Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Chadema hamko serious. Watu wanawaamini, lakini wakiingia ndani na kuona incompetence ya Mheshimiwa Mbowe, anaongoza chama kama ukumbi wa starehe--wanaona mnawapotezea. Huo ndio ukweli wenyewe. Nakaaya dada msomi na sio mamluki, kawaamini halafu mkadisappoint. Zitto mwenyewe has been frustrating with the Chadema leadership. Halafu leo mnataka tuwape nchi. Mnacheza nyie. Hamko serious.
CCM mko makini? Eti kilimo kwanza wakati Tani 15,000 zimewashinda kuzinunua huko Mbeya harafu mnatuambia kilimo kwanza hafu tupeleke wapi hayo mazao na kuya uza nje hamtaki?
 
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.


Mods

Badilisheni title ya hii thread. Nakaaya HAJARUDISHA kadi ya CHADEMA. Kama angekuwa amerudisha angewapelekea CHADEMA, kwani wao ndio waliompa. CCM haikutoa kadi ya CHADEMA na kumpa Nakaaya. Hivyo si sahihi kusema kwamba amerudisha hiyo kadi. Usahihi ni kwamba isomeke "Nakaaya amkabidhi JK kadi ya CHADEMA". Basi! Ieleweke hivyo kwa usahihi wake, ili tuweze kuijadili mada hii kwa mapana na marefu yake!

-> Mwana wa Haki
 
CCM mko makini? Eti kilimo kwanza wakati Tani 15,000 zimewashinda kuzinunua huko Mbeya harafu mnatuambia kilimo kwanza hafu tupeleke wapi hayo mazao na kuya uza nje hamtaki?

So, Rais Dr. Slaa, Makamu wa Rais Said Mzee Said, and Waziri Mkuu DJ Mbowe. Hamko serious nyie. Mtapiga makelele humu ndani, lakini watu wenye busara na upeo wa kuona mbali hawawapi kura wala nchi. When you become serious, tutawapa kura. Mnatuwekea wagombea mamluki, mnachukua vibaraka wa CCM (Shibuda kamchangia Kikwete laki 2 majuzi tu hapa, leo mnamuona mkombozi wenu), mnachagua mgombea mwenza mchovu, mnapoteza muda kuongelea Mama Salma na Kinana badala ya kutuambia mtatoa vipi nchi kwenye umasikini. Vijana wenye busara (Nakaaya) wameingia Chadema wakaona uozo wameondoka.

Jipangeni, mkiwa serious tutawapa nchi.
 
Nilishangazwa sana na kitendo cha Nakaaya kuamua kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama hicho. Nakaaya kwenye Magwanda ya CHADEMA nilikuwa namwona kama nuru ya vijana wenye mioyo ya kimapinduzi na wenye kutakia mema Tanzania yetu. Baada ya kutafakari sana nilimegundua nilikuwa nakosea, Nakaaya ametumia haki yake na maamuzi yake lazima yaheshimiwe. CHADEMA ni taasisi na si mtu ama watu, wengi watajiunga na wengi wataondoka ila chama kitakuwepo na kitaendelea kuimalika kwa wale wote wenye moyo na itikadi za CHADEMA.

Mapinduzi ya kweli yanahitaji askari wenye moyo na wale wenye uwezo wa kujitoa muhanga. Sasa kama unapewa ice cream na unaweza kutoa siri wapi alipojificha jemadari mkuu wako ni hatari sana! Heri ukaachana na mapambano kabla hujasaliti. Nimeonana na Nakaaya mwanzoni wa mwaka huu nikampongeza kwa wimbo wake wa Mr Politician tukaongea mengi, mipango yake ya music na siasa. Anajiamini sana hana haiba za wadada wengi wa Kitanzania, anapenda ishi maisha yake. Siku ile alikuja na ML class Mercedes Benz nyeusi, Mchungaji nikaweka heshima. Sijui kama ni la kwake ama alikuja safisha nyota!

Kama kweli Mil 30 alizoahidiwa mwisho wa Kampeni kama wale wasanii wenzake, walio kwenye kampeni za CCM, ndicho hasa kilichomtoa CHADEMA basi siasa hatoziweza maana akipewa dhamana yuko tayari kuuza hata uhuru wetu.

Kuwa Upinzani kunahitaji uwe na moyo wa Simba, si kila mtu anaweza. Mchungaji nimejitoa muhanga niko tayari hata kujilipua uongozi wa imla na kikoo wa CCM ufikie mwisho. Nimalize kwa kumpongeza sana sana kwa uamuzi wake wa kwenda kwenye kundi la ndege analofanana nalo rangi! Sababu anajua udhaifu wa kiutendaji wa Mwenyekiti wake mpya basi kura yake bado tunaihitaji CHADEMA.

Vote for Slaa

Wenu Mchungaji

Rev Masa

Peace with you all
 
Mi nampongeza kwa kuonyesha makucha yake mapema maana huko mbele angetuletea balaa.
 
