NAKICHUKIA SANA KIFO😭

NAKICHUKIA SANA KIFO😭

šŸ˜„Hii last verse imenifikirisha sana mkuu

Hapa napata swali huenda tukifa ndio basi tena hakuna hiyo eternal life tunayoahidiwa

Wenzangu wameahidiwa mabikra 12

Sisi tumeambiwa tutaketi na Mungu kwenye kiti cha enzi.

Kwa misingi hii nilijiuliza sana kuhusu kifo nikajikuta nakuwa mzito sana kwenda kanisani.

Maana stori za motoni kwa sisi watenda maovu zinaogofya sana.

Leo mchungaji kasema sisi ambao hatufanyi mema tutatupwa ziwa liwakalo moto
Ukifa maisha yako ndiyo mwisho, hakuna ushahidi kwamba utaendelea.

Maisha yataendelea kwa matter yako kuwa funza, mimea, eventually atoms zako zitarudi kwenye viumbe wengine.
 
Mimi ni mtu ninayekichukia sana kifo ingelikuwa ninao uwezo wa kuzuia watu kufa basi ningefanya hivo

Leo nimejikuta namkumbuka sana Dkt.Ferdinand Masau, Mtu bingwa sana kama nchi tuliwahi bahatika kuwa nae akibobea kwenye masuala ya magonjwa ya moyo na taasisi yake ya Tanzania Heart Insitute hadi pale ilipokumbwa na gharika ikafungwa mwaka 2012.

Alikuwa na maono makubwa sana sema ndio hivo wakati mwingine unaweza kuwa na maono makubwa sehemu isiyo sahihi nadhani msongo wa mawazo ulipelekea nae akafarika mwaka 2013.

Vijana wa juzi ndio wanaweza wasijue sana habari zake huyu Dkt.Masau alikuwa bingwa kweli kweli kabla hata ya akina Janabi wanaovuma leo kwenye masuala ya moyo.

Wakati nikikumbuka ule uzi wa tanzia ya kifo cha dkt.ferdinand nikagundua hayati Ndugulile nae aliumizwa sana na kifo kile sema kifo kilivo nae leo hatupo nae kaenda kuungana na dkt. Masau.

Wana mageuzi wengi hawaishi sana sijui kwanini huwa naumia sana.

Hapa chini naambatanisha salamu za pole alizozitoa Dkt.Ndugulile wakati ule 2013 kufuatia kifo cha Dkt Ferdinand Masau.

Nimelia sana leo, Dkt.Masau hakuwahi kuwa ndugu yangu ila nimemkumbuka na kama kuna yeyote alihusika kwenye njama za kumvuruga kisaikolojia Dkt.Masau laana iwatafune hadi kizazi cha nne.

WATU WAZURI HAWADUMU
Umenijunbusha mbalii sana na huyu mwamba
 
Ni kweli sikupingi ila haiondoi uhalisia wa kuwa nakichukia kifo
Mimi nakushauri usikichukie! Na badala yake ungekipenda tu. Maana hakikwepeki. Yaani siku ikifika, lazima utakufa tu!

Hapa cha msingi muombe tu Mola wako ili hiyo siku ikifika, basi ufe kifo chema! Naamani kile kifo cha uzeeni, huku ukiwa umezungukwa na wanafamilia wako. Na siyo ufe kifo cha kuchomwa moto, kutekwa na kuteswa, nk.
 
HILI NALO MKALITAZAME.

Namuagiza Dokta Janabi aende akalifanyie kazi hili jambo ili watanzania tuishi milele.

Dokta janabi nina imani na uzoefu wako wa kubomoa mioyo ya wagonjwa, umefanya kazi katika mashirika mengi pamoja na serikalini hivyo sina shaka na uwezo wako wa kutufanya tuishi hadi kiama.

Nakutuma ukafanye kazi kwa kujiamini.

Cc: Lucas Mwashambwa chiembe ChoiceVariable Extrovert Nyani Ngabu Lamomy Poor Brain Lloyd Munroe
 
Asee na kinatisha kweli kweli.
Tunaogopa sababu hatujui nini kinafata.
Kuna mtu alisema ukitazama safari ya mto, ni ndeefu yenye kasi ila huwa ukifika baharini unapunguza kasi mno, ni kama unaingia woga, kuitazama bahari kunatisha, ila mwishowe unaingia na kuwa sehemu ya bahari.
 
upo sahihi sana mkuu
 
HILI NALO MKALITAZAME.

Namuagiza Dokta Janabi aende akalifanyie kazi hili jambo ili watanzania tuishi milele.

Dokta janabi nina imani na uzoefu wako wa kubomoa mioyo ya wagonjwa, umefanya kazi katika mashirika mengi pamoja na serikalini hivyo sina shaka na uwezo wako wa kutufanya tuishi hadi kiama.

Nakutuma ukafanye kazi kwa kujiamini.

Cc: Lucas Mwashambwa chiembe ChoiceVariable Extrovert Nyani Ngabu Lamomy Poor Brain Lloyd Munroe
daaah we jamaa🤣🤣
 
Mimi nakushauri usikichukie! Na badala yake ungekipenda tu. Maana hakikwepeki. Yaani siku ikifika, lazima utakufa tu!

Hapa cha msingi muombe tu Mola wako ili hiyo siku ikifika, basi ufe kifo chema! Naamani kile kifo cha uzeeni, huku ukiwa umezungukwa na wanafamilia wako. Na siyo ufe kifo cha kuchomwa moto, kutekwa na kuteswa, nk.
Mbona watu wema wengine wanakuf vifo visivyo vema kumbuka kifo cha Ali kibao
 
Back
Top Bottom