Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Sorry doctor nlikuwa mfanya mazoez mzuri waviungo na nlikuwa nikipenda sana mazoez ila miez kadhaa najikuta nimekuwa mvivu sana wa mazoez..napanga asubui ntafanya ila uvivu unaniingia
 
Sorry doctor nlikuwa mfanya mazoez mzuri waviungo na nlikuwa nikipenda sana mazoez ila miez kadhaa najikuta nimekuwa mvivu sana wa mazoez..napanga asubui ntafanya ila uvivu unaniingia
Jaribu kutafuta motisha mfano mtu wa kufanya nae mazoezi mkuu,kama ni kundi la watu pia itakuwa vyema.Kila la kheri.
 
Habari!! Nilikua naomba kujua flared rib inasababishwa na nini? Effect zake pamoja solution. Asante
 
habar dk! mimi ni mjamzito, ujauzto wang una wk12, sasa nina tatizo la kukojoa nasikia maumivu makali kama naungua vile, nimepima mkojo majibu nina UTI, na dawa nimechomwa powercef 1 leo, naomba kufaham dk je ina madhara kwa mtoto alie tumboni?
 
[URL="https://www.jamiiforums.com/" said:
baby
arrow-10x10.png
[/URL] voice;12526912]habar dk! mimi ni mjamzito, ujauzto wang una wk12, sasa nina tatizo la kukojoa nasikia maumivu makali kama naungua vile, nimepima mkojo majibu nina UTI, na dawa nimechomwa powercef 1 leo, naomba kufaham dk je ina madhara kwa mtoto alie tumboni?
hello baby voice,ceftriaxone inapita kwenda kwa mtoto,matumizi yake kwa wajawazito haishauriwi lkn naona daktari hakuwa na choice,hakuna vithibitisho kwamba ina madhara kwa mtoto aliye tumboni.
 
Last edited by a moderator:
Dr gorgeousmimi,

Naomba kujua tatizo la Moyo kutanuka linatokana na nini? Je ni moja kati ya magonjwa ya Moyo yanayotangazwa mara kwa mara? Je ni kawaida kwa tatizo hilo kutokea? Tiba yake ni nini hasa?

Shukrani.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Naomba unishauri je nitumie dawa gani kwa ajili ya kutibu majipu kwa mtoto wa miaka miwili?Nilimpa ampiclox ila naona yanazidi kuongezeka hasa maeneo ya usoni na shingoni.

Tatizo lingine ni kwamba mimi binafsi sina kabisa hamu ya kula.Mara nyingi nakula mara moja tu kwa siku na nisipate njaa.

Naomba unishauri kama kuna tiba ya kusaidia kuleta hamu ya kula
 
dr. nisaidie nikinyoa ndevu vipele vinaota sana. hi kitu ina dawa? nakereka sana mkuu?
 
Naomba unishauri je nitumie dawa gani kwa ajili ya kutibu majipu kwa mtoto wa miaka miwili?Nilimpa ampiclox ila naona yanazidi kuongezeka hasa maeneo ya usoni na shingoni. Tatizo lingine ni kwamba mimi binafsi sina kabisa hamu ya kula.Mara nyingi nakula mara moja tu kwa siku na nisipate njaa.Naomba unishauri kama kuna tiba ya kusaidia kuleta hamu ya kula
Hello, Nakushauri umpeleke mtoto hosp achukuliwe vipimo vya damu na culture ya usaha ili upatikane uhakika ni aina gani ya bacteria alokuwa nao ili kupata tiba sahihi....Usitumie tu antibiotic bila kujua aina ya infection inayomtatiza mtoto unamtengeneza resistence kwenye umri mdogo.

Suala la wewe kutopenda kula limeanza lini?
 
Hello,Nakushauri umpeleke mtoto hosp achukuliwe vipimo vya damu na culture ya usaha ili upatikane uhakika ni aina gani ya bacteria alokuwa nao ili kupata tiba sahihi....Usitumie tu antibiotic bila kujua aina ya infection inayomtatiza mtoto unamtengeneza resistence kwenye umri mdogo.Suala la wewe kutopenda kula limeanza lini?

