Nakwambia nimewaka ile ngumu!

Nakwambia nimewaka ile ngumu!

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
3,371
Reaction score
2,713
Ndugu zangu mwenzenu nipo katika majuto mjukuu
Kwa matumizi niliyokuwa nafanya wakati ule ni mabaya sana.

Nilipokuwa na pesa mfukoni matumizi yangu yalikuwa niya hali ya juu sana. Na nilikuwa napata pesa nyingi sana

Nikawa natafuta marafiki naenda kutumia sasa pesa zimeniishia Nguvu moja sina la kusema marafiki zangu wote wamenikimbia... Wakati ule nikiingia kwenye Bar/Hotel nawaambia marafiki kuleni kunyweni.

Sasa hivi wameniona nimewaka wananikimbia na wengine wananikebehi kwa kuniomba buku/ 1000/= wakati wanajua nimewaka ile ngumu na wengine wananicheka na kuniambia ndio ukubwa huo.
 
Sina la kusema wakuu sasa
Hata chenji ya shiling 50 mwenye duka namdai...maisha haya!!
 
Bora wewe unatumia na rafiki zake hata kama wamekutosa ipo siku watarejea, mimi ninapepo la kutokukaa na pesa nazitumia kama nina kichaa nikiingia sehemu ya starehe na 300k subaki hata na mia
 
Bora wewe unatumia na rafiki zake hata kama wamekutosa ipo siku watarejea, mimi ninapepo la kutokukaa na pesa nazitumia kama nina kichaa nikiingia sehemu ya starehe na 300k subaki hata na mia
Unatakiwa ufanyiwe maombi mkuu
 
Unatakiwa ufanyiwe maombi mkuu
Mkuu hapa nimehudhuria makanisa mengi sana kwa minajiri hiyohiyo ya maombi lakini wapi... Pepo halijaniacha hamna dini kubwa ambayo sijapita kusali.

Imebidi nikae tu nijiombee mwenyewe labda linaweza likaniachia maana Mungu anasikia zaidi maombi yako binafsi na si yale yanawasilishwa na mtu mwingine kwa niaba yako
 
Haha umenikumbusha mbali sana mkuu

Ngoja ninyamaze,ila najua pia ulikuwa hupokei ushauri mzuri kutoka kwa some of your friends
Wee acha tu kiongozi, bora unyamaze
Usinikumbushe machungu.
Jamaa walikuwa wananipamba na kuniita
Mzee wa bata
 
Back
Top Bottom