Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Akichanganya na za kuvua nanihii, labda zitakuwa nyingi kidogo..........lakini ataweza kwenda kubadilisha damu kila mara kama mwenzake?

Bigirita: Ebu fafanua zaidi hapo maneno ambayo nimeweka rangi nyekundu!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mungu wangu Sipati picha kabisaaaaaaaaaa..............
 
Mi nadhani wangedai hela zao mapema kabla ya mwisho wa kampeni, wasije wakajuta huko mbele.........................
I am just trying to think, if kwenye uchaguzi MZEE akatoswa................., kweli hela itatoka?
Chukua Chako Mapema; si ndo slogan yao?
 
Jamani Nakaaya ametumia haki yake kama mtanzania. Tumwache aende!!

Mi sishangai maana niliyoyaona kwa wanafunzi wa UDOM ni mabaya zaidi!! Hii ni kama MV MAPENZI. Nahodha kachupa baharini sisi safari inaendela!!!:horn:
 
Ishu si kuwauma watu!...tunatumia uhuru wetu wa kutoa mawazo!

Lakini inashangaza kwa mtu ambaye amejenga trust na heshima overtime ndani ya CHADEMA, anakuja kurubuniwa kipindi cha kampeni!...

Mi nilidhani zile nguo za CCM zinapendwa na watu wa class fulani, kumbe hata watu wa aina ya Nakaaya wanazitolea povu la mdomo, hadi kufikia kuuza utu...

So far CCM wenyewe washamjua kuwa huyu ni mtu wa fedha, so watakaa wakijua jinsi ya kumtreat, na hawawezi kumpa nafasi zenye siri, maana 'in no time' atawavuruga!

Popo si ndege...Popo si Mnyama! ( .... just something in-between!..huh)

Ningeshukuru Kama mngenipa mwanga wa kunionyesha kile alichofanya hadi kuonekana mtu wa maana sana au wa hadhi ya aina yake.
 
Njaa jamani akale wapi?
Atleast she has shown her true colours
 
Hata wakati wa ukoloni walikuwepo Watanzania waliowavi=unja moyo watanzania wenzao ktk mapambano ua UHURU
Pole Nakaaya kwa kujiunga kwenye msafara wa MAMBA
 
Nadhani ameahidiwa kuwa meneja wa ule mradi wa mastering studio ya wasanii wa shs milion hamsini
 
Humjui huyo jamaa? huwa ni mkurupukaji na mropokaji na mdini

Mchungaji sasa mbona tunakoseana heshima. Sasa huo udini wangu umetoka wapi? And I apologize kama unaona naropoka. I try to be objective. And in that lens, mie naona chama cha demokrasia na maendeleo hakina watendaji ambao wako serious. And have incompetence across the board.
 
A beg a beg a geg....Nakaaya ni msomi? Kasoma wapi?

Selemani umekurupuka...au kujua kusoma na kuandika kiingereza ni usomi???

Haya basi mdau, nimekosea. Nakaaya hana usomi wowote. Hoja ya msingi inabaki pale pale.

So, Rais Dr. Slaa, Makamu wa Rais Said Mzee Said, and Waziri Mkuu DJ Mbowe. Hamko serious nyie. Mtapiga makelele humu ndani, lakini watu wenye busara na upeo wa kuona mbali hawawapi kura wala nchi. When you become serious, tutawapa kura. Mnatuwekea wagombea mamluki, mnachukua vibaraka wa CCM (Shibuda kamchangia Kikwete laki 2 majuzi tu hapa, leo mnamuona mkombozi wenu), mnachagua mgombea mwenza mchovu, mnapoteza muda kuongelea Mama Salma na Kinana badala ya kutuambia mtatoa vipi nchi kwenye umasikini. Vijana (Nakaaya) wameingia Chadema wakaona uozo wameondoka.

Jipangeni, mkiwa serious tutawapa nchi.
 
Mchungaji sasa mbona tunakoseana heshima. Sasa huo udini wangu umetoka wapi? And I apologize kama unaona naropoka. I try to be objective. And in that lens, mie naona chama cha demokrasia na maendeleo hakina watendaji ambao wako serious. And have incompetence across the board.