Asante kwa ushauri.Nitafanya hivyo.Hilo suala la kutokula nina kama miezi mitatu
 
Dr gorgeousmimi,Naomba kujua tatizo la Moyo kutanuka linatokana na nini? Je ni moja kati ya magonjwa ya Moyo yanayotangazwa mara kwa mara? Je ni kawaida kwa tatizo hilo kutokea? Tiba yake ni nini hasa?Shukrani.BACK TANGANYIKA
Hello,
Swali lako ni pana na linahusiana na vitu vingi.Kupanuka kwa moyo kitaalamu tunaita ni kukua kwa caridiac muscle kutokana na moyo kuongezeka kufanya kazi/jitihada ya kusukuma damu.Kuna aina mbili ya kuongezeka kwa moyo nazo ni HYPERTROPHY(kuongezeka kwa thickness ya msuli wa moyo) na DILATION (kuongezeka kwa upana wa chambers za moyo)
Right ventricle inasukuma damu kutoka kwenye mapafu(deoxygentated blood/damu chafu) na left ventricle inasukuma damu kwenda mwilini(oxygenated blood/damu safi).Valve za moyo zimefunguka kwenye picha moyo ukisukuma damu zinajifunga ili kuepuka backflow ya dam.
heart chambers and valve.jpg
  • Sababu mmojawapo ya hypertrophy ni kuongezeka kwa presha kwenye mapafu au mwili.Kazi ya ziada ya kusukuma damu kutokana na kuongezeka presha inasababisha ventricle kupanuka baada ya muda ni kama misuli ya mwili inavyotanuka ukibeba vitu vizito.
  • Kuongezeka kwa presha inasababisha LEFT VENTRICULAR HYPERTROPHY (LVH).
  • Hypertrophic cardiomyopathy ni sababu nyingeneyo huu ni ugonjwa wa kurithi unasababisha muscle fibers za moyo kuwa weak.Kwasababu hizi fibers zinatakiwa zifanye kazi ya ziada ya kusukuma damu zinatanuka baada ya muda.
  • Sababu nyingine ni magonjwa kama emphysema(damage in the lungs air sacs/alveoli) au cystic fibrosis ambayo yana damage mishipa ya damu iliyopo kwenye mapafu na kusababisha kuongezeka kwa presha kwenye baadhi ya mishipa na kusababisha RIGHT VENTRICLE HYPERTROPHY(RVH)
​Vitu vingine vinavyosababisha cardiac dilation ni
  • Unywaji wa pombe uliokithiri
  • Mshtuko wa moyo
  • Inflammation kwenye msuli wa moyo ambayo inatokana na viral infection
  • Chemotherapy
  • Kuongezeka kwa madini ya chuma mwilini kutokana na ugonjwa unaoitwa Hemochromatosis
  • Matumizi ya cocaine
  • Matumizi ya dawa za ukimwi au dawa za kutibu schizophernia zinasababisha QT-elongation
  • Baadhi ya magonjwa kama thyroid
  • Exposure ya madini ya cobalt,lead na mercury haswa kwa watu wanaofanya kazi viwandani.
  • Matatizo kwenye valves za moyo kama valves kushindwa kufunga ipasavayo na kuababisha damu kurudi(backflow) kila wakati ambapo moyo unasukuma damu.
  • Matatizo mengine ya moyo kama heart failure,angina,mapigo ya moyo kubadilika(arythmia) yanaweza kupeleka pia kutanuka kwa moyo.
Tiba inaweza kusaidia kupunguza au kureverse ugonjwa kama ukiwahiwa mapema na kutibu dalili zilizopo.Hakuna dawa ya kusaidia moyo urudi katika hali yake ya awali damage inayopatikana hapo ni permanent.Ni muhimu mtu abadili mfumo wa maisha na kuacha uvutuaji wa sigara,kula vyakula sahihi,kupunguza uzito kama umeongezidi na kuacha unywaji wa pombe.Ni muhimu pia mgonjwa akipatia tiba ijulikane sababu iliyopelekea moyo kutanuka na kurekebisha hilo kwanza kwa mfano kama ni kuongezeka kwa presha inabidi litibiwe hilo kwanza au kama ni heart failure inabidi litibiwe hilo kwanza.Kwa wale wenye matatizo ya valves za moyo upasuaji unaweza kutumika au mabadilko ya heart rythyms pacemaker inaweza kutumika
Dawa ambazo zinaweza kutumika ni
  • Kwenye baadhi ya kesi za hypertophy zinaweza Beta-blockers na dawa kama Calcium channel blocker inaweza kusaidia moyo urelax (kuupunguzia moyo kazi)
  • ACE-inhibitors/Angiotensin receptor blockers:zinasaidia kupunguza presha ambayo moyo unatakiwa upambane nayo kusukuma damu
  • Diuretics:Kusaidia kupumua na kupunguza excess fluids zilizopo mwili kama kwenye miguu hata mapafu,Hasa kwa wale wenye heart failure
  • Digoxin ni dawa nyingeneyo na nyingenezo zinaweza kutumika kutokana na kichochoeo kilichosababisha moyo kutanuka.
 