Mchungaji kumbe dau sio 60mil tena. Wamemwahidi 30mil tu? Kwa matumizi ya kawaida kwa mwanamuziki kama yeye hiyo ni hela ya matumizi ya kawaida ya kama miezi 15 tu. Kumbe Tz kuna watu wana majina makubwa kumbe 'value' yao ni mil 30 tu?
 
Sina uhakika ameahidiwa nini tena na kiasi alichochanguliziwa ila mwisho wa Kampeni atakunja Tshs 30,000,000/= .Pesa balaa kumbuka sasa hivi hapokei simu na huenda amebadili hata line
 
sielewi kwa nini chadema iwaume sana kwa huyu mtu kuondoka ........................au alikuwa na nguvu kuliko wengi tulivyodhani?
 
sielewi kwa nini chadema iwaume sana kwa huyu mtu kuondoka ........................au alikuwa na nguvu kuliko wengi tulivyodhani?
Tunampa pongezi kwa uaminifu wake kwa CHADEMA kwa kuondoka mapema ili asiharibu sana huko mbeleni...na tunamtakia kila la kheri
 
Sina uhakika ameahidiwa nini tena na kiasi alichochanguliziwa ila mwisho wa Kampeni atakunja Tshs 30,000,000/=

Mchungaji, hata kama mwisho wa yote ni 100mil kwa yeye bado itakuwa ndogo. Kuuza uhuru wa ubunifu kwa 100mil ni bei ndogo sana hasa kwa umri wake kama mwanamuziki. Huyo mwenyekiti wake ana probability ya kuongoza kwa miaka 5 tu! Labda nilikuwa nampa huyu bibie hadhi ya juu sana kuliko uhalisia wake
 
A beg a beg a geg....Nakaaya ni msomi? Kasoma wapi?

Selemani umekurupuka...au kujua kusoma na kuandika kiingereza ni usomi???

Humjui huyo jamaa? huwa ni mkurupukaji na mropokaji na mdini
 
Mchungaji.
Kwa jinsi hao jamaa walivyo wanaweza kumtoa kavukavu baada ya kampeni...
Sa hizi wako desparate..ahadi yoyote wanatoa..
Pole yao daktari Silaha akikaa mjengoni...
 
Lakini ujumbe wa ule wimbo wake wa Mr. Politician si unawahusu CCM. Walisema maisha bora kwa kila mtanzania lakini hayo maisha bora hakuna! Sasa inakuwaje anapingana na mahudhui ya wimbo wake? Opportunist huyo!!!!!!!!!!!
 
Sina uhakika ameahidiwa nini tena na kiasi alichochanguliziwa ila mwisho wa Kampeni atakunja Tshs 30,000,000/= .Pesa balaa kumbuka sasa hivi hapokei simu na huenda amebadili hata line
Kumbe hawa wasanii wameahidiwa 30M kwa kampeni za JK? Kama ulivyosema Mchungaji kuwa kuwa upinzani hapa Bongo lazima uwe na moyo wa simba siwezi kuwalaumu sana hawa vijana wanaomkampenia JK huku wakiamini kabisa wakiimbacho sio kilichoko mioyoni mwao,maana kwanza wapewa umasikini kwanza na wakati wa kampeni wameonyeshwa mnofu kwa mbaali.
Wasiwasi wangu ni kuwa kama malipo ni baada ya kampeni kwisha( maana yake baada ya uchaguzi) na CCM ikapigwa chini hapo ndio watakapo jua kuwa afadhali hata wale wadosi wanaowaibia kazi zao kuliko CCM kwa dhuluma. Maana hawatalipwa tena. CCM kwa kutosa watu kiaina ndio yenyewe. Kawasalimie huko Nakaaya, ila tarehe 6/11/2010 utajiita una bahati kuwa uliwahi kumkabidhi kadi Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa hadhara.
 
sielewi kwa nini chadema iwaume sana kwa huyu mtu kuondoka ........................au alikuwa na nguvu kuliko wengi tulivyodhani?
Ishu si kuwauma watu!...tunatumia uhuru wetu wa kutoa mawazo!

Lakini inashangaza kwa mtu ambaye amejenga trust na heshima overtime ndani ya CHADEMA, anakuja kurubuniwa kipindi cha kampeni!...

Mi nilidhani zile nguo za CCM zinapendwa na watu wa class fulani, kumbe hata watu wa aina ya Nakaaya wanazitolea povu la mdomo, hadi kufikia kuuza utu...

So far CCM wenyewe washamjua kuwa huyu ni mtu wa fedha, so watakaa wakijua jinsi ya kumtreat, na hawawezi kumpa nafasi zenye siri, maana 'in no time' atawavuruga!

Popo si ndege...Popo si Mnyama! ( .... just something in-between!..huh)
 
MODS post za nakaaya zimekuwa tatu sasa unganisheni na nakaaya-arudisha-kadi-ya-chadema
 
Back
Top Bottom