Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?


Nutella na asali.....interesting....
 
Relax, take a back seat and enjoy the view. kama unachosema ni sahihi hayo mambo ya kawaida kabisa. Hata wewe kuna vitu unalalamika ni ubinadamu tu, vitu vingine vidogo vidogo kama hivi haviwezi kukosekana vinginevyo labda useme ulitegemea "a perfect relationship"!. By the way ngoja nikuchekeshe kuna mdada yeye akimuandaa mume asubuhi jamaa anazingua ile mbaya utasikia hiyo nguo sitaki nipe ile au hata kuchagua mwenyewe wakati mwingine, sasa siku akiachwa achague pia anasema, "mke wangu wewe ndiyo mamaa hebu nichagulie viwalo bwana" yaani alimradi ni ubinadamu tu.
 

Ni kwa nini mchuniane? hilo linalofanya mchuniane huenda likawa sehemu ya malalamiko yake,rekebisha kama linarekebishika wakati ukiendelea kutafiti kiini cha malalamiko yake.Kuhusu simu jitahidi kuiepuka wakati uko na mumeo,hata kama utaona kuwa yeye yuko nayo busy, Jizoeshe kumshukuru kwa kila anachofanya kizuri na uombe msamaha pale unapokosea,asante mume wangu,nisamehe mume wangu yaweke kwenye matumizi ya maneno yako ya kila siku. Usioneshe hasira zako waziwazi mbele yake pindi akikuudhi,na usiongelee jambo au kuandika msg ukiwa na hasira,mwanaume hapendi kukaripiwa,subiri hasira zishuke kwanza. Nakuombea ulivuke hili salama,Nami nimepitia kipindi kama hiki ila mwisho wa siku niligundua tatizo nikasolve.
 
Tubarikiwe sote sist, nimefurahi kama umepata japo ujumbe wa kuutuliza moyo wako... Usibadilishe hayo uyatendayo kwani lawama zitazaa ugomvi. Keep it up nadhani unakumbuka ushauri wangu kwa Mr
Nakumbuka, ahsante pia
 
Kwakweli kwenye swala la simu naona udikteta wa wazi wazi
 

It's not about psychology, nlichoongea ni mambo ya kawaida majukumu ya mwanamke ndani ya nyumba..... OK hayo ulifanyiwa chuo ulipo graduate unafanyiwa yapi?
 
Mie nadhani sio rahisi kumridhisha mtu yeyote yule, let alone a man. huwezi jua what is enough kwa mtu huyo mpaka uje useme hadharani kwamba umempa vya kutosha. hivi ukija kumsikia anawaambia watu pembeni kwamba hujui kupika, au una mapungufu kitandani...utasemaje...Mie nadhani hakikisha jipe first priority kwanza...just be you fanya mambo ndani ya uwezo wako...sex kwa wanaume ni psych...kufanya different styles au kila kona hizo ni adventures tu na men tunapenda games. lakini sio guarantee ya sex satisfaction...madada wengine mpaka anafikia kusema nimempa hadi kinyume lakini simuelewi huyu kaka...nafikiri just be you, fanya kazi kwa bidii kuwa successful woman, ujenge heshima yako , mheshimu, msikilize....
Pia jambo kubwa wewe una handle vipi mikwaruzano ndani ya nyumba, you should handle them calmly.... nina imagine mama Hillary Clinton ali handle vipi aliposikia mumewe anatembea na monica lewinsky....
 

Wala sijachange kitu chochote naishi maisha ya Kweli kabisa, tena tulivokua tumekutana naona ndo I was faking kujifanya siongei, najifanya sister Maria....tulivozoeana nikaanza kuishi maisha halisi with true colors kupika, kufua n.k nilianza tangu anaishi geto, good thing ananijua in and out kama vile kaniumba yeye lol
 
It's not about psychology, nlichoongea ni mambo ya kawaida majukumu ya mwanamke ndani ya nyumba..... OK hayo ulifanyiwa chuo ulipo graduate unafanyiwa yapi?
Ni Mambo Ya Kawaida Sawa, Ila Ww Unaona Umemaliza Kila Kitu Kiasi Kwamba Unasema Unamfanyia Kila Kitu Lakin Bado Haridhiki!! Mean Umemaliza Kila Linalostahil Yy Kufanyiwa Lakin Haridhiki!!!
 
Sijakuelewa kiukweli, he is 30s I am 20s hebu rudia tena sasa nikuelewe
 

Mmmh jamani huko kwenye sita kwa sita nshasema ni hobby.... Anyway haya bana
 
Ha ha ha maneno yapi
 
Last edited by a moderator:

Nawaz tu......labda bibie anampenda sana mwanaume ........kwa hiyo anajitahidi kufanya kila awezalo kuonyesha upendo wake!!!!!!!
 
Nawaz tu......labda bibie anampenda sana mwanaume ........kwa hiyo anajitahidi kufanya kila awezalo kuonyesha upendo wake!!!!!!!

Inawezekana...tukipenda huwa tunabadilika...
love is blind but the neighbors can see
 
Ha ha ha gelofriend bado tu kutoa michicha ndani ya friji tuingie sie
Hahahha ingieni tu afu junior aje awafungie na funguo. Ila kila kitu kina mwisho wake gelofriend, vumilia tu huku ukiendelea kumuombea. Ndo mumeo, ndo udhaifu wake huo na Inawezekana huo ndo mzigo wake unaotakiwa kumbebea. Ila wewe mtoto ni mbayaaaa jamani hahahhaa
 
Nimesoma nikarudia nikasoma. Sasaaa... dah! ndoa naipenda lakini iko kama itanipita jameni. Una mtoto mdogo, unapata muda wa kupika (sasa sijui ni kila siku?) na chakula unapeleka mezani wewe, unamnawisha mume, mtoto nae anakungoja umlishe, umesema unapasi, unapeleka maji bafuni, unamuandalia nguo, viatu....

Nimetafakariii nikajiangalia ili mimi niweze kuwahi kazini kwa kujihudumia mwenyewe naamka saa 11. Nikihamia nje kidogo ya jiji kuamka itakuwa saa 10. Sasa nikianza kumhudumia na mtoto mkubwa hadi kusafisha viatu si ndio nitaamka saa 9? Kazi za mwajiri ufanye kama mtumwa, urudi home ukiwahi sana saa 12 uvae apron uingie jikoni....kuna viwatu vya kukaguliwa au kusaidiwa homework... sijui nini.... ukimaliza hapo useme ukaoge ujitupe kitandani mwenzio yeye ana nguvu zote wewe mgongo unalia kama vijiti vikavu..

Kama sitapata mume anayeweza kujitegemea kwa mambo na sina hela za kununua mashine za nyumbani (kama heater, mashine za kufulia, sinki la kunawia dining...) itabidi nichague kuwa hausiwaifu tu na sijui kama niko tayari maana nilishagundua siko kwenye kundi la superwomen.

Unajua ni rahisi sana kusema mume anahitaji kufanyiwa kama mtoto lakini mnasahau kuwa watoto wana rewards za kutia moyo. Kwanza unajua hajiwezi kwa hiyo unajiskia raha kumsaidia mtu asiyejiweza. Unaweka na bidii ili kumwelekeza aweze kujitegemea; ukimhudumia hana matusi wala dharau. Wakati mwingine hawaridhiki na unachowapa, wanweza kukulilia hadi ukatamani kuhama nyumba lakini unawavumilia kwa kuwa hawajui chochote kuhusu hela wala mipango. Wanatulilia tu kama sisi tunavyomlilia Mungu. Unaweza kumnunulia nguo ya laki halafu we moyoni unajiskia raha kweli ulivyogharamia gauni halafu unakuta amelivaa anachezea mchanga ila ukimnunulia pipi au chama anashukuru mpaka anakubusu!! Halafu mapenzi yao hayana masharti. Mnakosana, baada ya dk chache anakufata kujaribu kurudisha uhusiano. Vimbwanga vyote atakavyofanya unajua anafanya kwa sababu mtoto. Haya, mtu mzima analinganishwaje na mtoto? Na mtu mzima wa kike yeye ni mtu mzima tu toka utotoni hadi uzeeni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…