Habari
Kuna ugonjwa mmoja wa ngozi kama vile Fungasi .,wengi wamezoea kuuita Mba .,mara nyingi wanapata wanafunzi wa shuke za bweni . Unakua kama na Viduara Vyeupe .
Ugonjwa huu sasa unamsumbua kwa muda wa mika sita ,unakuna na kupote anapotumia Cream ,mara nyingine alaishauriwa kutumiwa Mafuta ya Break,Dawa ya Mba ya maji ,lakini tatizo bado lipo pale pale ,Pia alitumia Fluconazal/Vidonge ,lakini bado tatizo lipo palepale.

Na sasa linasambaa mwili mzima mpaka kila mahali .

ushauri tafadhali tiba ya ugonjwa huu .

Na sasa ukiwa unarudi unakua kama vipele vidogovidogo vya baridi kisha ukipaka cream ndio vinakua Vya duara tulivyozoea kuviona hivyo vya mba .

Msaada hapanana ushauri
 
Kwenye maisha..ndio yapo.Situmii dawa
Hali yako ya kupoteza ham ya kula ni ya kisaikolojia zaidi my dia,nakushauri urekebisha matatizo yako yanayokukabili kwenye maisha na hamu ya kula itarudi kama awali.Pole sana na kila la kheri.
 
Habari
Kuna ugonjwa mmoja wa ngozi kama vile Fungasi .,wengi wamezoea kuuita Mba .,mara nyingi wanapata wanafunzi wa shuke za bweni . Unakua kama na Viduara Vyeupe .
Ugonjwa huu sasa unamsumbua kwa muda wa mika sita ,unakuna na kupote anapotumia Cream ,mara nyingine alaishauriwa kutumiwa Mafuta ya Break,Dawa ya Mba ya maji ,lakini tatizo bado lipo pale pale ,Pia alitumia Fluconazal/Vidonge ,lakini bado tatizo lipo palepale.

Na sasa linasambaa mwili mzima mpaka kila mahali .

ushauri tafadhali tiba ya ugonjwa huu .

Na sasa ukiwa unarudi unakua kama vipele vidogovidogo vya baridi kisha ukipaka cream ndio vinakua Vya duara tulivyozoea kuviona hivyo vya mba .

Msaada hapanana ushauri
Anahitaji tiba ya strong topical corticosteroid kama elocon(mometason),flutivate(flutikason) hizo ni GROUP III CORTICOSTEROIDS/GROUP II CORTICOSTEROID with antibiotic since ana infected eczema/infectious seborroiske dermatittis so anaweza kujaribu betnovat with chiniform au synalar with chiniform kwa muda wa wiki moja asipopata nafuu itabidi atumie group 3 au systemic kama prednisolon mfanomandella ni muhimu pia akitumia hio strong steroid astep down yaani mfano atumie group 3 once a day kwa wiki moja,kisha atumie once every second day kwa muda wa wiki nne kisha atumie twice per week kwa muda wa wiki nne ili kuepuka kupata ugonjwa tena na kupata athari nyingine kwenye systemic cortison production.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom