Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

asante saaana dada gorgeousmimi, mimi nina bacterial effect-ions za tonsils na huwa natumia ampiclox lakini huwa inatibika na kurudi kwa mda mfupi nishauri nitumie dawa gani,, na nitaweza kuzitibu side effects za ampiclox na nini?
Ukiwa unatumia antibiotic ni muhimu umalize cure yote. Ni kawaida ukianza matumizi ya dawa unapata nafuu baada ya siku 2-3 lakini ukiacha kutumia infection inarudi upya na ni kwasababu humalizi dawa zote kama inavyotakiwa.

Nakushauri kama unafanya hivo uache mara moja hali hio ikiendelea kwa muda hao bacteria watatengeneza antibiotic resistance. Ambapo wanatengenza njia mpya za kusurvive na kuwia ugumu kuwaua.

Nakushauri utumie Erythomycin 250mg,vidonge viwili asubuhi na viwili jioni kwa muda wa siku 10.Vidonge hivi ni vyema ukivila na chakula ili kupunguza Gastrointestinal side effects.

Unatatizwa na athari gani ya ampiclox?
 
Last edited by a moderator:
Shukraan mpenzi wangu,karibu anytime ukiwa na swali lolote!

Mkuu hongera kwa kutusaidia na pole kwa kazi nzito ya kuokoa maisha yetu!swali lengo ni hili;

CHLORALMPHENICAL EYE DROP ni marufuku kutumia mjazito na imeandikwa pale juu,kuna dada yangu mmoja yuko huko kijijini alinunua hii dawa akatumia siku ya alhamisi ya wiki iliyopita na alikuwa na ujauzito wa wiki32,yesterday amekwenda hospital akaambiwa mtoto amefia tumboni!!(so sad)je hii dawa yaweza kua ni chanzo??
 
Mkuu hongera kwa kutusaidia na pole kwa kazi nzito ya kuokoa maisha yetu!swali lengo ni hili;

CHLORALMPHENICAL EYE DROP ni marufuku kutumia mjazito na imeandikwa pale juu,kuna dada yangu mmoja yuko huko kijijini alinunua hii dawa akatumia siku ya alhamisi ya wiki iliyopita na alikuwa na ujauzito wa wiki32,yesterday amekwenda hospital akaambiwa mtoto amefia tumboni!!(so sad)je hii dawa yaweza kua ni chanzo??
Kimbley ni kweli chloramphenicol ni dawa ambayo haishauriwi kutumika kwa wajawazito haswa waliopo kwenye 3.trimester kwasababu inapita kwenye placenta na kumfikia mtoto.

Na kama inabidi kutumika lazima daktari achukue maamuzi juu ya umuhimu wa tiba ni kwa manufaa zaidi ya muhusika kuliko risk ya uhai wake.Chloramphenicol ni dawa ambayo haijafanyiwa uchunguzi juu ya madhara yake kwa mtoto aliye tumboni mwa mwanaadamu,lakini kwa wanyama wa maabara ilisababisha teratogenic effect(Mtoto kuzaliwa mwenye mapungufu).

Inajulikana pia intravenous chloramphenicol inaweza kusababisha mtoto kuzaliwa mwenye "GREY BABY SYNDROME".

Siwezi kuthibitisha kama mtoto amefia tumboni kwaajili ya matumizi chloramphenicol since sina kithibitisho kuwa inaweza kusababisha hilo,lakini vilevile kwasababu haijafanyikiwa uchunguzi juu ya matumizi yake kwa wajawazito inaweza kuwa possibility vilevile.

Mpe pole sana mfiwa wa mtoto.
 
Last edited by a moderator:
Kimbley ni kweli chloramphenicol ni dawa ambayo haishauriwi kutumika kwa wajawazito haswa waliopo kwenye 3.trimester kwasababu inapita kwenye placenta na kumfikia mtoto.Na kama inabidi kutumika lazima daktari achukue maamuzi juu ya umuhimu wa tiba ni kwa manufaa zaidi ya muhusika kuliko risk ya uhai wake.Chloramphenicol ni dawa ambayo haijafanyiwa uchunguzi juu ya madhara yake kwa mtoto aliye tumboni mwa mwanaadamu,lakini kwa wanyama wa maabara ilisababisha teratogenic effect(Mtoto kuzaliwa mwenye mapungufu).Inajulikana pia intravenous chloramphenicol inaweza kusababisha mtoto kuzaliwa mwenye "GREY BABY SYNDROME".
Siwezi kuthibitisha kama mtoto amefia tumboni kwaajili ya matumizi chloramphenicol since sina kithibitisho kuwa inaweza kusababisha hilo,lakini vilevile kwasababu haijafanyikiwa uchunguzi juu ya matumizi yake kwa wajawazito inaweza kuwa possibility vilevile.Mpe pole sana mfiwa wa mtoto.

