Nakuchukia Baba yangu

mkuu, mama aliyetoka kujifungua siku kumi na nne kuanza kufanya kazi sio mateso?
Watoto wadogo miaka 9 na dada yangu miaka 12 kufanya vibarua kwa ajiri ya chakula na mahtaji ya shule hayo si mateso.
Pole sana kijana wangu ila bado nakupa neno, huyo bado ataendelea kuwa babako hadi siku unaingia kaburini.

Baba alishirikiana na Mama yako ukapatikana wewe, wkt mwingine kuna maisha ya kifamilia mamako anajua shida ilipoanzia na hawezi kukwambia.

Mambo ya wanaume kukimbia mke na watoto huwa sitaki kuamini ni mtu anaamka asubuhi na jioni harudi nyumbani kuna sababu tu.

Mimi siafiki hilo lililotokea ila bado nataka kujua (wewe hujui) sababu ya babako kukimbia ni nini?

Ongea vyedi na mamako akupe picha halisi then njoo hapa.
 
Watu wengi hapa wanamshambulia mleta mada na wengine na matusi juu. Chonde tujifunze ku reason kistaarabu kwa faida ya watu wote kwasababu kila mtu anaweza kujifunza kitu kwenye mijadala kama hii. Kila mtu ana haki ya kutetea msimamo wake bila matusi.

Mimi nasema, umasikini Afrika hauwezi kuisha kama tunakimbia responsibilities. Sitaki kuandika ukurasa mzima, lakini niulize nyinyi mnaosema baba ni baba, okay sasa hivi yuko wapi? Au baba ni baba akizeeka au akishikwa na njaa? Sasa hivi mmeamua kumlaumu mama yake bila kujua ukweli, kweli mwanaume na pumbu zako utakubali mtu akuchukulie mwanao?
Kama kweli laana ipo, kwanini wanaotelekeza familia wasipate laana?
 
Wewe unambishia kwamba hakuondoka na mwanamke mwingine, aliondoka na wewe?

Yaani unamjua baba yake mleta mada, kuliko mleta mada ambaye ni mwanae?
Nimeuliza swali, amejuaje kama baba yake aliondoka na mwanamke mwingine? Si ajibu tu..
 
mama yangu tangu aolewe na baba mwaka 1986 hadi leo hawawahi kuzaa na mwanamme mwngn tofauti na baba yangu mimi, na tuko watoto 8 je mama ni singe maza?
Pole sana mkuu. Story yako ni ya upande mmoja, huwezi jua kipi kilitokea nyuma ya pazia kwani muwamba ngoma ngozi huvutia kwake. Muombe sana Mola akuepusha na roho za visasi.
 
Amina
 
Shukuru Mungu upo salama.
Huwezi jua kiburi na dharau alizopata toka kwa mama yako hadi kuamua kuondoka, sumu uliyomezeshwa kuhusu baba yako unapaswa kuitema.
Msingi na sekondari wanaume, huwa tunajitahidi sana kulinda legacy ya familia kwa kukaa kimya hata km tunachafuliwa kwa uongo usiokuwa na maana.
Mm nilikuwa km ww lakini nilipokuja kugundua ukweli sahihi, nilienda kuomba msamaha kwa baba yangu.
 

Bro, dharau kutoka kwa mwanamke ndio excuse ya kuacha watoto wateseke? I'm trying to understand you lakini ubongo wangu hautaki.
Nikuulize, una watoto?
 
Bro, dharau kutoka kwa mwanamke ndio excuse ya kuacha watoto wateseke? I'm trying to understand you lakini ubongo wangu hautaki.
Nikuulize, una watoto?
Dharau niliyoongelea hapa siyo nyodo wala kujibiwa vibaya.
Ulishawahi kujiuliza kwa nn watu wanaachana na kila mmoja anaamua kuanza maisha upya kwa namna anayoijua yeye?.
Anyway, mm niliambiwa pia mzee wangu aliniacha nikiwa mdogo, lkn nilipokuja kugundua ukweli halisi ilibidi nikimbie kwa mzee wangu kuomba msamaha.
Wanawake ni mama zetu na tunawapenda sana lkn tuishi nao kwa akili
 
Kuna wakati mtachukia baba zenu lakini mkae mkinua kuna wakati mama zenu ndio matatizo makubwa ndio maana baba zenu wanaamua kuondoka ili mama abaki mwenyewe .
Kabla ya kuchukia tafuta kujua root ya yeye kufanya hivyo na huwezi tu kuambiwa hivi kama utaweza kufunuliwa hata kiroho itakupa foundation na utajua namna ya kutatua .. chuki ni lowest vibration kabisa
 

Kuachana na kutelekeza watoto ni vitu tofauti. Wewe unaachana na mama si watoto.
Nimekuuliza swali, wewe una watoto?
 
Subiri na wewe uwe baba ndo utajua masahibu aliyokua anapitia baba yako!!!

Wanawake ni miongoni mwa viumbe hatari especially hawa single mingle mazazi
Mvulana kamwe hawezi kuielewa hii kauli ila ngoja awe mwanaume sasaa ndio atakuja kuelewa kipi ulimaanisha
Binafsi kabla sijaoa (kipindi naishi na wazazi) nilikua upande wa Mama kwenye matukio mengi nikiona kuna kutokuelewana baina ya wazazi wangu japo kuwa ilikua changamoto ndogo ndogo
Ila baada ya kuoa tuu ndo nikaelewa nafasi ya Baba, na kuanzia hapo nilizidisha Mapenzi makubwa mnoo kwa marehem Baba yangu, Mungu amuweke mahala pema
Wanaume tunapitia changamoto kubwa saana kwenye mahusiano ni vilee tuu huwa hatuna muda wa kulalamika lalamika
 
Kujipatia tu ushaanza kuchukia wapenzi. Na haujawahi jua kwanini Mzee akiondoka nyumbani.

Kaa kwanza na wanawake ndio ujue kwa nini wazazi huwa wanaacha familia zao na kwenda kusiko julikana.

Cha msingi wewe endelea na maisha Yako .. chuki mwachie mama Yako..mpenzi wake na baba Yako.
 
Mkuu umeoa, je una watoto?
 

Mkuu, watoto waliotelekezwa wote hawako sawa mpaka wapewe maelezo ya kueleweka. It's not easy for them like that. They want to know the truth
 
Ni kweli mwanaume haamki tu na kukimbia familia au watoto, huwa inawezekana amekutana na mchepuko uliompumbaza, ulevi au kuchanganyikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…