Nakubaliana na ndugu Bashe kuruhusu wakulima kuuza mazao popote wanapotaka

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nimeona humu watu wengi sana wakiishambulia serikali Kwa kutozuia mazao kuuzwa nje ili kupunguza mfumuko wa bei. Ukweli ni kwamba serikali inaweza kuzuia mazao kuuzwa nje.

Jambo hilo ni hatari sana Kwa mustakabali wa kilimo na wakulima wa Tanzania. Gharama za uzalishaji zimepanda sana, kila nyanja ya maisha vitu vimepanda je hayo mazao ya kilimo yakiuzwa bei chini nani atafidia gharama za ziada?

Mwaka ambao nililaani kilimo ni ule mwaka Serikali ilizuia mazao kuuzwa nje eti kwa sababu ya kulinda bei tuliuza gunia shs 30 elfu hata hivyo hapakuwa nawanunuzi. Kuna kipindi serikali ikatutangazia kuwa itanunua mahindi yetu sijui tani ngapi lkn haikusaidia chochote wakulima tukiendelea kusota na mazao.

Likiwa hilo halijapoa serikali ikakosana na wanunuaji wa mbaazi badala yake nikamsika manyanya anasema mbaazi ni tamu sana wakulima kuleni.

Ndugu zangu soko la uhakika na lenye bei nzuri la mazao yote ya kilimo ni muhimu sana kwa uhai na ukuaji wa kilimo kuliko kushinikiza mazao yashuke bei.

Nakumbuka mama alipo apishwa alizinguka sana kwa majirani kuomba waruhusu mazao ya Tanzania yauzwe kwao. Kuna wakati Kenya walisema mahindi yetu yana sumu ilileta maafa Kwa wakulima
 
Tafuta video za nyuma. Anachoongea Bashe leo ndicho alichokuwa anakisema Magufuli.
 
Nimeona humu watu wengi sana wakiishambulia serikali Kwa kutozuia mazao kuuzwa nje ili kupunguza mfumuko wa bei. Ukweli ni kwamba serikali inaweza kuzuia mazao kuuzwa nje.
Jambo hilo ni hatari sana Kwa mustakabali wa kilimo na wakulima wa Tanzania. Gharama za uzalishaji zimepanda sana, kila nyanja ya maisha vitu vimepanda je hayo mazao ya kilimo yakiuzwa bei chini nani atafidia gharama za ziada?
Naunga mkono hoja Bashe ni mzalendo sana, Wapinzani msione aibu kushirikiana na CCM kwenye hoja zenye maslahi ya Taifa! Bashe ni mzalendo, aungwe mkono na wote!
P
 
Wakati mwingine unaweza kufikiri kwamba Historia ya Tanzania ilianza na Magufuli na kuishia na kifo kwamba hakuna Historia ya Tanzania bila Magufuli kama ukiwasikiliza baadhi ya watu wanaongozwa na emotions badala ya logic, maraisi wote wote wa Tanzania waliopita walizuia uuzwaji wa mazao nje ilipobidi lkn imegeuka ni Magufuli ndiye aliyeanzisha na kuuwa kilimo kana kwamba kabla ya Magufuli kulikuwa na kilimo chochote cha maana ambacho kimeuliwa.

Wakati mwingine intelligence ya watu humu iko chini ya kiwango, kuzuia kuuza mazao nje ni mfumo wa CCM na siyo kwamba ulianzishwa na Magufuli, besides unatumika Dunia nzima hata capitalists kama USA, Europe au hata China hufanya pale inapobidi, huwezi kuexport chakula nje wakati wananchi wanakufa njaa!
 
Na kwa akili zenu mnadhani wakulima wanafaidika?

Wanaofaidika ni madalali. Mteja (tajiri) anatoka Dar au nje ya nchi anaenda kijijini kutafuta mazao, madalali wanamdaka wanamwambia we tulia usihangaike sisi tutakutaftia kwa bei nzuri, wao ndo wanawajua wakulima, wanaenda wanawalangua kwa bei wanayo taka wao madalali, wakipeleka bidhaa kwa mteja wanapandisha cha kwao.

Sasa hiyo nimeongelea wale wakulima wa chini kabisa. Hamna faida ya tofauti wanayopata ila middle men ndo wanafaidika. Mkulima ukigoma kutoa mazao kwa bei wanayotaka wanaenda kusambaza mtaani kwamba bidhaa yako haina ubora. So ili visidode mkulima anaamua tu akubali.

Na kumbuka sio wakulima wote wenye uwezo wa kusafirisha mazao yao wenyewe kwenda nje. Wanawategemea madalali. Things are absurd kwa ground
 
Serikali ikishikilia msimamo huo, na Mimi mwaka huu nalima.

Yaani Kuna majitu yanacheza karata asubuhi mpaka jioni, mkulima anamenyeka shambani, halafu baadae yanataka yake chakula Cha Bure.

