Siyo kawaida mtu kupata fungus kwenye koo. Ingawa inawezekana kutokea, ila siyo jambo la kawaida. Sasa inapotokana mtu anakuja na fungus kwenye koo au mdomoni, cha kwanza kabla ya kuanza kutibu ni kuhakikisha kwamba ni fungus na pia kuangalia immunity (kinga ya mwili) ya mgonjwa husika. Mara nyingi fungus ya koo husababishwa na upungufu wa kinga ya mwili na inabidi uboreshe kinga ya mwili kwa kutibu kinachosababisha upungufu wa kinga hiyo pamoja na kutibu fungus. Usipofanya hivyo, hata ukitumia dawa ya fungus, inaweza isifanye kazi, au ikawa inajirudia rudia mara kwa mara.