"Nakwenda yaani basi tu" kauli hii imeninyima raha sana

"Nakwenda yaani basi tu" kauli hii imeninyima raha sana

Kirchhoff

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,735
Reaction score
8,541
Wakuu,

Salam.

Juzi nilitaka huyu mwanamke aende mahali kutekeleza wajibu fulani akasema haendi hajisikii kutoka. Nikaumia kidogo lkn nikamezea. Baadaye akaniuliza "mahali kwenyewe ulitaka niende kufanyaje" nikamuambia asiende Tena Kule ambako ni mbali Bali aende kwingine karibu kunisaidia kulipa deni. Akanijibu "Naenda Yaani Basi Tu!" Katika sauti iliyoonyesha dharau kweli kweli.

Ikabidi nimuambie kamaa hataki kwenda aache tuu nitaenda mwenyewe na kumtaka aniandalie nguo. Baada ya Muda nikaingia chumbani nikakuta kaweka Suruali na mkanda anaendelea kutafuta nyingine. Huku natoka nje nikajisemea "niandalie nguo nzuri Ili nisherehekee Eid Huko huko (sio muislam Mimi though)".

Nikaendelea na shughuli nyingine nikisubiri niambiwe nguo tayari. Baada ya Muda namuona nje kabafikisha nguo tayari kwenda mjini ananiuliza "hiyo Hela Iko wapi nipeleke?" Nikampatia akapeleka.

Toka Jana najiuliza sana je ilikuwa Sahihi kunijibu vile Mimi Mume wake "naenda yaani basi Tu?"

Bado sijaliongelea hili suala nasubiri hasira ziishe na niwe na maswali mengine mawili matatu Yaa kumuhoji. Muda mwingine sioni Kosa kuliona ni lijanamke.

Ni vile sina mkono wakupiga mwanamke ningeshasambaratisha sebule.
 
Una gubu kha!! Ina mana hapo hujaelewa nn? Hakua na mood ya kutoka, hakujiskia kwenda kokote hio siku, na alienda akuridhishe tu sasa shida iko wapi?? punguza gubu na maneno madogo madogo yanakosesha furaha ya nyumba.
 
Hadi sasa unajua sababu iliyomfanya atamke hivyo?

Je, alikuwa kachoka, alikuwa na uchovu, alikuwa akijisikia uvivu, alihitaji company n.k?
 
Jamani wajameni...hivi ndoa ni kitu gani. Mbona tunachokifahamu na kilichopo ni vitu viwili tofauti. Wengi wetu tunadhani ndoa ni raha, furaha, amani, kicheko, kuelewana, kupatana tu. Yani ndo kila mtu anadhani hivyo na anategemea hivyo kwenye ndoa zetu.

Lakini hakuna anaetaka makuzi, uchokozi, matusi, kejeli sometimes na dhihaka, sometimes kudharauliwa pia. Jamani eeh haya pia yapo. Kuna muda wanawake wanakuwa na gubu la.mawifi usiombe. Kuna muda wanaume hawaelewi somo hata usemeje mwanamke utahisi mume ana dharau, hakupendi tena..sijui upendo umeisha. Na mwanaume na wewe utasema huyu kashapata bwana mwngne...

Hivi ni vitu vidogo sana ongea nae mwambie hujapenda af aombe msamaha. Asipojishusha you can chose to forgive kwa afya ya akili yako. Msifikirie ndoa ni vcheko saa 24 ebooo...kubalini na makuzi yake!!!!

#itsworthit#
 
Nanukuu;-
"akasema haendi hajisikii Kutoka"
"mahali kwenyewe ulitaka niende kufanyeje"
"Naenda Yani basi tu"

Pole sana mkuu, hizo kauli zitakua ni za makasiriko ya kukosa mualiko na Zawadi ya Eid.

NB;-
Hongera kwakutokua na mkono mwepesi.
 
Hiv wanaume jaman mna nn, hamjawah kuwaza na ss n binadamu kama nyie.

Kuna wakat hujisikii kutoka hata nje ya nyumba, sasa aksema ukweli mnahs n ujeuri na dharau jaman.

Mtu amekuambia ukweli kuwa "haendi hajisikii Kutoka" lkn bado ukamshinikiza, kwa kuwa ww n mwanaume na hutakiwi kupingwa( vle mjionavyo).

Wakat mwngne mnafanya mambo yawe magumu, alivyokujibu jibu la kwanza ww ungeenda kujiandaa uende ww. Unaweza mlazmisha akaenda pata ajali akavunjika uti wa mgongo sjui utasemaje!?
 
Back
Top Bottom