Nakuchukia Baba yangu

Nakuchukia Baba yangu

Hakuna mwanaume hapendi familia yake
Iweje ugomvi wao na mzazi mwenzie hasira na adhabu iwe kwa watoto? Nimeshaona saaana kwa ndugu jamaa na marafiki sa zingine akili inawapungua kuhisi asipohudumia watoto mama atashika adabu which is upumbavu kabisa
 
Hii story ya wewe kutusimulia habari za wakati una wiki 2 hauwezi kuwa ni zako, umesimuliwa na mama yako baada ya baba yako kumkimbia alipomfumania na mwanaume mwingine. Baba yako akajua wewe siyo mwanae akaona ajiondokee tuu.
Wanaume tuna mengi ya moyoni hatuwezi waambia watoto wetu ni aibu.
Kama una kifua mwambie baba yako akwambie kwanini alimkimbia mama yako ambae ni mwanamke akachukua mwanamke mwingine,
kama nilikuwa na wiki mbili tangu nizaliwe niliwezaje kwenda kwenye vibarua nikitoka skuli? Rudia kusoma thread yangu.
 
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo

Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!

Kwa kuwa hujui mengi yaliyo msibu baba yako mpaka akatoroka, usimchukie. Wewe endelea na maisha yako. Usimpe nafasi moyoni mwako. Kiufupi mpotezee tu ili uwe na amani moyoni mwako. Kama ukiweza msamehe pia, maana tunavyosamehe wengine na kujisamehe sisi wenyewe ni kwa faida yetu wenyewe tunao samehe. Tunajipunguzia mambo mengi sana magumu tukiwa na moyo wa kupuuza na kuachia mambo yapite. Let it go.
Hata ikitokea baada ya muda mrefu amekuja kwako mpokee bila masimango. Sisi wababa huwa tunapitia mengi, lakini hatuna hulka ya kuongea.
kuna mmoja hivyo hivyo aliiachia mji familia baada ya kuthibitisha pasipo shaka, watoto wawili wadogo kati ya watatu, hawakuwa wakwake. Aliwatelekeza wakati yule mkubwa akianza form 1. Alirudi kufunua hiyo issue baada ya mtoto mkubwa yuko chuo kikuu. Yule kijana akamuomba sana msamaha baba yake na kutaka kumuwashia moto mama yake. Lkn yule baba akamuomba asifanye hivyo kwani huyo hata kama kafanya makosa bado ni mama yake. Hivyo, wababa wana mengi. Hivyo wasamehe tu so long as huna taarifa sahihi za upande mwingine
 
Iweje ugomvi wao na mzazi mwenzie hasira na adhabu iwe kwa watoto? Nimeshaona saaana kwa ndugu jamaa na marafiki sa zingine akili inawapungua kuhisi asipohudumia watoto mama atashika adabu which is upumbavu kabisa
Kama umeshindwa kuwalea wapeleke kwa baba yao!!! Hunipendi mimi na hela zangu zichukie pia
 
Kwakua wewe ni mtoto na hujui sababu ya baba yako kukimbia. Wewe sio lazima umpende ila cha kukusaidia usimchukie mtu usiyemjua.

siku ukija kufahamu ni mama yako ndio alimkimbiza kwa kumtamkia kuwa "hawa sio wanao" sijui utajisikiaje.

Ngoja na wewe uwe baba, halaf uyajue mazonge ya akina mama ndio utapata fursa ya kutafakar sawa sawa
kuna mengi ya kuzungumza,msimlimbikizie mama kuwa mwenye tatizo,ndio mana nikawaambia kuwa siku nyingine nitawaletea kisa na mkasa wa baba uliomsababisha aondoke, na nitabia yake tangu mwanzo,nimewauliza watu wazima ambao wameona ukuaji wa mzee akiwemo bibi mzaa mzee wangu. So usikimbilie kutoa hitimisho ili hali mada haikuisha mkuu
 
kama nilikuwa na wiki mbili tangu nizaliwe niliwezaje kwenda kwenye vibarua nikitoka skuli? Rudia kusoma thread yangu.
Nimekuelewa, kwahiyo huyo mdogo wako akiyezaliwa 2011 na wiki mbili baadae baba yako akakimbia ndo alisababisha mgogoro wa baba na Mama yako?
Sijui unanielewa,?
 