Ahsante sana mkuu mungu akubariki
 
Last edited by a moderator:
mimi ni kijana(kiume),mwenye umri wa miaka 25.nina tatizo la kuvimba matiti.nimejaribu kupata tiba hospitalini lakini imeshindikana.kwa mara ya mwisho tiba niliyo patiwa nilichomwa sindano tatu za DICLOFENAC SODIUM na dose ya vidonge vya DICLOFENAC pamoja na VOLINI GEL kwa ajiri ya kupaka lakini sikupina.Tatizo hili linasababishwa na nini na nini tiba yake sahii?naomba msaada wako tafadhari.
Hello Arch.katunzi,
Tiba uliyopatiwa si sahihi na haihusiani na kuongezeka kwa matiti.Hizo ni dawa za kupunguza pain and inflammation na ndio maana hukupata nafuu yoyote.
Kuvimba kwa matiti kwa wanaume kitaalamu tunaita GYNECOMASTIA.Hali hii inasababishwa na mapungufu ya hormone ya kiume testosterone na kuongezeka kwa hormone ya kike estrogen.
Kuna vitu tofauti vinavyoweza kusababisha hali hio kwa kuathiri mfumo wa hormones kama
  1. Hypogonadism
  2. Hyperthyroidism:
  3. Matatizo kwenye mafigo(Renal failure)
  4. Matatizo kwenye Ini(Liver failure)
  5. Tumor kwenye pitutary gland
  6. Umri kuongezeka
  7. Utapia mlo
  8. Matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kupelekea hali hio pia kama first generation antipsychotic au dawa za ukimwi ARV´s,Anabole steroids,androgens,anti-androgens,benzodiazepines(diazepam-dawa ya anxiety),Tricyclic antidepressants(dawa ya depression),Cimetidine(dawa ya vidonda vya tumbo),chemotherapy(dawa ya cancer),Dawa za moyo kama Calicum channel blockers au digoxin, amphetamines, na baadhi ya antibiotics
Ni muhimu ijulikane chanzo cha matiti kuvimba kama ni kati ya matatizo niloyaorodhesha au dawa nilizoziorodhesha ili kupata tiba sahihi.Clomiphene au tamoxifen ni dawa ambazo zinaweza kujaribiwa.
NB😛uberty gynecomastia inapotea baada ya miaka 3.
 
Last edited by a moderator:
Tiba zipo tofauti za anxiety:
Cognitive therapy:ni therapy inayofanywa na psychologist kusaidia kuondokana na stress,fikra hasi na kukusaidia kukupa fikra chanya.
Dawa pia zinaweza kutumika kama
  1. Benzodiazepines(diazepam,oxazepam):Hii ni first choice kwa emergence situations,hazitakiwi kutumika muda mrefu kutokana na kusababisha toleranse na addiction,zinapaswa zitumike Kwa wiki 2-4,matumizi ya muda mrefu zaidi ya huo ni baada ya makubaliano na psychiatrist.
  2. Betablockers ni dawa ya presha na moyo lakini pia zinaweza kutumika temporarily kucontrol symptoms za anxiety kama za kimwili mfano kutetemeka,moyo kuenda mbio,kutoka jasho n.k
  3. Antidepressant ni dawa za depression kama venlafaxin zinazoweza kutumika pia kutibu anxiety/symptoms lakini zinachukua muda wa wiki 2-4 mpaka upate nafuu.
  4. Pregabalin ni antiepileptic,dawa hii pia inaweza kutumika kutibu anxiety na ina effekt sawia kama Benzodiazepines au venlafaxin.

Asante nimeridhika.. Ubarikiwe sana
 
msaada plz..mara nyingi nikimaliza kula baada ya muda flan najisikia kiungulia,hususani nikila chakula chenye mafuta mengi..hali hii inasababishwa na nn? ni hayo mafuta au kuna tatizo jingine?
 
Naomba kuuliza mwanamke aliyefanyiwa operation ya apendix anapaswa kukaa muda gani bila kukutana na mumewe kimwili?
Naomba jibu Doctor..
 
Samahani Sana doctor naomba msaada wako kuhusu hili

Mke wangu baada ya kujifungua aliweka vijiti vya uzazi wq mpango yeye aliwekewa mkononi sasa baada ya hapo akawa anableed utakuta wiki nzima halafu anapumzika siku 2 au tatu anaanza tena hali hii iliendelea kwa muda kidogo lakini kwa sasa hivi anamda mrefu hajaziona siku sake.