Sele

Remove lids from your eyes! Be objective. Got brains sawa?
 
ndio hivyo kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo, mapinduzi kazi ngumu wengi wanayakimbia
 
Sishangai kwa Huyo binti kuhamia ccm, Mwaka jana nilikutana nae nje ya tz. she is not as most of us think she is 'mentally'! Thanks to the guidences she is getting from her family, definetly angegombea kwenye jimbo langu nisinge mchagua. Kwa ustawi wa Chadema nawapa hongera. Unaweza imba wimbo 'Sofia si.. anakuzimia' na watu wakakuona upo ndani ya penzi kweli kumbe wimbo tu tena umetungiwa. Hongera Nakaaya
 
Nilishangazwa sana na kitendo cha Nakaaya kuamua kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama hicho. Nakaaya kwenye Magwanda ya CHADEMA nilikuwa namwona kama nuru ya vijana wenye mioyo ya kimapinduzi na wenye kutakia mema Tanzania yetu. Baada ya kutafakari sana nilimegundua nilikuwa nakosea, Nakaaya ametumia haki yake na maamuzi yake lazima yaheshimiwe. CHADEMA ni taasisi na si mtu ama watu, wengi watajiunga na wengi wataondoka ila chama kitakuwepo na kitaendelea kuimarika kwa wale wote wenye moyo na itikadi za CHADEMA.

Mapinduzi ya kweli yanahitaji askari wenye moyo na wale wenye uwezo wa kujitoa muhanga. Sasa kama unapewa ice cream na unaweza kutoa siri wapi alipojificha jemadari mkuu wako ni hatari sana! Heri ukaachana na mapambano kabla hujasaliti. Nimeonana na Nakaaya mwanzoni wa mwaka huu nikampongeza kwa wimbo wake wa Mr Politician tukaongea mengi, mipango yake ya music na siasa. Anajiamini sana hana haiba za wadada wengi wa Kitanzania, anapenda ishi maisha yake. Siku ile alikuja na ML class Mercedes Benz nyeusi, Mchungaji nikaweka heshima. Sijui kama ni la kwake ama alikuja safisha nyota!

Kama kweli Mil 30 alizoahidiwa mwisho wa Kampeni kama wale wasanii wenzake, walio kwenye kampeni za CCM, ndicho hasa kilichomtoa CHADEMA basi siasa hatoziweza maana akipewa dhamana yuko tayari kuuza hata uhuru wetu.

Kuwa Upinzani kunahitaji uwe na moyo wa Simba, si kila mtu anaweza. Mchungaji nimejitoa muhanga niko tayari hata kujilipua uongozi wa imla na kikoo wa CCM ufikie mwisho. Nimalize kwa kumpongeza sana sana kwa uamuzi wake wa kwenda kwenye kundi la ndege analofanana nalo rangi! Sababu anajua udhaifu wa kiutendaji wa Mwenyekiti wake mpya basi kura yake bado tunaihitaji CHADEMA.

Vote for Slaa

Wenu Mchungaji

Rev Masa

Peace with you all

Mchungaji i can feel SADNESS Between your lines.. nikama unampa farewell speech.. bado muna mpenda na kumthamini !! yaani nikama chadema alikuwa undergraduate kaja ndani ya chama cha mapinduzi kufanya postgraduate !! Inshallah atafanya vizuri sana na atakuwa mwanafunzi mwema kwani naamini chadema kulikuwa na walimu wazuri!:becky:
 
Mchungaji i can feel SADNESS Between your lines.. nikama unampa farewell speech.. bado muna mpenda na kumthamini !! yaani nikama chadema alikuwa undergraduate kaja ndani ya chama cha mapinduzi kufanya postgraduate !! Inshallah atafanya vizuri sana na atakuwa mwanafunzi mwema kwani naamini chadema kulikuwa na walimu wazuri!:becky:

Duu hujamsoma mchungaji! Haya mkuu kanyaga twende
 
Back
Top Bottom