bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,334
- 2,463
Habari ya asubuhi wanajamii.
Kuna mambo mengi sana ya kuiga hapa duniani lakini kuna mengine siyo ya kuiga kabisa kama jambo ambalo amefanya Mr Blue kuvaa mavazi ya kinazi kwenye video ya music inayokwenda kwa jina MAWE akiwa kashirikishwa yeye pamoja na RayVanny na msanii wa kitaa ambaye [kitaa kinamwamini kama kiongozi wa Dini] Nyandu Tozi.
Na yeye sio wa kwanza kwa vijana wa kitanzania kuonyesha kufurahishwa sana na Adolf Hilter bila kujua zaidi juu ya mtu huyu.
Kwanza kabla ya yote yapaswa kujua ya kwamba NAZI walikuwa watu walioamini katika falsafa ya kutokuwepo usawa baina ya binadamu. Waliamini binadamu hatujaumbwa sawa na muumba, waliona baadhi ya binadamu ni bora kuliko wengine hivyo binadamu walio bora ndio wapate malazi malezi bora pasipo kujali binadamu wa mataifa mengine.
Katika mpangilio wao wa ubora wa binadamu waliona wazungu wenye nywele blonde, warefu wenye asili ya Aryan ndio bora wakifuatiwa na wazungu wengine huku watu wa mwisho kwa ubora wakiwa ni Waafrika, Wahindi na Waisrael inasikitisha kuona msanii mkubwa kuvaa mavazi ya watu hawa.
Mbali na sera hizo za kibaguzi za NAZI jambo lingine kubwa la kuzingatia ni kiongozi wao mkatili Adolf Hilter. Ipo wazi endapo nchi ikiongozwa na kiongozi katili basi na nchi inakuwa katili kwa raia waishio ndani yake.
Huyu dubwana Adolf Hilter alikosa kabisa heshima kwa binadamu wengine wenye asili tofauti na Germany aliona binadamu wengine ni kama sisimizi ambapo angeweza kuwa flush mara moja kwenye uso wadunia.
Mtu kama huyu sio wa kuigwa wala kushabikiwa kabisa kwani kila mmoja anajua ambavyo anajisikia vibaya akidharauliwa sasa huyu anakunyima na haki ya kuishi kabisa ni uovu kiasi gani.
Hata hivyo yeye mwenyewe hakuwa pure Aryan lakini bado akasababisha uharibifu mkubwa (kama sio ukichaa ni nini sasa)
WATU WA KUBEBA LAWAMA
Designer wa mavazi katika shooting hiyo yawezekana mr blue siye aliyechagua hayo mavazi bali alivalishwa na mshauri wa mavazi. Na kutokana na ujinga wao kuhusu historia wakajikuta wanatenda jambo ambolo limeniudhi sana.
Yapaswa kutokushadadia jambo bila kufanya uchunguzi wa kutosha kuepuka fedhea kama hizi. Ona sasa Mr Blue anaonekana vibaya.
Mwenye wimbo (NYANDU TOZI). Hii ni ngoma kali ambapo ulikuwa unamrudisha tena Nyandu kwenye charti ilibidi amake sure kila jambo linaenda sawa. Sasa ona na yeye anaonekana vibaya kwa kuruhusu mavazi ya Mr Blue kupoteza dira kabisa ya ngoma yake.
Na sidhani kama stesheni kubwa zinazojielewa zinawezaa kuweka uchafu wa fikra katika mavazi Mr Blue. Hii ngoma itaishia hapa tuu nchini na sidhani kama hilo ndio lilikuwa wazo la bwana Nyandu MAKO kweli kweli.
BASATA hawa naona wamekalia kuzuia maungo ya kike tu yasionekane mambo ya msingi kama kuchafuliwa kwa picha mgando na mavazi kuashiria UNAZI wapo kimya hata hawaelewi majukumu yao yapaswa wapigwe MAWE. Hizi ndio ilikuwa pointi ya kuchukua kuonyesha ukomavu wao katika kulea wasanii wetu.
Ona sasa na wao wanakuwa na makosa, BASATA yapaswa kustopisha mara moja video ya wimbo huu.
WANA WA ISRAELI
Maskini namwonea huruma Mr Blue wana wa vita wakiamua kumshukia, kutokana na ujinga wake. Watu wengi sana walikuwa wahanga wa sera za kinazi amboko Israel walipoteza ndugu zao yapata million sita huku kwa ujumla vita vilivyosababishwa na huyo dubwana Hilter vikileta jumla ya vifo million arobaini.
Usione hizi number za vifo ni rahisi kuzichapa na kuzitamka machungu yake hayaelezeki ni machozi kiasi gani wamelia watoto ambao walipoteza wazazi wao kaka zao dada zao katika vita vile ? Ni huzuni kiasi gani waliyopata wahanga wa sera hizo kipindi hicho.
Tuache ujinga wa kushabikia mambo pasipo kujua undani wake.