Je hii ni hali ya kawaida au kunatatizo? Majibu yako please
 
Samahani Sana doctor naomba msaada wako kuhusu hili
Mke wangu baada ya kujifungua aliweka vijiti vya uzazi wq mpango yeye aliwekewa mkononi sasa baada ya hapo akawa anableed utakuta wiki nzima halafu anapumzika siku 2 au tatu anaanza tena hali hii iliendelea kwa muda kidogo lakini kwa sasa hivi anamda mrefu hajaziona siku sake
Je hii ni hali ya kawaida au kunatatizo? Majibu yako please

Ni hali ya kawaida ukiwa unatumia uzazi wa mpango!
 
naomba kujuzwa madhara ya kutumia dawa za uzaziwa mpango kwa m2 ambaye hajazaa .
pia naomba kujua madhara ya kutumia condom kila mara
 
msaada plz..mara nyingi nikimaliza kula baada ya muda flan najisikia kiungulia,hususani nikila chakula chenye mafuta mengi..hali hii inasababishwa na nn? ni hayo mafuta au kuna tatizo jingine?
Kula chakula chenye mafuta mengi huchochea hali hio kutokea na inasababishwa na muscle iliyopo katika esophagus na tumbo kulegea na kusababisha accumulation ya contents zilizopo kwenye tumbo including HCl-acid kwenye eneo hilo.

Dawa tofauti zinaweza kutumika kama acid neutralizers (sodium bicarbonate), Aluminium/magnesium hydroxides au PPI(Protonpumpinhibitors like pantoprazol) au Histamin[SUB] 2[/SUB]receptor antagonists kama ranitidin au Foam barriers kama Gavison.

Nimeandika kuhusu suala hili post za nyuma pia unaweza kusoma unufaike zaidi.
 
Kula chakula chenye mafuta mengi huchochea hali hio kutokea na inasababishwa na muscle iliyopo katika esophagus na tumbo kulegea na kusababisha
accumulation ya contents zilizopo kwenye tumbo including HCl-acid kwenye eneo hilo.Dawa tofauti zinaweza kutumika kama acid neutralizers(sodium bicarbonate),Aluminium/magnesium hydroxides au PPI(Protonpumpinhibitors like pantoprazol) au Histamin [SUB]2[/SUB] receptor antagonists kama ranitidin.Nimeandika kuhusu suala hili post za nyuma pia unaweza kusoma unufaike zaidi.

Nashukuru sana kwa maelezo yako..ntajiribu kupitia..je swala la muscles kulegea umeliongelea pia?

Kama hapana ningependa kujua nini kinasababisha muscles hizo kulegea?

Na hizo dawa ulizoziorodhesha zinaondoa tatizo ili la kulegea kwa muscles??..msaada wako pls..nilikuwa nachukulia ni swala dogo ila maelezo yako yamenishtua
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako..ntajiribu kupitia..je swala la muscles kulegea umeliongelea pia?? Kama hapana ningependa kujua nini kinasababisha muscles hizo kulegea?? Na hizo dawa ulizoziorodhesha zinaondoa tatizo ili la kulegea kwa muscles??..msaada wako pls..nilikuwa nachukulia ni swala dogo ila maelezo yako yamenishtua
Sababu mojawapo ni kuongezeka kwa pressure kutoka kwenye tumbo mfano kwasababu ya ujauzito au kuongezeka kwa uzito wa mwili.

Sababu nyingine ni hiatal hernia ambapo sehem ya juu ya tumbo imesogea juu ya diaphragm na kuzuia esophageal spintcher muscle (muscle inayotenganisha tumbo na kifua) kufanya kazi yake ipassvyo .

Hali hii inaweza pia kuwa dalili ya vidonda vya tumbo
 
Sababu mojawapo ni kuongezeka kwa pressure kutoka kwenye tumbo mfano kwasababu ya ujauzito au kuongezeka kwa uzito wa mwili.Sababu nyingine ni hiatal hernia ambapo sehem ya juu ya tumbo imesogea juu ya diaphragm na kuzuia esophageal spintcher muscle (muscle inayotenganisha tumbo na kifua) kufanya kazi yake ipassvyo .Hali hii inaweza pia kuwa dalili ya vidonda vya tumbo

Dr unanitisha..is it very serious???..matibabu yake yakoje??
 
Mr. ray lee usitishike,hili si jambo la hatari na linaweza kurekebishika.Epuka kufanya vitu vifuatavyo

  • Kula milo mikubwa,vizito na vyenye mafuta mengi na kulala baada ya mlo,
  • Kama una uzito jaribu kupunguza hilo,
  • Kula snacks kabla ya kulala,
  • Kula vyakula vyenye ukakasi(nyanya,vitunguu saumu,vitunguu maji) au viungo vingi,
  • Kuvuta sigara kama ni mvutaji,
  • Kunywa pombe ,soda,kahawa na chai na
  • Kula baadhi ya dawa zilizo kwenye group ya NSAID`s kama aspirin au ibuprofen.
Tiba nimeshakutajia zipo tofauti na zinafanya kazi tofauti lakini dhumuni ni aidha kuneutralize gastric acid iliyopo tumboni na ANTACIDs(Acid neutralizers) inafanya kazi hio (natrium bicarbonate, aluminium/magnesium hydroxide), Foam barriers kama Gavison zinatengeneza kama povu na kuzuia gastric acid kuvuka eneo la tumbo na kwenda kwenye esophagus au kupunguza utengenezaji wa gastric acid.

Protonpumpinhibitors na Histamin[SUB]2 [/SUB]antagonists zinazuia production ya gastric acid.
 
Back
Top Bottom