Nakuchukia Baba yangu

Nakuchukia Baba yangu

kuna mengi ya kuzungumza,msimlimbikizie mama kuwa mwenye tatizo,ndio mana nikawaambia kuwa siku nyingine nitawaletea kisa na mkasa wa baba uliomsababisha aondoke, na nitabia yake tangu mwanzo,nimewauliza watu wazima ambao wameona ukuaji wa mzee akiwemo bibi mzaa mzee wangu. So usikimbilie kutoa hitimisho ili hali mada haikuisha mkuu
Sasa sisi tuna comment kwa yale umeandika maana hatujui nin hujaandika bado
 
itabidi nitulie mkuu niandike thread nyingine, kuelezea history ya mzee wangu tangu amuoe mama,na story hii nitakayoisimulia skusimuliwa na mama yangu mimi,bali nilisimuliwa na mama yake baba ambaye ni bibi yangu mimi. Yani hapo kumuacha mama akiwa na wiki mbili akiwa amejifungua na mdogo wangu huyo kichanga kuwa sababu si kweli ni tabia ya mzee toka ukuaji wake.
Kama ndo tabia yake huyo baba yake basi itoshe kusema mama yako hakupata mtu sahihi kwenye maisha. Hilo linaweza kumtokea mtu yeyote. Sasa wewe hutakiwi kuiga tabia mbaya ya baba yako ya kutelekezana. Ukiiga hiyo tabia ukamfanyia baba yako, Sasa tofauti yenu iko wapi?
Angalia hiyo roho mbaya ya baba yako isikuvae. Muombe Mungu hata kizazi cha nne kisichukue hilo pepo.
 
Mimi dingi yangu aliwahi ninyima chakula siku kadhaa na wanakula hapo na mke wake (mama wa kambo). Wanakucheka!!

Niliwahi kuumwa kwa kuzidiwa kabisa nimelala karibu na uwani kwasababu nilikuwa natapika saaana (wakati mzee anatoka bafuni na mkewe ikabidi nimwombe angalau ela niende hosp kucheki maana hali ni mbaya) " kauli aliyoniambia ni kwamba we unayo?'" yaani hio ela nnayo omba mi nnayo?? Ikabidi niseme Sina.. nayeye akajibu Hana pia!!

Niliwahi fukuzwa home, sio mara moja!

All in all mzee wangu (dingi) namkubali sana pamoja na yote..

Nilishaapa sana kwamba haitakuja kutokea nimkubali!! Lakn ndo hivyo akiwa na shida akikucheki tu! Mtu upo tayri uazime ela sehem umtumie (I don't know hii Hali inakuwaje kuwaje)
Una uhakika ni babako?
 
Ww una nn mpka sasa? Kumpita baba yko.
nipo hivi nilivyo kwa sababu ya baba yangu! Labda baba yangu angeamua kutulea ktk njia anayotakiwa kumlea mwanae nisingekuwa kapuku,maskini,mbangaizaji na hohehahe kama nilivyo sasa. Kidato cha nne nilifaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita,ila sikwenda kwa sababu ya ukata, wenzangu niliosoma nao wapo mwaka wa tatu vyuo vikuu,mimi sjui future yangu,ila ushauri wa wadau nimeufanyia kazi,na kesho naenda kukutana na baba yangu. Kwani nimepigiwa simu sasa kuwa umetokea msiba wa babu yangu mkubwa upande wa baba kuwa amefariki na mzee kanihimiza niende,hivyo naenda kukutana nae na ikiwezekana nirudi nae nyumbani kwa mama, pombe ndio chanzo kikubwa cha baba kufanya hayo yote. Ahsanteni wote mliotoa ushauri wenu mkiongozwa na Mshana Jr
 
kama nilikuwa na wiki mbili tangu nizaliwe niliwezaje kwenda kwenye vibarua nikitoka skuli? Rudia kusoma thread yangu.
Huyo mtoto mwenye alikua week mbili ndio chanzo babako kukimbia, muulize mamaako vizuri huyo ni mtoto wa babaako kweli au?
Haiwezekani babaako akimbie baada tu ya mtoto kuzaliwa.
Si angekimbia Mimba basi,
Jifikirie
 
Kama baba anakuja mara moja moja, basi sio single mother, ila wadau wanachokueleza ni kuwa mama ndio anaweza kuwa msababishi.

Sababu ingekua tatizo ni fedha faza asingeoa mke mwingine maana huyo mke angemkimbia tu. Tatizo linaweza kuwa ni bi mkubwa hapo
Tatizo linaweza kuwa mwanaume pia
 
Back
Top Bottom