NAJUTA SANA: Nilizaa nje ya ndoa, mke wangu haniamini tena. Natamani siku zirudi nyuma

Wewe ndio umeoa huyo mwanamke au huyo mwanamke ndio kakuoa wewe??
 
Kaka hakuna maisha magumu na mabaya kama kutokuishi na baba yako mzazi. Suluhisho hapo ni kuwa mkweli. Mifano ipo kwa watu ambao hawajaishi na baba zao.

Utaficha mpaka lini na mtoto ana kuwa akijua baba yake yupo ila hamjali anamficha? Kama mwanamke anakupenda amini brother anakusamehe daima kutoka moyoni kumbuka wanawake ni ubavu wetu.

Mpe mke wako zawadi atasamehe na huyu mtoto wa nje atakuwa huru kujua ndugu zake. Pesa sio kila kitu maishani wala kumbukumbu ya pesa haikusaidii ukisha kufa. Bali kumbukumbu ya upendo na ukweli itakupa amani maishani mpaka kaburini.
 
Usimbembeleze sana mwanamke kama anazingua piga chini...
 
Ndio maisha uliyojichagulia, pambana.
 
Huo ndo uanaume pambana broo,.wanawake hata Kama hujazaa nje ya ndoa..ila Sio sababu ya kuacha makelele yao
 
Yaani ulikuwa na wewe unaweka mshahara wako mezani kila mwisho wa mwezi ili mpange mipango….!!? Kosa la kwanza

Miezi 4 mimba unaogopa kumpelekea moto mkeo….Au mkeo ndo master mind yy ndo anahamua aisee…!! Sijajua kama kuna madhara kusex kipindi she mjamzito..!!

Miaka 6 mpo kwenye mahusiano….afu mwanamke kashika dini,apa kuna shida some where
 
Kwanini huyo Mtoto usimpeleke kwenu kwa Mama'ko ili alelewe na Bibi yake?
Tena mama yake alimshauri kabisa ni damu yako umchukue ili azoeane na wenzie, duu mama mkwe kama nayeye ni mwanaume si mwanamke!
 
Sijaona kosa lolote hapo,,yaani nimkane mwanangu kisa mwanamke? Hupaswi kujutia lolote. Labda kama wewe unategemea kipato cha huyo mwanamke kimaisha. Be a man.
Tupo wengi tuna watoto nje,
Cc Equation x
Kwahiyo mke akichepuka apate mtoto ni sawa au!
 
Wewe kwa uandishi huu utakuwa mke wa pili [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Injiri = injili, kurisha = kulisha, najiraumu = najilaumu. HII NI CHAI PROMAX. Mwanamke kabla hajajifungua ndo huwa anataka sana kutiana hasa ile miezi ya mwanzo. Sasa wewe hii chai yako kwamba alivyopata tu mimba ukaacha kufanya nae tendo ni ya wapi? Ungesema karibu kabisa na kujifungua na mara baada ya kujifungua ungeeleweka.
 
Matatizo ni mawili tu hapo.

1. Kumtegemea mke katika kipato
2. Kuwa vuguvugu na kukosa akili ya mahusiano. (Walokole huwa na hili tatizo)

Suluhisho ni moja tu.
1. Kuwa mwanaume mwenye uwezo wa kujisimamia kifedha na kimsimamo.

Kila la heri.
Halafu ushauri unachukua kwa mama
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…