Sababu kubwa ya Tanzania kuwa na squatter nchi nzima ni watu kuwa na mawazo kama yako
Nchi nyingine haujengi tu kiholela ndo maana sehemu kubwa ya makazi ya watu Tanzania ni kubaya sana
ukienda nchi nyingine kama Europe, china, Japan, Korea unajiuliza hawa watu waliwezaje mbona miji Yao mizuri sana Waliwezaje kuwa na miji mizuri ni kwa sababu ya sheria Kali ya ujenzi ambayo huku Tanzania watu akiwemo mleta uzi hawataki kuifuata wanataka watu wajenge wanavyojisikia
Point yako iko tofauti kabisa na mada aloleta jamaa!
Swala la kupanga mji vizuri sio hivyo vibali vya ujenzi. Hizo nchi unazosema Nyumba zao zimepangika ni kwasababu kabla watu hawajavamia maeneo kwaajili ya makazi, serikali inaenda kupima hivyo viwanja inatengeneza mitaa na njia za miundo mbinu yote Kama Maji&maji taka na umeme kisha wananchi ndo wanauziwa viwanja na kujenga(Yaan unajenga nyumba kila kitu kipo hapo). Sasa ni wapi serikali yetu imefanya hivyo? Squatter zinatokea kutokana na watu wa ardhi kutowahi maeneo na kuyapima kabla wananchi hawajauziana. Leo hii mtu ukiwa tu na shamba lako kisemvule basi unalikata viwanja vidogovidogo vingine hata havitoshi kujenga Banda la ng’ombe!! watu wanauziwa wakianza kujenga ndo Halmashauri zinakuja kudai kibali cha ujenzi!(ujinga mtupu).
Squatters hazisababishwi na vibali vya ujenzi wa Halmashauri.