Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

asnte sana je ni dawa gani inaweza kumaliza maumiv makali wakti wa mp
Tumia Naproxen 250mg.Kula vidonge viwili unapoanza kupata maumivu ya siku za hedhi,baada ya hapo unaweza kutumia kati ya kidonge kimoja (=250mg) mpaka vidonge 5 (=1250mg) kwa siku.Kila la kheri
 
Mzio-Kuwashwa mara kwa mara mwili mzima dawa yake nini?
Hello mkuu,nakushauri utumie antihistamin kama cetrizin kidonge kimoja kwa siku.

Nimeandika zaidi kuhusu mzio kwenye post za nyuma. Itakuwa ni vizuri pia ukipata nafasi za kusoma hayo.
 
Side effects za tramadol ni zipi, zina we za kuleta madhara yoyote kwenye tumbo la uzazi wakati mgonjwa anazitumia kwa ajili ya maumivu ya mgongo?
 
Side effects za tramadol ni zipi, zina we za kuleta madhara yoyote kwenye tumbo la uzazi wakati mgonjwa anazitumia kwa ajili ya maumivu ya mgongo?
Sijakuelewa vizuri anaetumia ni mjamzito?Tramadol haishauriwi kutumika kwa mjamzito inapita kwenye placenta na kumfikia mtoto dosage kubwa kwa wanyama imeonekana inaweza kusababisha matatizo kwenye kukukua kwa viungo ,kujengeka kwa mifupa na hata kupelekea kifo.Kwa watoto waliozaliwa inaweza kusababisha matatizo kwenye kupumua.
 
@ gorgeousmimi nimepata tatizo la kusikia maumivu baada ya tendo la ndoa pia nikipata joto kidogo tu nawashwa sehemu za siri.

nilikwenda hospital wakasema sina ugonjwa ila nimeze antibiotics.
siku mbili hizi naona tatizo limerudi tena
inaweza kuwa ni nini?

na matibabu yake ni nini?
 
Sio mjamzito
Ok…athari za kawaida na zinazopatwa na wengi in general ni mdomo kuwa mkavu na constipation,nyingenezo ni kizunguzungu,kuchoka kama kusinzia,kichefchef,kutapika,na kuumwa na kichwa
 
@ gorgeousmimi nimepata tatizo la kusikia maumivu baada ya tendo la ndoa pia nikipata joto kidogo tu nawashwa sehemu za siri.nilikwenda hospital wakasema sina ugonjwa ila nimeze antibiotics.siku mbili hizi naona tatizo limerudi tenainaweza kuwa ni nini?na matibabu yake ni nini?
Je kuna mabadiliko yoyote uliyoyapitia kwenye tendo la ndoa unayohisi yanapelekea hali hio?Uke kuwa mkavu kupeleka michubuko?Kutoka kwa discharges?Ni muda gani tangia utumie dawa?Ilikuwa formulation gani na kama ni ya kula ulikula antibiotic cure yote?
 
hakuna ukavu.
majimaji yameongezeka wiki imepita toka nimemeza.
 
hakuna ukavu.majimaji yameongezeka wiki imepita toka nimemeza.
Inaonekana una disturbance ya normal flora ukeni una bacterial vaginosis/trichomonas vaginalis.
Hali hio inasababishwa na
  • Matumizi ya sabuni kali kusafisha ukeni
  • Kubadili wenza mara kwa mara au kuwa na mwenza mpya
  • Matumizi ya njia za uzazi wa mpango zinazopitia ukeni kama hormonal spiral
  • Ufuaji wa nguo za ndani na sabuni kali
  • Uvutaji wa sigara
Baadhi ya watu hawapatwi na dalili(inakuwa asymptomatic).Lakini dalili kubwa ni
  • kutokwa na discharges ukeni aidha kama maji maji mepesi,au
  • ute mzito mweupe/wa kijivu, au
  • discharge yenye harufu kali kama ya vumba la samaki
Dalili nyingenezo ni:

  • Kuwaka moto kwa uke wakati wa kujisaidia haja ndogo
  • Kuwashwa kwenye eneo la uke.
Tiba ya mwanzo ni metrodinazole unatakiwa ule vidonge viwili kwa siku kwa muda wa siku saba.Ipo pia in gel form unatumia mara moja kwa siku kwa muda wa siku 5.Na kama hujapata nafuu hali inajirudia unapaswa kutumia clindamycin kwa formulation ya cream ambayo unapaka ukeni kila siku kwa muda wa siku 7.Nakushauri pia utumie probiotic(lactic acid vaginal capsules) kwa muda wa siku 7.
 
samahani mkuu,naomba msaada nifanye nini nimeng'atwa na nyuki tangia jumamosi usiku,lakini tangia Jana kidole kinavimba tu,mpaka Leo hali ndo hiyohiyo..unaweza kunisaidia huduma yake ya kwanza ni IPI? Nitashukuru.
 
honeyHot,Tumia cetrizin na nakushauri uwahi hosp umepata allergic reaction.
 
Last edited by a moderator:
Dr habari, nina shida kwenye ulimi kwa ndani, huwa nahisi km nimechomwa na sindano, baada ya hapo nahisi maumivu makali sana kisha yanapoa, nikipaangalia naona kidoa chenya weupe kidogo. Ni miaka imepita sasa, nimetumia dawa za kusukutua kakini wapi, naomba msaada dr.
 
gorgeousmimi uendelee kuwa gorgeous kwa jina la aliyetuumba.

Tatizo langu ni kupata maumivu makali ya tumbo na kuharisha sana muda mfupi baada ya kula chakula chenye mafuta sana. Mfano maziwa ya ng'ombe ambayo hayajaungwa na cocoa wala kahawa, au nyama yenye mafuta sana. Mafuta ya mimea hayanisumbui. Tatizo ni nini na nifanyeje?
 
Ni kwasababu tumbo linapata mshtuko baada ya msosi wa mafuta...kama hali hio inatokea ukila msosi wa mafuta mengi huna tatizo mkuu...siku ukila msosi wa aina hio mfano kwenye shughuli tumia loperamid.Kama unasumbuliwa na tumbo baada ya unywaji wa maziwa au diary products then una lactose intolerance!
 
Last edited by a moderator:
Dr habari, nina shida kwenye ulimi kwa ndani, huwa nahisi km nimechomwa na sindano, baada ya hapo nahisi maumivu makali sana kisha yanapoa, nikipaangalia naona kidoa chenya weupe kidogo. Ni miaka imepita sasa, nimetumia dawa za kusukutua kakini wapi, naomba msaada dr.
Vidonda kwenye eneo la mdomo vinasababishwa na herpes simplex infection.Imegawanyika katika makundi mawili Herpes simplex virus 1(HSV-1) na herpes simplex virus 2(HSV-2).Ni virusi ambao asilimia 20-80 wanao na kupata maambukizi kutoka utotoni.Huyu virusi anakuwepo mwilini in latent stage na anakuwa activated ukiwa na stress,magonjwa au immune system ikiwa down.Nakushauri uende hospitali kupata uhakika zaidi.Tiba ni antiviral kama vaciclovir oral tablets au aciclovir topical maalum ya mdomo.
 
Dr Habari Yako Tatizo Langu Mimi Huwa Nikisimama Kwa Muda Mrefu Napata Kizunguzungu Je Kinasababishwa Na Nini Na Tiba Yake Ni Hipi?
 
Back
Top Bottom