"Nakwenda yaani basi tu" kauli hii imeninyima raha sana

"Nakwenda yaani basi tu" kauli hii imeninyima raha sana

Japo sometimes Mimi Nina mfumo dume hila hapo sijaona kosa la shemeji
Jibu la shemeji yanaacha maswali mengi , 'Naenda lakini basi tu' hiyo basi tu , kuna kitu hakipo sawa na jamaa hajui ni kipi!
 
Wakuu,

Salam.

Juzi nilitaka huyu mwanamke aende mahali kutekeleza wajibu fulani akasema haendi hajisikii kutoka. Nikaumia kidogo lkn nikamezea. Baadaye akaniuliza "mahali kwenyewe ulitaka niende kufanyaje" nikamuambia asiende Tena Kule ambako ni mbali Bali aende kwingine karibu kunisaidia kulipa deni. Akanijibu "Naenda Yaani Basi Tu!" Katika sauti iliyoonyesha dharau kweli kweli.

Ikabidi nimuambie kamaa hataki kwenda aache tuu nitaenda mwenyewe na kumtaka aniandalie nguo. Baada ya Muda nikaingia chumbani nikakuta kaweka Suruali na mkanda anaendelea kutafuta nyingine. Huku natoka nje nikajisemea "niandalie nguo nzuri Ili nisherehekee Eid Huko huko (sio muislam Mimi though)".

Nikaendelea na shughuli nyingine nikisubiri niambiwe nguo tayari. Baada ya Muda namuona nje kabafikisha nguo tayari kwenda mjini ananiuliza "hiyo Hela Iko wapi nipeleke?" Nikampatia akapeleka.

Toka Jana najiuliza sana je ilikuwa Sahihi kunijibu vile Mimi Mume wake "naenda yaani basi Tu?"

Bado sijaliongelea hili suala nasubiri hasira ziishe na niwe na maswali mengine mawili matatu Yaa kumuhoji. Muda mwingine sioni Kosa kuliona ni lijanamke.

Ni vile sina mkono wakupiga mwanamke ningeshasambaratisha sebule.
Pole ila inategemea na wewe umem-treat vp saa ingine polite language kwa wanawake Huwa wanaichukulia kama anakuweza vile, jaribu kuwa harsh unapokuwa unatoa maelekezo kwa mkeo.
 
Hao wake zenu ni maroboti na hawatumii damu???

Haya ndio matatizo ya kuoa wake na kudhani ni watumishi wenu badala ya rafiki na patner wa gurudumu la maisha.
 
Una gubu kha!! Ina mana hapo hujaelewa nn? Hakua na mood ya kutoka, hakujiskia kwenda kokote hio siku, na alienda akuridhishe tu sasa shida iko wapi?? punguza gubu na maneno madogo madogo yanakosesha furaha ya nyumba.
Kaoa Roboti

Halina hisia

Mipango

Wala taratibu

Kwanza siku hizi hela zinatumwa hata kwa simu
 
swala la kutuma kwa sim yawezekana wapo jirani tu ila kuambiwa naenda bas tu nalo ni kosa kha!
Yani huoni Kosa Hapo?
Wakati namuomba aende nilikuwa kwenye shughuli nyingine ya lazima na yeye hakuwa na shughuli na Jana yake nilimuhoji ratiba yake ya siku inayofuata. (Mimi ni democratic husband). Hivyo wakati namuagiza nilizingatia Hilo. Hakuwa na kizuizi na allikuwa huru kusema "Mume wangu sitaweza kwenda Kwa sababu a,b,c..."

Ikawaje akaenda?
 
Back
Top Bottom