Ukifuatilia kampeni za ccm utapata sababu za Nakaaya kukimbilia huko. CCM haina hoja za kuwavutia wasikilizaji wake kwenye mikutano yao ya kampeni. Asilimia takribani 80 za muda wao wa kampeni hutumia kutumbuiza adhara iliyopo, zinazobakia ndio hutumika kuwasilisha hoja zao kwa wananchi.
Kwa hiyo haishangazi kuona wanaongeza msanii mwingine, kwani wataingia mzunguko wa pili muda si mrefu hivyo wanahitaji vitu vipya vya kisanii.
Fikiria, JK anafikia hatua ya kuomba msanii fulani apande jukwaani kuburudisha badala ya yeye kuendelea kushawishi wasikilizaji wake ili wamchague. Alifanya hivyo kwenye Uwanja wa Sokoine pale Mbeya, alimwita Kazita kwa sauti akitumia kipaza sauti na kusema "Kazija njoo utuibie wimbo wako." Kazija hakutokea, naye akateremka kutoka jukwaani ukawa mwisho wa hotuba!!!
Kampeni za CCM ni fiesta nyingine, haina tofauti na ile inayojumuisha vijana wa muziki wa izazi kipya. Safari hii hata Komba hana nafasi, amefunikwa na kina Malowa, Bushoke, Kazija, kina Juma Nature na wengine!! VK sasa mambo yametulia, hajisumbui sana, kwa hiyo anahitajika wa kuchukua nafasi yake!!!!