu SAWA HAKUNA SHIDA NI MTOTO WAKO NA ATAENDELA KUWA WAKO TUU.
Kusema ukweli sikufikilia labda mke wangu atapata maumivu kiasi gani mimi nilivyoona yeye kakuabali mimi nikaona sawa. Nimwambia mother akasema kama kakubali sawa mchukue tuu ila kuwa karibu na mtoto.
Baada ya kama wiki nilimchukua mtoto japo mama yake alikuwa mgumu ila nilimchukua, na kuishi nae home.
Ila uwezi amini , ukaribu na mke wangu ulikufa kabisa , si ukaribu wa ndoa. Namaanisha ushirikiano kama Wanandoa.
Kipato chake sikukiona tena , mambo yote tuliokuwa tunashirikiana hasa ya kimaendelo na kiuchumi zilishia kabisa, ndani ya kama mwaka mmoja hivi niliona kipata ndani kimepungua kabisa, nilijua shida ni ile ishu, nilijaribu kukaa na kuongea nae tena sana, yeye anasema kuwa yeye yupo sawa hana shida. Nilijaribu kupambana mimi mwenyewe na maisha ila wapi ni vijipesa vidogo tuu ndo vinaingia ndani na mshahara wa kazini tuu.
Mke wangu yeye yupo na mambo yake haniusishi kabisa mimi.
Sometime nikawa najipa tuu moyo kuwa mimi ndo me ninatakiwa kurisha familia yangu, naamua kusonga mbele ila mambo yanaenda kawaida na mambo yangu mengi wanaanguka, mishe hacienda kabisa.
Natafuta ushauri kwa watu wa ninaokutana nao kwenye bar na sehemu zingine , wengi wanasema tuu ulizingua mara nyingi watoto hao tunawaacha kwa mama zao huko huko, kwani ulivyofanya hivyo umemwonyesha mkeo ushahidi kuwa ulimsaliti tena ukamletea home kabisa ushahidi. Wengi wanasema tuu usaliti unauma sana huyo mkeo anaumia mpaka kesho. Wananiambia tuu potezea kaka.
Ila ni kitu ninakijutia sana sio kwamba ninamchukia mtoto hapana nachukia ule uzinzi nilifanya .
Nilimueleza mother aliniambia tuu kama mtoto anaishi nae fresh hakuna shida kubali matokeo tuu.
Sometime natamani kuona siku zinarudi nyuma ila haiwezekani, Najuta sana maana naona maisha yamedrop sana. Yale maendeleo hakuna kabisa kama awali.
Sasa nina umri wa miaka 42,
Maisha napambana tuu mimi mwenyewe kama Baba wa familia sioni ushirikiano kutoka kwa mke wangu, lakini nimejipa moyo kuwa mimi ndo mwanaume nitalisha familia yangu. Ila kinachoniuma ni mahusiano wa kushirikiana na mke wangu yamekufa kabisa. NAJUTA SANA.
Marafiki zangu wengi wapo na mafanikio sana na wake zao nawaona hata jinsi wanavyoishi.
Kuna rafiki yangu mmoja wa karibu sana mwezi wa 3 aliingiza Toyota land cruiser LC300 GX la kwake na mke wake GX.
Huyu ni mmoja tuu wapo wengine wapo fresh sana , najua wapo hivyo kutokana na mahusiano na wake zao hasa ya kiuchumi.
Mimi hapa ni na ka harrier changu kimetengenezwa miaka 14 iliyopita naona hata aibu kuwakaribisha hata home friends wangu.
Na Hata kukutana nao tuu.
NB; JAMANI WANAUME WENZANGU TUTULIE KWENYE NDOA ZETU HASA TUNAPOPATA MKE MWENYE MIBARAKA KWENYE NDOA ZETU. NI MUHIMU SANA UNAWEZA UKAONA STORY ILA MWENZENU YAMENIKUTA.
SOMETHING NAJIRAUMU KUWA NINGEJUA NINGEMUACHA KWA MAMA YAKE NIKABAKI MUUDUMIA.
SOMETHING NAONA NILIKUWA SAHIHI KUMCHUKUA.
Sorry mimi sio mwandishi mzuri, naomba radhi kwa makosa mtakayo baini.
Kuna wazazi wanalelewa vizuri na watoto wa nje; na wengi huwa ni ma geniusSio vizuri kuzaa nje kaka.
Best Comment of the Thread. Case closed! Ukiwaogopa sana wanawake wanakuendesha haswa. Ishatokea hakuna haja ya kujuta! Hakuna kosaSijaona kosa lolote hapo,,yaani nimkane mwanangu kisa mwanamke? Hupaswi kujutia lolote. Labda kama wewe unategemea kipato cha huyo mwanamke kimaisha. Be a man.
Tupo wengi tuna watoto nje,
Cc Equation x
Kosa la jamaa,anamtegemea mke wake kiuchumi.Hujafanya kosa lolote na pia hongera sana ungekuwa mwoga ungetelekeza mtoto wako. Cha kufanya wewe pima kama mke wako anakupenda au hakupendi. Ukitaka kumjua kama bado anakupenda badilika.
chukua mtoto wako peleka kwa bibi. Nyumbani usikae wala nini hakikisha kwamba unapunguza attention na mke wako na usirudi home na ukisafiri usitoe taarifa just mjulishe mwamba leo sita rudi
Kama anakupenda hiyo ndiyo test atakuulizia na itamuumiza lakini akikupotezea my brother achana naye.