Namba yako ya simu unayotumia sasa ulianza kuitumia mwaka gani?

Namba yako ya simu unayotumia sasa ulianza kuitumia mwaka gani?

Tritel ilikuwa na cc640 nc01 ndio mtandao wa kwanza kusajiliwa hapa tz, mobitel ulikuwa wa pil kusajiliwa ukapata namba cc640 nc02, nc03 nafikir ni zantel, 04 vodacom 05 ni celtel baada ya hapo vurugu ikazidi akina sasatel walikuja wakapotea, sasatel alianza na masafa ya 3G pekee yaani hata kiswaswadu kiwe cha 3G, alikuja na tech kubwa kabla ya muda, yakamshinda
Hapo tritel enzi hizo wanachuana na mobitel ambayo ndo tigo sasa, walikuwa na tangazo lao la njiwa anaruka alafu jogoo linabaki linademadema ikatafsiriwa kama dongo Kwa mobitel kwamba tritel ni njiwa alafu mobitel ni jogoo haliwezi kuruka enzi hizo mobitel alikuwa analogy huku tritel alikuwa digital
 
Ukitaka kujua laine umeanza kutumia lini unaingiza code gani maana wengine tusahau hata tarehe na mwaka
 
Tuandamane ili watulipe tushawaingizia pesa nyingi 😂😂
Kweli aisee, mimi voda wamenila sana hela zangu, kwa mara ya kwanza voda nimeitumia 2007 .
Mpesa kuweka na kutoa na kutuma heka,muda wa maongezi kupiga sim sms dana na kutuma salio kwangu haipungui milioni 70 mpaka 50 kama faida kutoka kwangu, ndio maana hawaachagi kunitakia siku njema ya kuzaliwa kila mwaka.
 
Back
Top Bottom