Wakuu habari!
Mimi ni mtanzania kijana nilie graduate chuo mwaka huu nikitokea mkoani kanda ya ziwa, kwanza niweke wazi kutokana na trend ya ajira ilivyo nchini nimeamua kupambana na kuhangaika mwenyewe katika nyanja ya kujiajiri maana nikitegemea ajira ya serikali naweza kufa njaa na ndoto zangu zisitimie maana umri pia unaenda, nimesoma education (science) naelewa ajira zitakuja lakini nataka niweke vyeti kabatini nipambane ajira zitanikuta mbele ya safari huko.
Katika maisha yangu ya kusoma ndoto yangu kubwa ni kufanya biashara ili niweze kujikwamua kiuchumi japo naelewa kwa sisi watoto wa maskini safari ni ndefu saana, nilipokua chuo nimefanikiwa kusave boom langu kwa kujibana saana nimefikisha 1 million. Najua kwa watu wengi hii Pesa ni ndogo na ni matumizi ya week tu au mwezi lakini kwangu ina maana kubwa sana maana naelewa inaenda kunikomboa.
Japo pia naelewa "safari ya maili 1000 uanza na step moja"
Idea yangu kuja kufanya dar ni hipi?
Naelewa Dar ni mji Mkubwa hata mzunguko kwa biashara ni Mkubwa pia, ninayo access ya kupata dagaa wakavu (dagaa kauzu) kutoka gosber kisiwani so idea yangu ni kuleta dagaa huko Dar ninao mtaji wa kuanza na gunia 10. Japo lengo langu kubwa ni kuleta nafaka zote pamoja na mafuta ya alizet though mtaji wangu ni mdogo nataka nijikite kwenye dagaa kwanza then mwangaza wa asubui ukishaonekana basi naweza fungua ofisi kubwa nianze kuleta hivyo vitu.
Nilitaka nifike dar kwanza nifanye research nizunguke kwenye masoko mbali mbali nataka niuze jumla kwa madalali na rejareja NIKIPATA MEZA SOKONI ITAKUA VIZURI (japo sijui nitapataje).
WAKUU KWA SABABU MTAJI WANGU NI MDOGO NA CHANGAMOTO YA DAR NI SEHEMU YA KUKAA NA KUKAA KWA MTU NI NGUMU KUTOKANA NA HALI YA MAISHA YALIVYO (kila mtu anashida zake)
Next week nakuja kufanya research ya maeneo kuongea na madalali na kutafuta eneo langu la kufanya kazi.
Nilikua natafuta chumba sehemu ya kujishikiza (sio kufikia kwa mtu) ambapo mwenye nyumba atanikubalia kulipa kodi ya Mwezi mmoja huku Mimi nikiendelea kufanya research zangu kuhusu hiyo biashara endapo nikipata godoro nitashukuru sana.
Asanteni.