Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Ni Dr Slaa tu ambaye wamemshindwa! Yeye huomba sahihi 3, ya kwako, ya yule aliyekutuma, na Yesu! Nakaya ni mganga njaa kama watz wengi tulivyo na kwa sababu ya njaa zetu tumekuwa target ya siasa chafu za CCM.

Kitu kizuri katika hilo ni kwamba wananchi wanafahamu fika kwamba huo ni usanii wa CCM, hata mtoto mdogo huwezi kudanganya! Unarudi CCM kipindi cha Kampeni kwa jema lipi walilofanya? Kwa sela zipi? Next tutawategea mtego! watanasa tu!!!!!
 
inasikitisha sana kwakweli....

pole yake nakaaya!....
NJAA MBAYA SANA.

sikutofautishi na KAHABA ''kisiasa''
 
CHADEMA ni taasisi na si mtu ama watu, wengi watajiunga na wengi wataondoka ila chama kitakuwepo na kitaendelea kuimarika kwa wale wote wenye moyo na itikadi za CHADEMA.

Mapinduzi ya kweli yanahitaji askari wenye moyo na wale wenye uwezo wa kujitoa muhanga.


Asante REV tumekusoma, tunatafakari, tutachukua hatua
 
Huyu Nakaya huyu!???? Duh, Zitto upoooo? nakumbuka sana kuwa unamkubali sana huyu dada na yeye anakukubali kama Mwanasiasa makini na anaikubali Chadema, sasa kumetokea nini? hebu Zitto tufumbue macho kinachoendelea
 
nilishangazwa sana na kitendo cha nakaaya kuamua kukabidhi kadi ya chadema kwa mwenyekiti wa ccm ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama hicho. Nakaaya kwenye magwanda ya chadema nilikuwa namwona kama nuru ya vijana wenye mioyo ya kimapinduzi na wenye kutakia mema tanzania yetu. Baada ya kutafakari sana nilimegundua nilikuwa nakosea, nakaaya ametumia haki yake na maamuzi yake lazima yaheshimiwe. Chadema ni taasisi na si mtu ama watu, wengi watajiunga na wengi wataondoka ila chama kitakuwepo na kitaendelea kuimalika kwa wale wote wenye moyo na itikadi za chadema.

Mapinduzi ya kweli yanahitaji askari wenye moyo na wale wenye uwezo wa kujitoa muhanga. Sasa kama unapewa ice cream na unaweza kutoa siri wapi alipojificha jemadari mkuu wako ni hatari sana! Heri ukaachana na mapambano kabla hujasaliti. Nimeonana na nakaaya mwanzoni wa mwaka huu nikampongeza kwa wimbo wake wa mr politician tukaongea mengi, mipango yake ya music na siasa. Anajiamini sana hana haiba za wadada wengi wa kitanzania, anapenda ishi maisha yake. Siku ile alikuja na ml class mercedes benz nyeusi, mchungaji nikaweka heshima. Sijui kama ni la kwake ama alikuja safisha nyota!

Kama kweli mil 30 alizoahidiwa mwisho wa kampeni kama wale wasanii wenzake, walio kwenye kampeni za ccm, ndicho hasa kilichomtoa chadema basi siasa hatoziweza maana akipewa dhamana yuko tayari kuuza hata uhuru wetu.

Kuwa upinzani kunahitaji uwe na moyo wa simba, si kila mtu anaweza. Mchungaji nimejitoa muhanga niko tayari hata kujilipua uongozi wa imla na kikoo wa ccm ufikie mwisho. Nimalize kwa kumpongeza sana sana kwa uamuzi wake wa kwenda kwenye kundi la ndege analofanana nalo rangi! Sababu anajua udhaifu wa kiutendaji wa mwenyekiti wake mpya basi kura yake bado tunaihitaji chadema.

Vote for slaa

wenu mchungaji

rev masa

peace with you all
ccm bwana hawa wasannii wakiwa upinzani wanaitwa wahahuni wavuta bangi na malaya lakin si ukiwa ccm
 
sielewi kwa nini chadema iwaume sana kwa huyu mtu kuondoka ........................au alikuwa na nguvu kuliko wengi tulivyodhani?

Sidhani kama imewauma watu na sidhani ama ana significance yoyote kwa chadema hasa ukizingatia hata kwenye musiki alikua bado ni rookie, kwangu mimi naona anajadiliwa kama akina kafulila alivyofanya, na wengi ukiwasoma wamegundua kwamba her move was to rescue her career more than a political path which she thought would promote her image

I hope kutoswa na lebo ya kumechangia kumshindisha njaa na ikabidi aje akubali kipande cha papa hata kama hakijaoshwa
 
wapambanaji hatuoni wa kushtuka
ufisadi ni kama umalaya=una sura nyingi sana. Tutaona na kusikia mengi
 
. Nimalize kwa kumpongeza sana sana kwa uamuzi wake wa kwenda kwenye kundi la ndege analofanana nalo rangi! Sababu anajua udhaifu wa kiutendaji wa Mwenyekiti wake mpya basi kura yake bado tunaihitaji CHADEMA.
Kheeee heeeee heeeee!
 
