Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Jamani wana jamii F,nauliza better melon ni tunda gani?
Hilo tunda linaitwa bitter melon, sio tikiti maji bali ni tango pori linalotumika kwenye juisi au saladi na chakula. ni chungu na linatumika kutibu magonjwa mengi
 
mbilimbi sio bitter melon, mbilimbi ni chachu na bitter melon ni chungu, zinajulikana kama tango pori
 
Nikimaliza kula dkka 10 lazima niende chooni alf naharisha kwa mda tatizo laweza kuwa nini
Tatizo utakuwa umeishiwa taulo la tumboni ambalo linakazi ya kumengenya na kufyonza chakula. Tafuta probiotics au maziwa mgando unywe itakusaidia
 
@ gorgeousmimi dr asante sana kwa elimu yako nimechelewa kusoma!anyway... Je P.I.D huweza kumfanya mwanamke asipate ujauzito? Ni nini tiba au dawa yake ?nina ndugu yangu ana mwaka anatafuta ujauzito hapati baada ya kufanyiwa ultrasound akaambiwa ana P.I.D,kapewa dawa inaitwa NOR-T na BROFEN atumie siku saba je hizi dawa ni sahihi? Ataweza kupata ujauzito?au atumie dawa gani ? Mana amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo siku chache kabla ya hedhi na wakati wa hedhi.Ntashukuru sana kama ntajibiwa!
 

Pia oral sex nayo inasemekana kusababisha tatizo hilo.
 
Naomba kuuliza silver nitrate pencil inafaa kutibu warts kwa mjazito wa miezi sita alietokewa na warts sehemu za siri kwa nje na ina madhara yyte! Asante
 
naomba kujuzwa tiba ya choo kigumu..yann kama cha mbuzi...maji nakunywa yakutosha +matunda..ila bado tatazo halijapotea..je kuna dawa amabyo naweza nikanywa ikanisaidia
.kupata choo cha kawaida!!
 
wakuu, mimi naombeni msaada wa kujua kipindupindu kinaitwaje kwa lugha ya kiingereza, ninakuwaga katika wakati mgumu sana ninapokuwa ninazungumza kwa lugha hii ya malkia kisha kikifuata kipengele cha kutamka ugonjwa huo huwa ninachenka sana!!!!!!!!!!
 
wakuu, mimi naombeni msaada wa kujua kipindupindu kinaitwaje kwa lugha ya kiingereza, ninakuwaga katika wakati mgumu sana ninapokuwa ninazungumza kwa lugha hii ya malkia kisha kikifuata kipengele cha kutamka ugonjwa huo huwa ninachenka sana!!!!!!!!!!
Cholera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…