Nakubaliana na hoja ya Spika: Serikali iajiri walimu wengi wa kiume kuliko wanawake

Nakubaliana na hoja ya Spika: Serikali iajiri walimu wengi wa kiume kuliko wanawake

Mpaka sasa serikali inaendelea kuboresha na kama unavyojua 'maboresho' sio suala la siku moja. Sasa basi unafikiri nini kifanyike katika kipindi hiki cha mpito walau shule za vijijini nazo zipate walimu wa kutosha kama ilivyo kwa shule za mjini??? .Tupe suluhisho lako..
Boresha mazingira ya kazi . Unajua mshahara wa madaktari na mwalimu ni tofauti? Kwann isiwe level moja. Nimrfanya kazi serikalini najua mengi. Acha kuleta siasa hayo maboresho unayosema nn???
 
Juzi spika aligusia kidogo suala la ajira kwa walimu na kuishauri serikali kutoa kipaumbele cha ajira kwa walimu wengi wa kiume kuliko wanawake.

Hoja ya spika ina mashiko kwa sababu nature 'asili' ya wanawake wengi hupenda raha na sio wavumilivu wa mazingira magumu.

Kwakuwa uhitaji wa walimu kwa sasa ni maeneo ya vijijini, serikali inapowaajiri walimu wa kike katika maeneo hayo baada ya muda huyakimbia kwa kuomba uhamisho wa kufuata wenza wao ambao wanafanya kazi mijini.

Kwakuwa rate ya walimu wa kike wanaohama ni kubwa ndio maana shule za vijijini zinakosa walimu wa jinsia hiyo kwa sababu asilimia kubwa wamerundikana shule za mjini ambako walihamia kwa kisingizio cha kufuata wenza wao.

Si hivyo Tu, hali hii pia huleta usumbufu kwa walimu wa kiume wanaofanya kazi vijijini kwani hukataliwa na walimu wa kike kwa kuamini kuwa endapo watawakubalia na kuishi kama wana ndoa wataendelea kuishi kijijini. Hivyo walimu wengi wa kike hulazimika kutafuta wenza walioko mjini ilikusudi wahame hali inayopelekea walimu wa kiume walioko vijijini kukosa fursa ya kuoa walimu wenzao.

Kumbe ni sahihi kabisa serikali ikatoa kipaumbele kwa walimu wa kiume kwa sababu ni wavumilivu wa mazingira ya vijijini kuliko wanawake ambao wakiajiriwa baada ya muda wanahama na hivyo kusababisha tatizo la uhaba wa walimu kwa shule za vijijini kubaki pale pale
Chamuhimu Happ naona sheria iwekwe kwa walimu wataokimbia vituo vya kazi, kuliko kupunguza namba kwa walimu wa kike
 
Back
Top Bottom