Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Huyu dogo anatafuta kazi hajaomba kutumiwa fedha, picha yake ipo hapo juu mimi nimekutana nae na kumsaidia kumpeleka kituoni na kumuonyesha magari ya kufika baracuda, atafanikiwa tuu na nyie mtabaki na aibu, Mungu ni wa ajabu sana jana hajalala nje, leo kapata hela ya kula na hatalala nje mnaobaki kuwa na mawazo hafifu ndio mnahisi ni tapeli, hajaomba mtu hela, anatafuta kazi hizo hela watu wamemtumia kwa kumuonea huruma...usihukumu mzee chukua muda wako mtafute ni mgeni dsm hapajui ila ni fighter na ana confidence za ajabu atatoboa tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu niko upande wako napingana na wote wanaomdhania janja ni tapeli! Mungu akubariki sana kwa vile ulivyotoa kwaajili yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza haiingii akilini mtu utoke nyumbani from no where uende mjini hujui unapokwenda kuanzia, especialy watu wa vijijini huwa ni waoga wa maisha atlist angekua mtu ambae ameshakaa mjini ni rahisi kwenda kutafuta maisha popote ila hawa wa vijijini mara nyingi huwa wanategemea kuvutwa na ndugu au marafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Wale wanaozamia meli na kwenda ulaya? Mbona wapo wengi wanakwenda South Africa au China hawajui wapi pa kufikia. Sijajibu hapa kwa kumtetea dogo ila naipinga hii hoja yako.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Jamani huyo ni muongo kasema yupo kwenye gari nimsubiri barakuda tabata nimeganda ofisini mpaka saa 3 usiku hajatokea toa namba hatoi...sasa mnaomsaidia endeleeni mimi nimejitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiangali comment ya dogo kufika baracuda ilikuwa ni saa mbili na nusu kama sikosei ila ni mida hiyo kabla ya saa tatu na alikuwa akisema eti kuwa eti wewe hujibu PM alizokutumia eti. Sasa na wewe umekaa ofisini unamsubiri eti mpaka saa tatu eti hujaona Pm eti. Dogo anaweza kuwa tapeli huyu eti.

Naendelea hapo chini...
 
Kujiuliza ni lazima lakini napata ukakasi kuna member humu kakutna nae makumbusho na kampa nauli na picha ya huyo dogo ikapostiwa humu akiwa ndani ya bus. Ina maana kama dogo ni tapeli ina maana hata member mwenzetu aliekutana nae alishindwa kulitambua hilo??

Ile picha ya dogo inaweza kukushawishi kuamini dogo anahitaji msaada lakini pia ujuzi wake wa kuitumia JF kama kuquote na kutag watu ameajuaje haraka hivi na ilhali yeye ni darasa la Saba?? Sijui walomtumia pesa waliongea nae vipi japo kwa njia ya simu ni rahisi kupigwa changa la macho.

Kama ni kweli anahitaji msaada hapa tutajifunza kitu kwenye maisha kupitia safari ya huyu dogo na kama ni tapeli pia tutajifunza kitu kwenye maisha yetu. Tuendelee kuendelea hapo chini mkuu

Naendelea hapo chini...
Atlist tungepata uthibitisho kutoka kwa watu watatu au zaidi maana onthe other side unaweza kukuta hao jamaa ni mtandao mmoja, all in all tunahitaji kujiridhisha ndio nia yetu, hatupo hapa kwa ajili ya kumjudge ila lazima tujiridhishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu niko upande wako napingana na wote wanaomdhania janja ni tapeli! Mungu akubariki sana kwa vile ulivyotoa kwaajili yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu amefika hadi baracuda kufuata kazi aliyoahidiwa bado wanamuona chenga, dogo kakimbia hali ngumu alipotoka kuja kutafuta maisha na simu yake ni tecno ya button hana smart phone, huko alipotoka kapigika haswa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili sakata kama la korosho mara wenye korosho waoneshe mashamba
 
Atlist tungepata uthibitisho kutoka kwa watu watatu au zaidi maana onthe other side unaweza kukuta hao jamaa ni mtandao mmoja, all in all tunahitaji kujiridhisha ndio nia yetu, hatupo hapa kwa ajili ya kumjudge ila lazima tujiridhishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika mkuu. Lengo ni kujiridhisha

Naendelea hapo chini...
 
Nimeongea naye.
Yupo Mbezi Magari saba (sina uhakika kama nimepatia.)
Ila amepata msamaria mwema wa kwenda kulala kwake hivyo huyo msamaria mwema amesema anatuma pikipiki imfuate hapo alipo.
So ndiyo anasubiri.
Ila kuhusu kazi ndiyo bado hajapata.
So aliamua kuchomoka toka baracuda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom