Namba yako ya simu unayotumia sasa ulianza kuitumia mwaka gani?

Mimi nilianza kuitumia mwaka 2008 enzi hizo unasajili bila NIDA na ndiyo laini yangu kuu mpaka leo yaani takribani miaka 16 sasa!

Ya kwako umeanza kuitumia mwaka gani?
Unakaa na laini miaka yote io ili iweje aseeee jifunze kubadilika kupata watu wapya na kuachana na wengine wasio na maana.
 
Mimi nilianza kuitumia mwaka 2008 enzi hizo unasajili bila NIDA na ndiyo laini yangu kuu mpaka leo yaani takribani miaka 16 sasa!

Ya kwako umeanza kuitumia mwaka gani?
Kila Mwaka nabadilishiwa namba
 
Tritel ilikuwa na cc640 nc01 ndio mtandao wa kwanza kusajiliwa hapa tz, mobitel ulikuwa wa pil kusajiliwa ukapata namba cc640 nc02, nc03 nafikir ni zantel, 04 vodacom 05 ni celtel baada ya hapo vurugu ikazidi akina sasatel walikuja wakapotea, sasatel alianza na masafa ya 3G pekee yaani hata kiswaswadu kiwe cha 3G, alikuja na tech kubwa kabla ya muda, yakamshinda
 
2019 nikiwa form six. Nilikuwa mkaidi naenda shule na Huawei mbovu hata wangeiba isingeniuma sana. Ikakamatwa nikaikana sio yangu.
Nikakaa kidogo bila simu ghafla tukapata tour ya kwenda shule ya wasichana nikawahi mjini kununua kisimu kidogo na kusajili laini na kuikariri namba hapohapo ili kesho yake nichukue namba za warembo.
 
Mnafukua makabuli ya enzi na enzi😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…