namba ya NIDA kutumika kusajili line nyingi bila muhusika kujua kinachoendelea.

namba ya NIDA kutumika kusajili line nyingi bila muhusika kujua kinachoendelea.

bonyeza *106# fata maelekezo chagua 3 then weka namba ya NIDA utaziona namba zite zinazotumia NIDA yako.
Ahsante sana nimeona.

Lakino kuna namba moja ya halotel niliisajiri kwa nida yangu ila sijaitumia muda mrefu kama zaidi ya miezi minne ivii na ishapotea, siioni kwenye orodha ya namba zilizotumia nida yangu.
 
Hapa nimeangalia tena, nakuta airtel namba 2 ambazo sizijui.

Na mie sijawahi tumia mtando wa airtel
Tena Airtel ndo kiboko Kwa kutumia vitambulisho vya watu. Sielewi Wana shida gani
 
Hazifutiki aisee

Me nilishakuta namba ambazo sizijui.. nikajaribu kufuta kwa namna ile iliyokuwa inasemekana zamani. Hazifutiki

Mpaka wakala, na wakala namba 1 anakufutia na buku
Yeah, mi mwenyewe pesa ilinitoka
 
Ahsante sana nimeona.

Lakino kuna namba moja ya halotel niliisajiri kwa nida yangu ila sijaitumia muda mrefu kama zaidi ya miezi minne ivii na ishapotea, siioni kwenye orodha ya namba zilizotumia nida yangu.
Huwa wanaiondoa wenyewe,,, mi mwenyewe Kuna namba ya Airtel sijatumia muda mrefuuu. Wameiondoa kwenye orodha na wamenifumgia huduma
 
Mkuu usiwe mjinga kiasi hicho kuna kipindi kwenye application ya usajili ya VODA ilikuwa imewekewa udhaifu uliowawezesha vijana wa kusajili kuhifadhi fingerprint yako hata kwa zaidi ya siku 7 sijui kama wamesishairekebisha kiufupi kampuni hasa vodacom wanaweka mazingira wezeshi kwa mafreelensa kufanya udanganyifu
Wanatakiwa washitakiwe ni kona kubwa sana kuhifadhi fingerprint ya mtu bila consent ya serikali
 
Acha ujinga wewe kilaza. Hakuna namna ya kutunza fingerprint kwenye ule mfumo. Unatumia fingerprint ku-retrieve data kutoka NIDA kama one time request. Lazima kidole kiwe kwenye mashine kwa muda fulani mpaka data zije. Usipende kuongelea usiyoyajua.
Wanatunza kwenye mfumo wao locally boss kabla hawajasubmit NIDA
 
Wale mnaosajili barabarani lazima iwe hivyo,maana wale wanawasajilia watu ili wapate hela,chamsingi pita ofisi ya kampuni husika thibitisha namba unazotumia
 
Hapa nimeangalia tena, nakuta airtel namba 2 ambazo sizijui.

Na mie sijawahi tumia mtando wa airtel

Hivi akifanya mauwaji au unyang’anyi wa silaha au au au
Mpaka kujinasua si itakula hela nyingi sana
Mungu atusaidie kwa kweli maana serikali huwa inakurupuka bila kufanya ABC kwanza la zoezi

Nakushauri ukafungue faili kuwa sio wewe na ukazifute haraka
 
Ujinga wa makampuni ya simu ama kasoro/masharti ya TCRA ni kuwa huwezi kufuta uajili kwa namba usiyoitambua hadi uende kwenye maduka ya mtoa huduma. Fikiria mkoa kama kigoma ukute kuna voda/tigo/halo/airtel shop moja kwa mkoa mzima, mtu asafiri kilomita 40 au zaidi ili kwemda kufuta usajili wa laini ya buku? Halafu walivyo na mbwembwe, ukipiga *106# kuna sehemu ya "futa usajili" wankera sana
 
Back
Top Bottom