Najuta zaidi ya Tsh. 500m nimezika katika majengo, mtaji wa kufanyia biashara umepungua pakubwa sana

Najuta zaidi ya Tsh. 500m nimezika katika majengo, mtaji wa kufanyia biashara umepungua pakubwa sana

Kama nmeelewa hii ni taarifa unatoa sio kuomba ushauri si ndio? Hongera kwa hatua kubwa mwanawane

Tukutane sheli.
 
Sasa mkuu hapa nimebaki namtaji wa 150m..nawaza biashara zingine kabisa zitakazo run kwa pesa hiyo ikakua faster nirud ktk game vizur
Nunua gari jipya (lorry) la mchina aina ya FAW kwa sh 90m halafu piga mishe za kusafirisha mizigo. Baada ya mwaka mmoja utakuja kunishukuru.
 
Ukinunua kiwanja ama ukajenga nyumba hela ile wala usiwazie sana fanya kama ulipoteza ama ulipata hasara.Hakuna kitu kinalipa km kiwanja.Kiwanja nilicho nunua mwaka 2012 kwa milioni mbili leo naweza kiuza kwa million 30 ama zaidi kama ulilenga sehem nzuri.Sijui unapata wapi hata mawazo ya kulalamika wakati unakiri mwenyewe hizo sehem ulizo jenga mbeleni utapiga mpunga wa maana.
 
Maisha hayana formula Moja Mimi nimechoma zaidi ya milioni 300 kwenye maproject halafu zikabuma najuta Bora ningewekeza kwenye mijengo nilambe kodi huku pesa yangu naiona.
Kwenye project ikipotea imepotea hio
 
Sio kila project inalipa halafu elewa project au biashara ni Giza ni rahisi kwenye karatasi na sio field
 
Hio m 500 miaka 10 ijayo itakuwa bilioni moja na point.
Majengo hayashuki thamani biashara inashuka thamani due to competition na technology
 
Umewahi fanya biashara? Au project yeyeto ni rahisi kama haujawahi Fanya.
Wazee wanastaafu wanalamba m 300 zinapotea kwenye project biashara wanakufa pressure.
Hadi utoboe vikwazo ni vingi uvishinde vyote kuna wachawi,madalali,mda,magonjwa,wezi,serikali,nk wote wanatolea macho ulichowekeza,mtu akitoboa bongo kwa akili yake kama sio freemason,au fisadi serikalini mpe maua yake
 
Mkuu kwa saa hizi nikiuza hayo majengo nitakua kama napata hasara tu maana Yako sehemu potential sana kwa baadae, baada ya miaka 10 pesa yake ni ndefu mno nikisema nipauze.
Basi hujaaribu kitu... Kuwa tu na Subira na kiasi ulicho nacho kisimamie tu vzr
 
Mkuu kwa saa hizi nikiuza hayo majengo nitakua kama napata hasara tu maana Yako sehemu potential sana kwa baadae, baada ya miaka 10 pesa yake ni ndefu mno nikisema nipauze.
Sasa unalalamika nini boss? Shukuru hata umeinvest kwa real estate..tujifunze kushukuru kuna watu hata chumba kimoja hawana ..nilichojifunza mwaka 2024 ni kusema asante mara nying unaongezewa pale padogo.
 
Never give Mkuu, 2-3 years back na mimi nilikuwa budget yangu ni buku 1 kwa siku, hapo naishi home maisha magumu sana, ila huwezi amini leo hii 2024 na mimi Mungu kashusha neema ya kuhesabu angalau 10M plus… naamini kwa mwendo naenda nao kabla ya 2030 ntakuwa nimefika huko sababu hata umri bado unaruhusu.
SAWA MKU, MAPAMBANO YAENDELEE
 
Mzee Bora Umejenga Hiyo Ni Long Term Investment, Biashara Huwa Zinapanda Na Kuporomoka. Hiyo Mijengo Ni Life Time Watoto Na Wajukuu Wataisimamia Ukiwapa Msingi Mzuri. Shida Yetu Ni Tamaa Ukiambiwa Biashara Inalipa Tunakurupuka. Tuache Tamaa Hata Kama Mijengo Inalipa Kidogo Lakini Ni Uhakika. Tulizama Moyo Wako. TAMAA MBAYA
 
Ni kweli usemalo ila kama pesa hiyo nisingewekeza ktk majumba Leo hii ningekuwa na uwezo wa kujenga majengo ya thamani hiyo maana mzunguuko wa biashara ungekuwa mkubwa sana sababu ya mtaji ni mkubwa na faida ingekua maradufu.
Wakati mwingine kujenga ni kuzik hela/mtaji
 
Hivi watu wenye pesa nyingi kama wewe nao huwa wanazurura humu jamiiforums? Najua humu tupo hohehahe hata kama tuna elimu ila pesa hatuna maisha yetu ungaunga mwana tu vitoto viende shule tulipe kodi ya nyuma makazi na nyumba biasha, tubadili mboga home mara mojamoja, kiofisi cha kiaina basi.
 
Habari wakuu, nawashauri msifanye makosa kama niliyofanya, ukipata pesa wekeza katika biashara na si majengo. Fursa nyingi zimenipita kutokana na mtaji kuwa mdogo sababu ya sehemu kubwa ya faida nilipokuwa naipata haikurudi kuwekeza katika biashara zaidi.

Matokeo yake wakati fursa naziona Sasa mtaji hautoshi bidhaa zingine nashindwa kuzinunua sababu mtaji hautoshi, sehemu ya faida haikurudi ktk biashara zaidi ya kwenda kwenye maujenzi ambayo hayaniingizii pesa ya maana tofauti na ambayo hizo pesa zingekuwa katika biashara.
Waongea kinyumeche...u maMkoa je?
 
Hivi watu wenye pesa nyingi kama wewe nao huwa wanazurura humu jamiiforums? Najua humu tupo hohehahe hata kama tuna elimu ila pesa hatuna maisha yetu ungaunga mwana tu vitoto viende shule tulipe kodi ya nyuma makazi na nyumba biasha, tubadili mboga home mara mojamoja, kiofisi cha kiaina basi.
Wengine twamiliki meli na tumo humu 👍
 
Back
Top Bottom