Serikali ikikazia hapo, hata wimbi la vijana kuwa bodaboda na kukimbilia mijini litakwisha, utajiri utarudi vijijini.

La msingi ni kuondoa madalali tu
 
Wakati mwingine unaweza kufikiri kwamba Historia ya Tanzania ilianza na Magufuli na kuishia na kifo kwamba hakuna Historia ya Tanzania bila Magufuli kama ukiwasikiliza...
Kuzuia soko la mkulima ukiwa hujasema utafidia vipi gharama za uzalishaji huku ukifurahishwa tu na bei ndogo ya mazao ndilo kosa kubwa sana lisilossmeheka Kwa wakulima wetu.

Na hii ndio imepelekea kilimo kukimbiwa na watu.

Haiwezekani gharama ya kuzalisha gunia moja iwe shs 90 alafu kwa kuwa serikali ina nguvu initengenezee mazingira niuze elf 50 - 60 hiyo hasara ya elf 30 - 40 atafidia nani?

Hayo mataifa mnataja yanazuia wakulima kuuza nje mazao yana mifuko maalum ya kufidia wakulima wao pindi wakiingia hasara, yapo mataifa mengine yameweka hadi bima ya kilimo.

As for now nasimama na Bashe mkulima auze popote
 
Maraisi wote wa Tanzania walizuia mazao kuuzwa nje ilipobidi why picked on Magufuli?
 
Sijakuelewa unakusudia kusemaje
Anachofanya bashe na ndio msimamo wa makamu mwenyekiti wa ccm bara kinana ni kuruhusu kuuzwa mazao kiholela ambapo wafanyabiashara kutoka nchi jiradi wanakuja kununua mazao. Nchi inategemea kulishwa chakula na wakulima wake kabla kutegemea nje.

Wakulima wauze chakula kwa yeyote ila inapokua chakula kinapelekwa nje lazima uwepo utaratibu kuhakikisha haitasababisha upungufu wa chakula nchini.

Ni sawa na tatizo lipo kwa viwanda nchini. Tunauza sukari nje na huku tunaagiza toka nje. Hapo ndio utaona ni mpango wa uwekezaji usiolenga mahitaji ya wananchi ila faida na matakwa ya muwekezaji kupata fedha ya kigeni. Hapo pia ndio anaepa kodi kirahisi.
 
Anachofanya bashe na ndio msimsmo wa makamu mwenyekiti wa ccm bara kinana ni kuruhusu kuuzwa mazao kiholela ambapo wafanyabiashara kutoka nchi jiradi wanakuja kununua mazao. Nchi inategemea kulishwa chakula na wakulima wake kabla kutegemea nje.
Wakulima wauze chakula kwa yeyote ila inapokua chakula kinapelekwa nje lazima uwepo utaratibu kuhakikisha haitasababisha upungufu wa chakula nchini.
Ni sawa na tatizo lipo kwa viwanda nchini. Tunauza sukari nje na huku tunaagiza toka nje. Hapo ndio utaona ni mpango wa uwekezaji usiolenga mahitaji ya wananchi ila faida matakws ya muwekezaji kupsta fedha ya kigeni. Hapo pia ndio anaepa kodi kirahisi.
Jukumu la kuhakikisha nchi ina chakula isiwe Kwa kuwaumiza wakulima serikali ifikiri namna gani itafidia gharama za uzalishaji badala ya kukimbilia kufunga soko kwa sababu wakulima wakikosa soko kilimo kinakufa tunaweza kifikia hata hicho cha gharama kubwa tusikipate kabisa. Bei nzuri ya mazao inavutia uwekezaji na wawekezaji kwenye kilimo.

Hakuna mtu anayefikiri vizuri eti achukue mkopo wake benk au achhukue akiba yake ya pesa aingize kwenye kilimo ambacho ana uhakika serikali itapanga bei bila kuzingatia gharama halisi ya uzalishaji.
 
Maraisi wote wa Tanzania walizuia mazao kuuzwa nje ilipobidi why picked on Magufuli?
Mkuu tunachojadili hapa ni zuio la kuuza mazao nje magufuli ni mojawapo ya waliowahi kuzuia shida Iko wapi nikimtaja
 
Na kwa akili zenu mnadhani wakulima wanafaidika?

Wanaofaidika ni madalali. Mteja (tajiri) anatoka dar au nje ya nchi anaenda kijijini kutafuta mazao, madalali wanamdaka wanamwambia we tulia usihangaike sisi tutakutaftia kwa bei nzuri, wao ndo wanawajua wakulima, wanaenda wanawalangua kwa bei wanayo taka wao madalali, wakipeleka bidhaa kwa mteja wanapandisha cha kwao.

