Asante sana Rafiki yangu...Mimi nakutakia mafanikio...ila Cha kukushauri kama hiyo JKT Yako sio ya mujibu...Ni wale wa kujitolea hakikisha unasoma fani ndogo ndogo...kama udereva...uchomeleaji au upakaji rangi...
Fani hizo zitakuongezea sifa ya kuajiliwa kwenye majeshi yetu.
Ukifanya vizuri kwenye hiyo kazi connection zipo nje nje...
Mimi ni mlinzi nilie amua kustaafu 🤣🤣🤣 ila amini nakwambia kupitia ulinzi Leo hii spika wa bunge ananifahamu japo hajanisaidia chochote🤣🤣🤣🤣
Nilishawahi kukutana uso kwa uso na aliekuwa IGP Simon Nyanghoro Sirro na Tip alinipa.
Niliwahi kukutana na waziri Wilium Rukuvi akiwa yeye na Familia yake huyu alinifanya niongeze Kasi ya kupambana maana eneo nililokuwepo alikuwa ananunua vitu vya bei mbaya bila kuomba discounts 🤣🤣🤣
Wasanii mbali mbali niliwahi kukutana nao na wengine Nina wasiliana nao hadi Leo.
Ila chanzo Cha kufahamiana na wote hao ni kazi ya ulinzi. Broh usikate tamaa itumie hiyo fursa kama daraja tu la kukuvusha...
Mwenyezi Mungu akupe hitaji la moyo wako, akupe matumaini na akuondolee machungu, ulionalo gumu liwe jepesi🙏🙏🙏🙏