Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Hellow mkuu ngalyas_t ugonjwa wako kitaaluma unaitwa migraine.
Ugonjwa huu chanzo chake maalumu hakijulikani lakini inasemekana unasababishwa na kutanuka /vasoconstriction ya mishipa iliyopo kwenye ubongo.Ni kawaida ukipatwa na migraine kuanza na aura kati ya dakika 5-20 na inakuwa chini ya dakika 60 mfano kwa baadhi ya watu macho kuwa mazito na kuchoka,wengine huhisi kama mikono kama inachomachoma na kufa ganzi,kizunguzungu au hata kushindwa kuongea.Kichefchef na kutapika pia huweza kutokea.Baada ya aura yanakuja maumivu ya kichwa kati ya masaa 4-72.Maumivu haya yapo tofauti kutoka kwa mtu na mtu.Wengine huumwa baadhi ya sehem za kichwa na wengine huumwa na kichwa kizima.Migraine inakuwa triggered na vitu tofauti kimoja wapo ni stress,kutopata usingizi wa kutosha,pombe,hedhi au baadhi ya vyakula.Ni muhimu ukitibu ugonjwa huu ule dawa pale unapoona aura inaanza yaani mfano macho kuwa mazito,hasa dawa ya kundi la triptanes.Ukichelewa kula dawa hazina manufaa.
Chaguo la kwanza la dawa ni painkillers za kawaida kama Paracetamol au NSAID´s ibuprofen/aspirin/naproxen/cataflam.
Chaguo la pili ni TRIPTANES(selective 5HT-receptoragonists).Hizi zipo za aina tofauti inayotumika sana ni sumatriptan/imigran nyingenezo ni zolmitriptan,eletriptan,rizatriptan,almotriptan.Betablocker kama pranolol pia inaweza kutumika kama prophylaxis method ya kutibu migraine.
Tukirudi kwenye swali lako sasa,hedex(paracetamol) haina madhara ukitumia muda mrefu as long as huimisuse.Kula mara kwa mara unapooumwa na kichwa hakuna shida.Kila la kheri.
Cc Mkoroshokigoli
Pole ngalyas_t tunasumbuliwa na tatzo Moja
 
Last edited by a moderator:
Busha linasababisha upungufu wa nguvu za kiume? Na je ukifanyiwa upasuaj haipunguz uwezo wa kufanya tendo la ndoa na kutia ujauzito?
 
Nikila samaki aina ya sangara navimba uso wakat mwingine nahic km kuna vinachoma choma mwilini,tatizo hasa ni nini?
 
Nikila samaki aina ya sangara navimba uso wakat mwingine nahic km kuna vinachoma choma mwilini,tatizo hasa ni nini?
Tatizo ni mzio nimeshaliandika hili post za nyuma.Usile sangara!
 
Nini kinasababisha tatizo la kukoroma?
Nilishalijibu hili post za nyuma nimekukopia

Tukilala musclature ya upper respiratory system ina relax,kwahio njia ya hewa inakuwa nyembamba na tukipumua eneo hilo lina vibrate,pressure inaongezeka na kupeleka msuguano kati ya soft tissues na kusababisha kukoroma.Pombe na dawa za usingizi zinasababisha njia ya hewa kuwa nyembamba,na hali inazidi kuwa mbaya ukiwa umelala usingizi mzito.Uvutaji wa sigara pia unaweza kuwa chanzo na uzito mkubwa.Ili kuepuka kukoroma

  1. kama uzito umezidi jaribu kupungua,
  2. epuka kunywa pombe,
  3. kuvuta sigara na sleeping pills (hypnoticum na sedatives),
  4. Ukilala lala ubavu epuka kulala na mgongo

Tiba zinazoweza kutumika ni nostril spray au plaster unayoweka juu kwenye pua ili kufungua njia ya hewa.​

Busha linasababisha upungufu wa nguvu za kiume? Na je ukifanyiwa upasuaj haipunguz uwezo wa kufanya tendo la ndoa na kutia ujauzito?
Hello sock masta,
Inategemea na ukubwa wa busha,Likiwa kubwa sana linaweza kuathiri uwezo wa kujamiiana kwasababu ya muongezeko wa ngozi na ukubwa wa eneo.Busha haliathiri testis,uzalishaji wa mbegu upo kama kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Simeticone 240mg,Kula kidonge kimoja baada ya chakula kikuu,Unaweza kula mpaka vidonge vitatu kwa siku.
au Dimeticone 200mg,tumia kidonge moja mara 3-4 kwa siku.

Kwani gesi ikiwa tumboni ina athari zozote?
 
Nilishalijibu hili post za nyuma nimekukopia

Tukilala musclature ya upper respiratory system ina relax,kwahio njia ya hewa inakuwa nyembamba na tukipumua eneo hilo lina vibrate,pressure inaongezeka na kupeleka msuguano kati ya soft tissues na kusababisha kukoroma.Pombe na dawa za usingizi zinasababisha njia ya hewa kuwa nyembamba,na hali inazidi kuwa mbaya ukiwa umelala usingizi mzito.Uvutaji wa sigara pia unaweza kuwa chanzo na uzito mkubwa.Ili kuepuka kukoroma

  1. kama uzito umezidi jaribu kupungua,
  2. epuka kunywa pombe,
  3. kuvuta sigara na sleeping pills (hypnoticum na sedatives),
  4. Ukilala lala ubavu epuka kulala na mgongo

Tiba zinazoweza kutumika ni nostril spray au plaster unayoweka juu kwenye pua ili kufungua njia ya hewa.​

Shukrani mzazi.
Nadhani uzito wangu umekuwa mkubwa sana.
Nisaidie kutoka hapo
 
Habar yako docter pamoja na wana jf......nina mdogo wangu umri wa miaka 19 ....amefanya baka usoni ..kwa muda mrefu na kila cku linakua... ametumia dawa nyingi ila bado ...but wakati alipo enda hospital alipofanyiwa uchunguzi akagundika ni tatizo la ukoma ...kwa muda mrefu sasa zaid ya miezi 6 anatumia zile dawa ila lile baka bado linazidi kungara hivi hakuna dawa yeyote ya kusuluhisha hilo tatizo sababu nahic linaengezeka naomba ushauri wako doctor ....
 
Msaaada;tumbo kuuma karibu na nyonga kushoto ni tatzo gan??na dawa yake please
 
Mama mwenye threatened abortion anakuwa treated na progesterone au bed rest tuu inamtosha?
 
Dr mie ninasumbuliwa na mba sijui au fangas pembeni ya mapaja na pumbu kuna kipindi huchubuka na kuweka alama hunitesa sana ila inakaa kama wiki 2 inakata nakuwa fresh ila kunakuwa na alama fulan sasa dawa gani nzuri dr ya kumaliza hili tatizo muda mwingine hadi pumbu hubabuka ngozi
 
Msaaada;tumbo kuuma karibu na nyonga kushoto ni tatzo gan??na dawa yake please

Fafanua hayo maumivu intensity yake ipoje?linauma wakati gani?hali hio imeanza lini na ina muda gani?umeshawahi kutibiwa suala hilo before?tiba gani?
 
Dr mie ninasumbuliwa na mba sijui au fangas pembeni ya mapaja na pumbu kuna kipindi huchubuka na kuweka alama hunitesa sana ila inakaa kama wiki 2 inakata nakuwa fresh ila kunakuwa na alama fulan sasa dawa gani nzuri dr ya kumaliza hili tatizo muda mwingine hadi pumbu hubabuka ngozi
Clotrimazol 1% cream paka mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki 2-3.Kama hali hii unayo muda mrefu ni vyema ukaonane na daktari inawezekana tatizo lako liko advanced zaidi ya fungus.
 
Back
Top Bottom