Namba yako ya simu unayotumia sasa ulianza kuitumia mwaka gani?

Hapo tritel enzi hizo wanachuana na mobitel ambayo ndo tigo sasa, walikuwa na tangazo lao la njiwa anaruka alafu jogoo linabaki linademadema ikatafsiriwa kama dongo Kwa mobitel kwamba tritel ni njiwa alafu mobitel ni jogoo haliwezi kuruka enzi hizo mobitel alikuwa analogy huku tritel alikuwa digital
 
Ukitaka kujua laine umeanza kutumia lini unaingiza code gani maana wengine tusahau hata tarehe na mwaka
 
Tuandamane ili watulipe tushawaingizia pesa nyingi 😂😂
Kweli aisee, mimi voda wamenila sana hela zangu, kwa mara ya kwanza voda nimeitumia 2007 .
Mpesa kuweka na kutoa na kutuma heka,muda wa maongezi kupiga sim sms dana na kutuma salio kwangu haipungui milioni 70 mpaka 50 kama faida kutoka kwangu, ndio maana hawaachagi kunitakia siku njema ya kuzaliwa kila mwaka.
 
2015 na ni Mdakuzi alinipa huo ushauri baada ya mtandao niliokuwa nikiutumia awali kusumbua sana upande wa Internet.
Lol! Huo mtandao unaotumia kwa sasa, ulipaswa unilipe kwa kuwafanyia marketing.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…