Uchaguzi 2020 Namba 3: Lazaro Nyalandu achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, asema watahakikisha mechi wanaipeleka sawasawa

Uchaguzi 2020 Namba 3: Lazaro Nyalandu achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, asema watahakikisha mechi wanaipeleka sawasawa

Maneno ya hekima sana. Haya mambo ya kishetani, ya kuwaweka watu ndani hovyo, kwa vile tu huwataki. Watu wanasingiziwa uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, halafu mwishoni mashtaka yote yanayeyuka, lazima yakome. Hakuna anayestahili kuonewa, bila ya kujali kama mtu huyo ni CHADEMA, CCM, CUF, ACT, n.k.

Haya mambo ya mtu kumkosoa tu Rais au Serikali halafu anatekwa na wasiojulikana, wakati mwingine hadi kuuliwa na wasiojulikana, ni ujuha na kazi ya shetani, lazima yakome. Wote kwa umoja wetu tukisema tunataka yasiwepo Tanzania, yatatoweka.

Tujenge Taifa la watu wastaraarabu, Taifa la watu wanaothamini utu na uhai wa binadamu, bila ya kujali mtu huyo unampenda

Tuondoke kwenye primitivity. Haya mambo ya kuvizia watu, kuwafunga, kuwapoteza, uwendawazimu wa hali ya juu, na yameutia dosari kubwa uongozi wa awamu ya 5. Na jambo hilo litabakia kwenye kumbukumbu ya vizazi vingi vijazo kama kumbukumbu chafu iliyowahi kuliharibu Taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom