Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Elections 2010 Nakaaya arudisha kadi ya CHADEMA

Huyu jamaa wa CCJ inaonekana njaa inamsumbua, nadhani hata hilo koti kaazima kwa John Komba maana limemvaa- siyo saizi yake. Ni kipindi kifupi mno kwa mtu kuhama hama vyama. Aliona akatafutie umaarufu CCJ kisha adandie CCM. Hawatampa kitu zaidi wata mu-enjoy kwani CCM ina wenyewe. Tuna hitaji wazalendo wa kweli siyo watu wanao endekeza njaa zao. Tanzania Kwanza.
 
Ukifuatilia kampeni za ccm utapata sababu za Nakaaya kukimbilia huko. CCM haina hoja za kuwavutia wasikilizaji wake kwenye mikutano yao ya kampeni. Asilimia takribani 80 za muda wao wa kampeni hutumia kutumbuiza adhara iliyopo, zinazobakia ndio hutumika kuwasilisha hoja zao kwa wananchi.

Kwa hiyo haishangazi kuona wanaongeza msanii mwingine, kwani wataingia mzunguko wa pili muda si mrefu hivyo wanahitaji vitu vipya vya kisanii.

Fikiria, JK anafikia hatua ya kuomba msanii fulani apande jukwaani kuburudisha badala ya yeye kuendelea kushawishi wasikilizaji wake ili wamchague. Alifanya hivyo kwenye Uwanja wa Sokoine pale Mbeya, alimwita Kazita kwa sauti akitumia kipaza sauti na kusema "Kazija njoo utuibie wimbo wako." Kazija hakutokea, naye akateremka kutoka jukwaani ukawa mwisho wa hotuba!!!

Kampeni za CCM ni fiesta nyingine, haina tofauti na ile inayojumuisha vijana wa muziki wa izazi kipya. Safari hii hata Komba hana nafasi, amefunikwa na kina Malowa, Bushoke, Kazija, kina Juma Nature na wengine!! VK sasa mambo yametulia, hajisumbui sana, kwa hiyo anahitajika wa kuchukua nafasi yake!!!!
maweee, hii ni kweli? basi hapo hamna kitu tuna boya tu, yaani kama uwanjani tunasema goli halina golikipa ila kuna jezi tu, anyway ndiyo bye bye tena atakumbuka historia tu
 
Binafsi si mshabiki wala mwanachama wa chama chochote kile.Lakini ninavyoona hii thread inaonyesha wazi kuwa huyo mtu ni influential na ndio maana hata hapa mmechukua muda mrefu kumjadili .Kama Paka mweusi ndio angekuwa kaenda CCM wala msingejisumbua hata kuweka thread hapa.Hivyo kwa mtazamo wangu nawaomba Chadema nao watafute njia au propaganda yoyote kujibu mapigo jukwaani kama walivyofanya wao.Maana hapa tatizo si kuwashawishi wakereketwa wa vyama bali ni kuvuta hisia na mawazo ya watanzania ambao si wanachama wa vyama vya siasa na wale ambao hawajajua bado watamchagua nani.
 
Binafsi si mshabiki wala mwanachama wa chama chochote kile.Lakini ninavyoona hii thread inaonyesha wazi kuwa huyo mtu ni influential na ndio maana hata hapa mmechukua muda mrefu kumjadili .Kama Paka mweusi ndio angekuwa kaenda CCM wala msingejisumbua hata kuweka thread hapa.Hivyo kwa mtazamo wangu nawaomba Chadema nao watafute njia au propaganda yoyote kujibu mapigo jukwaani kama walivyofanya wao.Maana hapa tatizo si kuwashawishi wakereketwa wa vyama bali ni kuvuta hisia na mawazo ya watanzania ambao si wanachama wa vyama vya siasa na wale ambao hawajajua bado watamchagua nani.
umekosea. Kinajadiliwa kinachomhusu na wala si yeye
 
Nakaaya.jpgHapo alipokuwa chadema damu
 
amelamba matapishi yake...soma hii kutoka kwenye blog yake
Its been a min since i posted something fresh. i have just been swamped with all kinds of activities. In short, i have been on the hustle.

Over the weekend niliwaita waandishi wa vyombo vya habari mbali mbali. Nia yangu ya kuwaita... ni kuwatangazia watanzania wenzangu kuwa nimejiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema).Uamuzi wangu umefuatia muda mrefu wa kuangalia vyama vyetu tofauti tofauti na i decided that chadema was best for me. Ni chama cha vijana shupavu na jasiri. wana ndoto zinazoendana na za kwango. Most of all, they have real passion. Something i have not seen in other parties.

I have realized i need to start practicing what i preach. One very wise man said 'BE THE CHANGE YOU WANT TO SEE' Haileti maana kabisa sisi kama watanzania waliopevuka kunyamaza au kutofanya chochote kuhusu haya matatizo tunayoyapitia. Je, wewe unaona sawa wanawake wajawazito kujifungulia chini? unaona sawa wagonjwa kushare vitanda? Unaona ni haki kupewa maji au umeme watapojiskia sababu ya wananunua mashine feki?

Kwa kweli nimechoka kufanywa mpumbavu.Wewe je? Haiwezekali Tanzania ikawa na rasilimali nyingi kiasi hichi na bado watu wanasota hivi jamani!Eti katika nchi masikini duniani, na sisi tupo!! Wanaokaa arusha, jaribu kupitia pale mount meru hsp ujionee maajabu. au wa moshi, katiza pale KCMC emergency room uone Tanzania tunakoelekea. Pia pitia wodi za akina mama uone dharau wanawake tunaopewa. Have you forgotten kwamba WE ARE THE BACKBONE OF THIS NATION? Tupo sehemu ya kusikitisha sana. Its time to RISE!

Ni aibu kwetu sisi kufumba masikio, na kusema hatutahusika na siasa. hatuta piga kura wala kuwa na chama. AMKENI!!! Enyi vijana, huu ndio muda wa kufuta wizi wa mali zetu. Sisi sio masikini. Sisi ni matajiri. Na mkicheza tena mwaka huu, mtapewa dozi kali kuliko iliyotokea hii miaka mitano chama tawala iliyotupa. Nyerere once described Tanzania as a country "stinking with corruption."

"Corruption in Tanzania has no bounds. Every country I visit they talk about corruption in Tanzania. Tanzania is stinking with corruption," Nyerere told journalists gathered at the Tanzania Press Club.

Referring to a tax fraud in the country that recently led to aid suspension by donor countries and organizations, Nyerere declared: "This was one quality of corruption."

"Any government that works for the wealthy does not collect tax, it chooses to harass small-time dealers," Nyerere charged. Je hamuoni haya mambo yanayofanywa na chama cha mafisadi yalishatabiriwa na Baba wa Taifa? Hicho chama sio cha mwananchi wa kawaida ndugu zangu, ni cha walionazo na wanaotaka kuzidi kutumaliza. Tunachohitaji, watanzania wenzangu, vijana wenzangu na wanawake wenzangu ni MATUMAINI na HAKI. Tumekuwa tukikatishwa tamaa kwa muda mrefu sana.Naona mwanga- CHADEMA. Napenda kuwahisi na nyie kujiunga na hichi chama chenye mwelekeo. Hebu tupiganie mabadiliko yetu wenyewe ndugu zangu. Tuchukue hatua kwa namna yoyote ile, tupate haki zetu.

Tukiuliza maswali sahihi, na kwa nia thabiti nina imani tutapata majibu tunayostahili na sio kuyeyushwa tunavyoyeyushwa.

Kuwa mabadiliko unayotaka kuyaona.

The harder the battle, the sweeter the victory!

I AM THE DAUGHTER OF NYERERE! And if he was alive today- trust me...angekuwa CHADEMA.
 
Kama sikosei ni mwezi mmoja uliopita alikabidhiwa kadi ya Uanachama wa CHADEMA now kajiunga na CCM; Tatizo ni Pesa nje nje CCM nadhani alipata record label SONNY ilienda wapi? Sasa kama kila mtu atakimbilia CCM kwa mali na kutajirika kwa milango ya nyuma Tanganyika itajengwa na nani? wote inaonekana hatuna moyo wa nchi yetu, tutabaki kuuza nchi yetu na madini yetu.
 
kazi kweli kweli mmefuta tena post yangu MOD please rudisha post zangu mbili
 
Hii kuhama chama inaweza hata kumnyang'anya washabiki wa muziki wake. Labda awe ameamua kufanya siasa kazi na ahadi ya uDC


Maangalizo mengine banaaa!!!! Watakaomuhama sio wapenzi wa muziki, bali ni wapenzi wa CHADEMA ambao waliupenda muziki wake kv alikuwa CHADEMA!!
 
]umekosea[/COLOR]. Kinajadiliwa kinachomhusu na wala si yeye



Umenielewa lakini nilichoandika?Usiseme tu kuwa nimekosea, mambo mnayoyaona madogo kama hayo ndio yanaweza sababisha mkakosa ushindi msione tu kuwa mnajaza watu mikutanoni mkajipa 100% ya ushindi bali rudieni somo la mzee Lyatonga-1995,na watu mnaowaona wadogo kama hao ndio wenye ushawishi mkubwa kwa ngazi ya chini.
 
Mimi nawasiwasi huyu binti kura jinsi atakavyo piga moyoni mwake kura atampa SLAA and that what she gonna cast her vote.

Sometime people get the offer which they cant refuse,refer "the God father movie"
 
Nakaaya aota magamba sugu ndani ya Chama cha Masharobaro.
Maana hasikiki na hata viti maalum alivyokuwa akivitarajia amevikosa.
 
Atii nini chama kisichojali masalahi ya taifa zaidi ya uvunjaji wa sheria.Upinzani si kuuana ni kuwa na chaguo ni vipi tuendeleze nchi yetu.CDM imefanya upinzani ni kuuana kwa sababu uchoyo wa viongozi wao wa ngazi za juu ambao ni wachoyo na wanachotaka ni kuingia Ikulu ili kupooza kiu chao.
 
I beg to differ... Sugu alianza uharakati kabla nakaaya hajaiba hata benki, sugu was not inspired by Nakaaya kama unajua vizuri histroria ya sugu utanielewa, mkoloni na dr joni walianza harakati from their fvery first song na wanajulika wazi, kumbuka kwamba nakaaya bado ni new generation ingawa she is a talent, kusema nakaaya alimisnpire sugu ni sawa na kusema Ali kiba aliminspire Professor Jay

Tulikua na too proud, hard blasters, kwanza unit na wengine mkuu, wote walikua wanaharakati... ni Clouds na Mkuu ndo wamekuja kubadili upepo na ukumbuke hata akina nature, Temba ni njaa ndo inawaweka pale clouds maana album haziuzi ni concerts na jingle ndo zinazolipa

Now pia tusisahau Karama wa bock 41 - KIKOSI CHA MIZINGA naye yuko kafu and ni mwanaharakati mzuri without nakaya inspiration

LETS NOT MIX UP THINKS HERE
Kweli mkuu,nakumbuka 1995 mnazi mmoja alipopanda jukwaani na kumwaga verse ya "mmachinga anasota,huku gabac**ri ankunywa juice!"...loong time.
 
Nakaaya Sumari amerudisha kadi ya Chadema jioni ya leo na kumkabidhi JK kwenye mkutano wake ulio fanyika leo mkoani Arusha, JK amempongeza sana kwa kitendo hicho na kumwambia karibu mama CCM ndicho chama pekee Tanzania.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom