Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Sasa Eve wewe kama ni mtanzania wa kawaida unataka kuniambia mke kumnawisha mume ni ishu nayo?!! Acheni utani bana hayo mambo ya kawaida sana kwenye jamii za kitanzania labda kama mnaongelea jamii ya hapo kwa jaluo mtaa wa pili.
Mpendwa umetembelea familia ngapi ukakuta wake wanawanawisha mikono waume zao? Kila kitu utakikuta mezani, endelea mwenyewe. Ni wachache mno honestly, hongereni kwa hilo
 
Mpendwa umetembelea familia ngapi ukakuta wake wanawanawisha mikono waume zao? Kila kitu utakikuta mezani, endelea mwenyewe. Ni wachache mno honestly, hongereni kwa hilo
Huku kwetu uswahilini mambo ya kawaida mnooo. Tatizo huko wanakoiga uzungu uzungu mwingi huwezi kukuta haya mambo.
 
Ubandidu huleta u sexy fulani
unafanya mtu anakuwa addicted na real you ambayo haipati kwa mwingine
na ile hofu ya kukupoteza inajitokeza...but ukiwa mama theresa unakuwa so predictable..
mtu anajiuliza why huyu ana act hivi?au kuna dhambi anaifanya?au yuko desperate kuwa na mimi?
au ni kimeo hiki kinajilazimisha kwangu? but ukiwa real you....ile sexiness inamvuta kila mtu...
'ndo mnaajaziana kila kwenye mapungufu' kila mtu anaziba ya mwenzie....

Kweli, ndo maana huwa nawaonea huruma decent ladies make huwa hawaishwi kuumizwa
 
Mpendwa umetembelea familia ngapi ukakuta wake wanawanawisha mikono waume zao? Kila kitu utakikuta mezani, endelea mwenyewe. Ni wachache mno honestly, hongereni kwa hilo

Sasa naanza kumuelewa housegirl
 
Last edited by a moderator:
Huku kwetu uswahilini mambo ya kawaida mnooo. Tatizo huko wanakoiga uzungu uzungu mwingi huwezi kukuta haya mambo.

Una generalize mambo kama kwako ni kawaida good for you.....
Kama best angu anavonishangaa mie kufua kunyoosha namie namshangaa yeye kulala huku mme wake anafua na kujinyooshea
 
Ni kwa nini mchuniane? hilo linalofanya mchuniane huenda likawa sehemu ya malalamiko yake,rekebisha kama linarekebishika wakati ukiendelea kutafiti kiini cha malalamiko yake.Kuhusu simu jitahidi kuiepuka wakati uko na mumeo,hata kama utaona kuwa yeye yuko nayo busy, Jizoeshe kumshukuru kwa kila anachofanya kizuri na uombe msamaha pale unapokosea,asante mume wangu,nisamehe mume wangu yaweke kwenye matumizi ya maneno yako ya kila siku. Usioneshe hasira zako waziwazi mbele yake pindi akikuudhi,na usiongelee jambo au kuandika msg ukiwa na hasira,mwanaume hapendi kukaripiwa,subiri hasira zishuke kwanza. Nakuombea ulivuke hili salama,Nami nimepitia kipindi kama hiki ila mwisho wa siku niligundua tatizo nikasolve.

Aaah kuzinguana, kuchuniana mambo ya kawaida sana wala sio cha kushangaa
 
NANDERA cha kusikitisha zaidi wanawake wanafanya haya yote na bado wanaachwa mwisho wa siku wanabaki kujiuliza wamekosea wapi. Cha muhimu is to be yourself.
 
Last edited by a moderator:
Hahha mpe tigo sasa...

On a serious note...huyo kakuchoka! Ingawa jibu zuri ungelipata kwake zaidi.
 
Ni Mambo Ya Kawaida Sawa, Ila Ww Unaona Umemaliza Kila Kitu Kiasi Kwamba Unasema Unamfanyia Kila Kitu Lakin Bado Haridhiki!! Mean Umemaliza Kila Linalostahil Yy Kufanyiwa Lakin Haridhiki!!!

And your point is?
 
Take it easy. Dont take marriage too serious. Utakufa kwa presha. Fanya unachoweza, usichoweza acha. Kumbuka wewe ni binadamu pia.
 
Sasa Eve wewe kama ni mtanzania wa kawaida unataka kuniambia mke kumnawisha mume ni ishu nayo?!! Acheni utani bana hayo mambo ya kawaida sana kwenye jamii za kitanzania labda kama mnaongelea jamii ya hapo kwa jaluo mtaa wa pili.

Wala Sina haja ya kukulazimisha
 
Unampa too much attention ndio maana haishi kulalama. Do your part with all your heart basi vingine mwachie yeye ahangaike navyo. Kuna watu wana gubu wewe na ukiendekeza atataka hadi umtafunie na kumlisha kila siku. Biandamu hatuko perfect na kama yeye anaona mapungufu au wewe ni jukumu lake kama mpenzio/mumeo/mkeo kukwambia darling hapa naona kuna kitu kinapelea from there you can talk ila mtu wa gubu mara hiki alalame mara hiki anune mhh huyo abebeki. Siku kausha tu maana ameshaona weakness yako ni kuogopa akilalamika . MAisha haya utaishi kwa kuguess kuwa sijui nifanye nini kipya asilalamike? utaweza? Mapenzi ni pamoja na uwazi na kuongea sio kumtegeshea mwenzio akosee ndio utoe malalamiko hayo hayatakuwa mapenzi bali utumwa.

Thanks, sio kuwa hata naogopa lawama but nashangaa tu....nimekupata
 
Sasa naanza kumuelewa housegirl
Hahhaa bora umuelewe tu, ili usije ukaingia na expectations kibao afu ukakuta hamna kitu. Ikitokea umejibahatishia mmoja kama gelofriend wangu, basi itakuwa zali la mentali
 
Last edited by a moderator:
Mbwa mzee kujifunza mbinu mpya hili nalo tatizo tena tatizo kubwa.

Huwa naona real men The Boss akiwa among wanasema mwanaume anahitaji mambo matatu: food, sex and space.

Katika hayo mambo kwakweli am doing the best inawezekana kabisa nina mapungufu yangu ila am doing the best kwakweli, food, napika japo sio bonge moja la mpishi kama farkhina but I cook tena delicious ones, sex hii si kuwa tu ni wajibu ila ni hobby yangu kitu ikiwa hobby kifuatacho itv ni known kabisa, space hapa kidogo pananishinda japo najitahidi ila sio kwa fungulia doggy, anaechungwa ni mbuzi kwa binadamu tunafanya kukaba tu japo kukaba kwenyewe ni kulinda bahari ila hivo hivo tu almradi kuna kibao "Punguza mwendo kazi inaendelea mbele" tunapunguziana speed natoa space kwa kiasi Chake may be majukumu yakinizidi itakua zaidi ya hapo.

Apart from hivo vitatu nafanya na mengineyo mengi napika mwenyewe simuachii dada wa kazi, mezani naweka mwenyewe kumake sure kila kitu kipo sawa, nguo nasaidiwa kufua ila boxa nafua mwenyewe, nanyoosha mwenyewe, asubuhi naanda maji ya moto napeleka bafuni (bafu halina heater) muda huo nshaweka nguo za kazini standby na viatu nimebrush kabisa mara chache naandaa Chai sio kila siku kwasababu ni mvivu kula BADILI TABIA bila shaka unanishangaa sana make haya mambo hautajagi ha ha ha nishangae tu ukinishangaa nami na kushangaa.

Swala la heshima na kujali nikijifanyia assessment najiona nina 99%,i do respect him much, much kwakweli nikijilinganisha na ndugu, jamaa na rafiki am the best, naweza kuwavisit katikati ya maongezi mara wachambane na waume zao mara wawafokee kitu ambacho mi huwa nashangaa unawezaje kumchamba mmeo au kumfokea mbele za watu mmh sijawahi na sitakaa nithubutu nikikereka nangoja tukiwa wawili nikiona nachelewa kutoa dukuduku naandika meseji.

Kuna shost angu alishawahi kunitembelea akaishia kunishangaa inakuaje nanyoosha nguo za baby dady yeye wanaishi wote ila hajawahi kumfulia wala kumnyooshea nikamshangaa pia na kuzidi kujiona am the best mie ni "mwanamke" hizi huduma nazionaga kwa wamana watu wazima ndo wanawalea waume zao ila mie kwa age yangu tu hii najiona nipo kama mama lowasa ha ha .

Point yangu what else should I do? Pamoja na kujiona mwanamke, najiona kama mama Lowassa ila bado nalalamikiwa jamani wanaume zaidi ya haya kunakuna yapi tena?au ni human nature tu kwamba hatunaga kuridhika? Au kunanii?

Unalalamikiwa kwa LIPI hasa? Be specific!
 
Evelyn Salt.Ongea na jamaa kitu ambacho huridhiki nacho mwambie tu usijiulize mara mbili mbili.
Nashukuru Mungu huwa siwezi kulala na kitu ambacho kimenikwaza yani😕 ntamuamsha hata usiku wa manane kumwambia ya moyoni.
Hongera dear unajitahidi kumjali mmeo,umenizidi la kubrashi viatu.
:thumbup::thumbup:
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma nikarudia nikasoma. Sasaaa... dah! ndoa naipenda lakini iko kama itanipita jameni. Una mtoto mdogo, unapata muda wa kupika (sasa sijui ni kila siku?) na chakula unapeleka mezani wewe, unamnawisha mume, mtoto nae anakungoja umlishe, umesema unapasi, unapeleka maji bafuni, unamuandalia nguo, viatu....

Nimetafakariii nikajiangalia ili mimi niweze kuwahi kazini kwa kujihudumia mwenyewe naamka saa 11. Nikihamia nje kidogo ya jiji kuamka itakuwa saa 10. Sasa nikianza kumhudumia na mtoto mkubwa hadi kusafisha viatu si ndio nitaamka saa 9? Kazi za mwajiri ufanye kama mtumwa, urudi home ukiwahi sana saa 12 uvae apron uingie jikoni....kuna viwatu vya kukaguliwa au kusaidiwa homework... sijui nini.... ukimaliza hapo useme ukaoge ujitupe kitandani mwenzio yeye ana nguvu zote wewe mgongo unalia kama vijiti vikavu..

Kama sitapata mume anayeweza kujitegemea kwa mambo na sina hela za kununua mashine za nyumbani (kama heater, mashine za kufulia, sinki la kunawia dining...) itabidi nichague kuwa hausiwaifu tu na sijui kama niko tayari maana nilishagundua siko kwenye kundi la superwomen.

Unajua ni rahisi sana kusema mume anahitaji kufanyiwa kama mtoto lakini mnasahau kuwa watoto wana rewards za kutia moyo. Kwanza unajua hajiwezi kwa hiyo unajiskia raha kumsaidia mtu asiyejiweza. Unaweka na bidii ili kumwelekeza aweze kujitegemea; ukimhudumia hana matusi wala dharau. Wakati mwingine hawaridhiki na unachowapa, wanweza kukulilia hadi ukatamani kuhama nyumba lakini unawavumilia kwa kuwa hawajui chochote kuhusu hela wala mipango. Wanatulilia tu kama sisi tunavyomlilia Mungu. Unaweza kumnunulia nguo ya laki halafu we moyoni unajiskia raha kweli ulivyogharamia gauni halafu unakuta amelivaa anachezea mchanga ila ukimnunulia pipi au chama anashukuru mpaka anakubusu!! Halafu mapenzi yao hayana masharti. Mnakosana, baada ya dk chache anakufata kujaribu kurudisha uhusiano. Vimbwanga vyote atakavyofanya unajua anafanya kwa sababu mtoto. Haya, mtu mzima analinganishwaje na mtoto? Na mtu mzima wa kike yeye ni mtu mzima tu toka utotoni hadi uzeeni?

Muda ninao may be nature ya kazi pia, namaliza mapema by saa sita nakua home kila siku....labda nikiwa bize zaidi ndio nitashindwa kutekeleza majukumu yangu
 
Back
Top Bottom