Kama umeshindwa kuwalea wapeleke kwa baba yao!!! Hunipendi mimi na hela zangu zichukie pia
Wise men hata hawawezi kuwaza ivo, nafikiri pia umasikini ndo uanchangia mtu kuwaza nikilea mtoto mama anafaidika, ila kwa wenye pesa hata huwa hawawazi watoto wakae wapi, wanasomesha watoto mashule mazuri kabisa na watoto wanalelewa na mama
 
Nimekuelewa, kwahiyo huyo mdogo wako akiyezaliwa 2011 na wiki mbili baadae baba yako akakimbia ndo alisababisha mgogoro wa baba na Mama yako?
Sijui unanielewa,?
itabidi nitulie mkuu niandike thread nyingine, kuelezea history ya mzee wangu tangu amuoe mama,na story hii nitakayoisimulia skusimuliwa na mama yangu mimi,bali nilisimuliwa na mama yake baba ambaye ni bibi yangu mimi. Yani hapo kumuacha mama akiwa na wiki mbili akiwa amejifungua na mdogo wangu huyo kichanga kuwa sababu si kweli ni tabia ya mzee toka ukuaji wake.
 
Usihukumu kwa kusikiliza Upande mmoja, Huenda hayo ni maelezo uliyopewa na mama yako, Jaribu kuketi na kusikiliza upande wa pili, Huenda ukabadili mtazano wako.
 
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo

Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
KADRI MTOTO WA KIUME ANAVYOKUA NDIVYO ANAZIDI KUMUELEWA NA KUMSAMEHE BABA YAKO

Utakua na familia na wewe utaondoka nyumbani kumuacha mke wako bila kumpa taarifa/sababu ya kuondoka

We pass through alot bro , How can you hate what you don’t know.

Ni sawasawa na kuchukia kitu ambacho hujawahi
 
Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo

Baba yangu aliondoka nyumbani 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha kakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.qq

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefka hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Mkuu pole sana
Hali ambayo unapitia hata mimi pia nimepitia_nimelelewa na mama kuanzia nipo mdogo hadi nimefika hapa nilipo,mama amejitahid kwa mchangi wa asilimia 98 hadi sasa

Nashukuru mungu simchukii baba angu bali nimeamua kumsamehe na kuootezea kwani sijui nini alipitia na changamoto gani alipitia hadi kufikia hali ya sasa,pia hata nawasiliano huwa nampigia na kumsalimia na hata kwenda kwao na kunsalimia akuwa yeye na familia yake,

Hata huo mchango wake wa asilimia 2 bado naushukuru

#tujifunze kusamehe sometimes wazazi wetu wanaakua kukwepa majukumu kwa changamoto mbalimbali kama vile uchumi mdogo,

#chuki binfsi na makasiriko ya mzazi(mama) kutokana na kuachiwa majukumu isiwe sababu ya kuwachukia baba zetu
 
Mm ni mhanga tena bora ww , story yangu ni ndefu mno lakin nakupa tu kifupi baba alikua askari lakin sisi watoto wote hajatusomesha yaaan yeye ndo alikua kikwazo cha sisi kusoma, mimi kwa uwezo wake mungu nikasoma kati yetu watoto watatu , baba aliwafanyia watu connection wakawa ma askari lakin sisi watoto wake hakuwahi kuthubutu, story ni ndefu mno nakupa tu summary sitaki kusema mali alizokua anamilik, sitaki kusema watoto wa nyumba ndogo ambao sio wake walivyokula mali zetu,
ni story ndefu naweza andika kitabu , mimi mungu alinitendea muujiza nimesomeshwa na mzungu , kutoka german, na kipind hiko baba bado yupo kazini na sikuwahi dhubutu kumwambia matatizo yangu yule mzungu, nilipewa kadi ya benk mpk leo ninayo nilikua nawekewa ada na pocket money kila mwezi suala la alinilipiaje lipiaje ni suala jingine, nimemaliza chuo mzee wangu hajui km nimesoma, nilikua na chuki sana moyoni na sikuweza kusamehe, nilikaa muda mlefu sana nna chuki moyoni namchukia sana mzee wangu,
siku moja moyo ukaniambia nitoe sadaka kwa baba yangu yule yule ninaye mchukia , haikua rahis ila nilipata pesa nikanunua nguo nzuri sana nikatuma mtu akapeleka maana mda huo tulikua hatukai nae alitufukuza sis na mama yetu,
baada ya sadaka hiyo mim ndo nilipata kazi, hebu fikiria nimemaliza kozi ya afya nimekaa home miaka miwili kila sehem nakosa kazi, had kujitolea nakosa na ni miak 7 iliopita sio leo....................................
Mkuu usimchukie Baba yako tena na alikua na mke mdogo wanawake wanatabia ya kuharibu mahusiano ya kwanza ya Wanaume ili wao na watoto wao wapate raha, yani mara mia kua na Baba mlevi tu kuliko na kua na Baba anae penda wanawake sana mzazi kama anaependa wanawake lazima Nyumbani mambo yatakua magumu Sana na familia itaishi kwa tabu sana. Utakuta Baba kapata mchepuko nje uko sass pesa zote zinaenda uko na nyinyi nyumbani mna kula mlo mmoja na Mchepuko ndiyo anazidi kuroga.
 
Back
Top Bottom