Ongera dada Nakaya kwa kuamua kurudi kwenye chama chako ukipendacho. Maana kuikomboa TZ ni vita ngumu sana na vita yenyewe inahitaji wenye moyo wa uzalendo na wapiganaji wa ukweli wenye moyo wa kufia nchi yao. Nenda dada nenda mapinduzi ni kujitoa na si kuimba "Mr Politician" ndio kuthibitisha kuwa wewe ni mpiganaji wakweli. MWENZETU umeshayaona maisha bora ndio maana umrudi kuungana na watoa maisha bora, tunao sota tunaendelea na mapambano Nenda Dada, Kweli ni uchungu kumpoteza mpiganaji vitani, ni uchungu sana mpiganaji anapofia mstari wa mbele au anapokamatwa mateka pale mlipozidiwa ktk mapambano, hila inasikitisha na kusononesa lakini haiumi pale mpiganaji mwenzenu anapojisalimisha mwenyewe kwa adui. kujisalimisha ni ishara ya kushindwa mapambano, kukata tamaa au usaliti je dada uko katika kundi lipi hapo? Nenda dada vita hi ngumu inaitaji wale walio kulia mlo mmoja na wanao endelea kuishi kwa mlo mmoja au bila mlo wa siku. Vita hii si ya ma Miss na Wanamziki wanaoimba kujirusha na kula bata utazani wapo kwa Obama vita hii ni ya wana hiphop wa kweli SUGU, MKOLONI, KALAPINA, AFANDE SELE nk. Dada nenda nenda Dada warembo kama wewe wanaukwa UDC ktk awamu ya JK kajaribu na wewe mwenzako VICKY KAMATA kapewa maisha BOT, kapelekwa kusoma Masters kiwanja na sasa anapewa Ubunge kisa kuimba "anawake na maendeleo" na "JK ni kiongozi mfano wa mfalme Suleiman" Nenda Dada CCM nafasi za UDC bado zipo nenda tumekupoteza lakini mapambano yanaendelea wanawanchi tutashinda bila kujali lini? Ila ukombozi umekaribia Nenda Dada nenda Kawape salam wote waambie wototo wa uswahilini na watoto wa wakulima wamechoka "MACHOZI, JASHO NA DAMU" vyote vyao mvua yao jua lao lakini haturudi nyuma mapambano yanaendelea tunafuata usia wa mwanamapinduzi wa kweli duniani hayati CHE GUEVARA kuwa damu yake iwe mbegu ya kuzaliwa wanamapinduzi wengi DUnianai NENDA dada msalimu RIDHIWAN, JANUARY, BENNO MALISA, ANGELA MKWIZU na vijana wengine wa UVCCM waambini sisi bado tunataabika katika nchi yetu wenyewe lakini hatukubali kuwa mateka wa BABA Ridhiwan
 
Huyu Nakaaya si ndo aliwahi kusema kwamba "laiti kama baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere angekuwa hai basi angehama CCM na kwenda CHADEMA" vipi mbona kama anakula matapishi yake tena mbele ya kadamnasi ya watu!!

Kweli njaa mbaya..!! Loh
 
Ndugu zangu wachukia-CCM, alichokifanya huyu mwanadada ni kitu bora sana kwa CHADEMA kwa sababu and i hate to say this, lakini wamo wengi sana wa aina yake wanaojivisha magwanda ya CHADEMA. Inatisha sana kufikiria scenario ya wabunge wa CHADEMA ambao wanapewa mshiko na akina Rostam ili wamchague Chenge kuwa Spika wa Bunge.......hapo ndio utakuwa mwanzo wa Bunge la kisanii. Tuombe Mungu hilo lisitufike na tupate wabunge wa upinzani wenye moyo wa kweli wa kujitolea.
 
Njaa inawatuma watu vibaya! bahati mbaya watu dizaini hii hawana aibu, cku akiona upepo unavuma vizuri alikotoka atarudi, uzuri bado kitambo kifupi.
 
Haki ya nani aisee! Hutambui umuhimu wa huyu binti kwa jamii?! Naamini ndiyo maana mnapiga piga kelele tu kutwa nzima hapa bila points. Huyu binti anaweza infuence watu zaidi ya 1000 kubadili mwelekeo. Unaelewa lakini maana yangu? Uliza nikupe maelezo? Mwambie na mwenzako mlionaye dark city. Kama hamtaki, endeleeni na jamvi la style yenu

.
Nnani kakwambia kwamba wa kushawishiwa anaweza kushashi? Would you p/se keep quite!!
 
Rev Masanilo, Asante kwa post.

Umenena yote vema. Wanafiki watajulikana vema kipindi hiki. Na ni vema wakajitoa mapema.
 
Nenda Nakaaya..Maisha mema Kwenye Ulimwengu wa Mafisadi..! Chadema ni zaidi ya Nakaaya na any one else..daima Tutasonga...!
 
Pamoja na kuwa ametumia uhuru wake wa kuamua ,lakini amekuwa influenced na ufisadi. Tunamshangaa alivyouza uhuru, dhamira , na nguvu zake dhidi ya utawala mbovu kwa vipande vichache vya fedha.Kwa hakika amekuwa looser ...loose point ... na huko alikoenda ndio watamtumbua vilivyo na sio aajabu huyo Petro wake aka. Mchumba akatema mzigo maana mafisadi hawana waachalo hasa kama umeshaonyesha tabia kama hizo za kidada poa.

Mwisho wa siku atakuja juta kama yule Yada Askari Yote. Niliwahi kusoma hapa eti alidhulumiwa mkataba wa sijui South Africa or what,kwa simple reason kuwa jamaa walimtaka akatolea nje. Sasa naanza kuamini kuwa huo ulikuwa uzushi. Inaelekea jamaa walimscrutinize diligently wakajua alikuwa sio material waliotegemea. Aibu.
 
Back
Top Bottom