Sasa hiyo nimeongelea wale wakulima wa chini kabisa. Hamna faida ya tofauti wanayopata ila middle men ndo wanafaidika. Mkulima ukigoma kutoa mazao kwa bei wanayotaka wanaenda kusambaza mtaani kwamba bidhaa yako haina ubora. So ili visidode mkulima anaamua tu akubali.

Na kumbuka sio wakulima wote wenye uwezo wa kusafirisha mazao yao wenyewe kwenda nje. Wanawategemea madalali. Things are absurd kwa ground
Mtu akinionyesha mkulima mwenye tani 500 za mahindi store,nitampa milioni 5 bure.
Nasisitiza mkulima aliyelima na kuhifadhi tani 500 store.
 
Na kwa akili zenu mnadhani wakulima wanafaidika?

Wanaofaidika ni madalali. Mteja (tajiri) anatoka dar au nje ya nchi anaenda kijijini kutafuta mazao, madalali wanamdaka wanamwambia we tulia usihangaike sisi tutakutaftia kwa bei nzuri, wao ndo wanawajua wakulima, wanaenda wanawalangua kwa bei wanayo taka wao madalali, wakipeleka bidhaa kwa mteja wanapandisha cha kwao.

Sasa hiyo nimeongelea wale wakulima wa chini kabisa. Hamna faida ya tofauti wanayopata ila middle men ndo wanafaidika. Mkulima ukigoma kutoa mazao kwa bei wanayotaka wanaenda kusambaza mtaani kwamba bidhaa yako haina ubora. So ili visidode mkulima anaamua tu akubali.

Na kumbuka sio wakulima wote wenye uwezo wa kusafirisha mazao yao wenyewe kwenda nje. Wanawategemea madalali. Things are absurd kwa ground
Mdogo wangu kaanza kutoa mpunga wake huko Moro tani 180,lakini anajiita mkulima wakati huwa ananunua msimu wa mavuno na kuweka store kusubiri bei ipande ndio auze.
 
Wakulima mnaowasema hamuwajui.

Sasa hivi wanao uza ni wafanya biashara. Wakulima wananunua vyakula pia.

Nahisi mnaishi nje ya hii nchi.

Waliuza bei chee sasa hivi wana Lia njaa. Serikali haiwezi kukwepa hii aibu.
 
Nimeona humu watu wengi sana wakiishambulia serikali Kwa kutozuia mazao kuuzwa nje ili kupunguza mfumuko wa bei. Ukweli ni kwamba serikali inaweza kuzuia mazao kuuzwa nje.

Jambo hilo ni hatari sana Kwa mustakabali wa kilimo na wakulima wa Tanzania. Gharama za uzalishaji zimepanda sana, kila nyanja ya maisha vitu vimepanda je hayo mazao ya kilimo yakiuzwa bei chini nani atafidia gharama za ziada?

Mwaka ambao nililaani kilimo ni ule mwaka Serikali ilizuia mazao kuuzwa nje eti kwa sababu ya kulinda bei tuliuza gunia shs 30 elfu hata hivyo hapakuwa nawanunuzi. Kuna kipindi serikali ikatutangazia kuwa itanunua mahindi yetu sijui tani ngapi lkn haikusaidia chochote wakulima tukiendelea kusota na mazao.

Likiwa hilo halijapoa serikali ikakosana na wanunuaji wa mbaazi badala yake nikamsika manyanya anasema mbaazi ni tamu sana wakulima kuleni.

Ndugu zangu soko la uhakika na lenye bei nzuri la mazao yote ya kilimo ni muhimu sana kwa uhai na ukuaji wa kilimo kuliko kushinikiza mazao yashuke bei.

Nakumbuka mama alipo apishwa alizinguka sana kwa majirani kuomba waruhusu mazao ya Tanzania yauzwe kwao. Kuna wakati Kenya walisema mahindi yetu yana sumu ilileta maafa Kwa wakulima
Wewe acha ujinga, Kwanza tambua kwamba Hakuna Maisha kama Hakuna chakula na tambua kuwa njaa haina mbabe, ukitaka wazungu wachukue Mali zetu kirahisi basi ruhusu njaa katika nchi watakuletea chakula Kwa kubadilishana na Mali asili.

Pia naomba uelewe kuwa ni rahisi kuwanyamazisha wakulima Kwa kuwapa pungufu ya walichokistaili kuliko kuwanyamazisha watu wenye njaa,ukiwa rais unapaswa uelewe kuwa kitu muhimu kustable utendekaji WA mipango ya Maisha ya wanainchi.

Kwa maana kuendesha nchi lazima kutegemeane kama ilivyo mbugani ambako Wanyama wanaishi hivyo Kati ya wala nyasi na wala nyama, ikitokea kutokana na mungu alivyotengeneza mazingira yakaenda ndivyo sivyo basi Kuna kundi litaangamia.
 
Back
Top Bottom