Zanzibar 2020 Namba 14: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar. Arejesha fomu hiyo

Zanzibar 2020 Namba 14: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha achukua fomu ya urais Zanzibar. Arejesha fomu hiyo

saidi kindole,

Jecha huyu huyu jecha wa jecha kiboko ya jecha muzee ya kupindua meza!
Duh nchi hii kuja kupata maendeleo itachukua miaka 1000.
Huyu ni "karma" tu inasubiri juu ya kesho yake. Kwa maana kwa imani ya dini yoyote ile maamuzi yake yaliikosea mbingu na dunia.
Mimi Jecha salim Jecha, huyu jamaa wazinzabar hawatomsahau kwa kufuta uchaguzi mkuu 2015.
Hahahaha, Jamani Twendeni na Jecha ZNZ 2020-2025

Siasa kweli mchezo mchafu, bila haya wala aibu kachukua fomu
 
Vuta tafakuri hawa wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi watatenda haki kweli? Kwani wote ni makada ukimjumlisha na yule alieteuliwa jana.
Katiba ya zanzibar inaeleza kabisa kutaka wajumbe kutoka ccm 6,na cuf 6,sijui wajumbe wa mwaka huu itakuaje kwa sababu wale wa cuf walijiuzulu,itabidi wateuliwe wengine toka cuf!!
 
Kazi kweli kweli.

Dunia ipo kama Farasi inayokokotwa na mkokoteni.
Yani mkokoteni uko mbele ya Farasi unaikokota.

Wanaofanya mambo ya hatari na ya kihuni kwa umma ndio wanaopeta na kujiona wajanja.
 
Bila kuwa na kadi ya ccm huwezi teuliwa kuwa mkurugenzi Wa tume ya uchaguzi kamwe.
 
Hivi kumbe wenyeviti wa tume za uchaguzi ni ccm halafu wapinzani wanakubali kushiriki uchaguzi?
Mkuu ndo unajua Leo? Wakurugenzi wote Wa halmashauri ndo wasimamizi Wa uchaguzi na Ni makada Wa ccm 100% na mteuaji Ni mwenyekiti Wa ccm.
 
#Habari:Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Bw.Jecha Salum Jecha amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar katika ofisi za CCM Kisiwandui. https://t.co/ebliz6cy7B
IMG_20200621_085527.jpg
 
Alijiunga na Ccm baada ya kustaafu
Huyu alikuwa CCM kabala , na alishawahi kugombea Ubunge huko nyuma katika jimbo fulani hapa Unguja.akashindwa kwenye kura zamaoni.
Kisha akateuliwa kuwa mwenyekiti wa Tume akiwa CCM kada mbobezi na lisikika akitamka hadharani kuwa Mpinzani akishinda Uraisi katu hato mtangaaza.

Tanzaniania Inachekesha sana.
 
Dwa yao iko tayari
Hsira za wengi zinalazimisha Laana
CCM itakumbana na laana, na Minyukano ya wenyewe kwa wenyewee
hadi kufa.
 
Back
Top Bottom