Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Jamani wana jamii F,nauliza better melon ni tunda gani?
Hilo tunda linaitwa bitter melon, sio tikiti maji bali ni tango pori linalotumika kwenye juisi au saladi na chakula. ni chungu na linatumika kutibu magonjwa mengi
 
Hilo linaitwa "bitter" melon sio "better". Hilo kwa kiswahili nadhani ndio tunaita mbilimbi. Unazijua mbilimbi? Ndo bitter melon hiyo sasa. Linasaidia sana kupunguza sukari mwilini. Wagonjwa was kisukari wanashauriwa kula sana hiyo bitter melon angalia pichani chini hapa l. View attachment 325355 View attachment 325355 View attachment 325355 View attachment 325355 View attachment 325355 View attachment 325355 View attachment 325356
mbilimbi sio bitter melon, mbilimbi ni chachu na bitter melon ni chungu, zinajulikana kama tango pori
 
Nikimaliza kula dkka 10 lazima niende chooni alf naharisha kwa mda tatizo laweza kuwa nini
Tatizo utakuwa umeishiwa taulo la tumboni ambalo linakazi ya kumengenya na kufyonza chakula. Tafuta probiotics au maziwa mgando unywe itakusaidia
 
@ gorgeousmimi dr asante sana kwa elimu yako nimechelewa kusoma!anyway... Je P.I.D huweza kumfanya mwanamke asipate ujauzito? Ni nini tiba au dawa yake ?nina ndugu yangu ana mwaka anatafuta ujauzito hapati baada ya kufanyiwa ultrasound akaambiwa ana P.I.D,kapewa dawa inaitwa NOR-T na BROFEN atumie siku saba je hizi dawa ni sahihi? Ataweza kupata ujauzito?au atumie dawa gani ? Mana amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo siku chache kabla ya hedhi na wakati wa hedhi.Ntashukuru sana kama ntajibiwa!
 
Siyo kawaida mtu kupata fungus kwenye koo. Ingawa inawezekana kutokea, ila siyo jambo la kawaida. Sasa inapotokana mtu anakuja na fungus kwenye koo au mdomoni, cha kwanza kabla ya kuanza kutibu ni kuhakikisha kwamba ni fungus na pia kuangalia immunity (kinga ya mwili) ya mgonjwa husika. Mara nyingi fungus ya koo husababishwa na upungufu wa kinga ya mwili na inabidi uboreshe kinga ya mwili kwa kutibu kinachosababisha upungufu wa kinga hiyo pamoja na kutibu fungus. Usipofanya hivyo, hata ukitumia dawa ya fungus, inaweza isifanye kazi, au ikawa inajirudia rudia mara kwa mara.

Pia oral sex nayo inasemekana kusababisha tatizo hilo.
 
Naomba kuuliza silver nitrate pencil inafaa kutibu warts kwa mjazito wa miezi sita alietokewa na warts sehemu za siri kwa nje na ina madhara yyte! Asante
 
naomba kujuzwa tiba ya choo kigumu..yann kama cha mbuzi...maji nakunywa yakutosha +matunda..ila bado tatazo halijapotea..je kuna dawa amabyo naweza nikanywa ikanisaidia
.kupata choo cha kawaida!!
 
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana.

A


B


C


D


E



F
wakuu, mimi naombeni msaada wa kujua kipindupindu kinaitwaje kwa lugha ya kiingereza, ninakuwaga katika wakati mgumu sana ninapokuwa ninazungumza kwa lugha hii ya malkia kisha kikifuata kipengele cha kutamka ugonjwa huo huwa ninachenka sana!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom