Namfananisha Tundu Lissu na Mwanasiasa wa Venezuela, Juan Guaido

Namfananisha Tundu Lissu na Mwanasiasa wa Venezuela, Juan Guaido

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,171
Reaction score
23,996
Baada ya Uchaguzi Mkuu kupita, nayaona yaliyojitokeza venezuela yakitokea kwa Mwanasiasa Tundu Lissu.

Namfanisha Tundu Lissu na mwanasiasa wa Venezuela, Juan Guaido ambaye alitumiwa sana na wanasiasa wa Marekani ili kumuondoa Rais Nicolas Maduro wakitegemea ana uwezo na nguvu za kisiasa kwa wananchi wengi lakini baadaye ikagundulika hana uwezo au nguvu hizo. Wanasiasa wa Marekani walimtambua kama ndiye Rais mtarajiwa wa Venezuela lakini baada ya kugundua hana uwezo na nguvu za kisiasa wakaachana naye. Wabunge wa kambi yake ya upinzani pia wakamuondoa kwenye kiti cha Rais wa bunge la Venezuela!

Wamarekani kwa sasa wanasema wanaandaa/kutayarisha mtu mwingine baada ua utawala mpya wa Joseph Biden au watakaa na serikali ya Maduro ili kufanya maongezi ya kisiasa.

Tundu Lissu naye ataachwa kimya kimya kama ilivyotokea kwa Juan Guaido kwa sababu wafanyabiashara wa kisiasa wa kimataifa hawana urafiki wa kudumu bali wana maslahi/manufaa ya kudumu.

Kushindwa kwa Tundu Lissu kuingia Ikulu au kufanikisha maandamano nchini ilikuwa ni ishara tosha kuwa hana ushawishi mkubwa na kwa msingi huo hawezi kubadilisha sura ya kisiasa nchini. Kutobadilisha sura ya kisiasa nchini ni gharama ambayo wafanyabiashara za kisiasa wa kimataifa hawawezi kuendelea kuibeba kwa muda mrefu.

Wafanyabiashara hawa wa kisiasa kwa sasa watakachofanya wataanza tena kujipendekeza kwenye serikali ya Rais Magufuli ili wapate fursa za kibiashara kwa gharama ambayo angalau ni kidogo ukilinganisha na gharama za Tundu Lissu kama ''lame duck'' politician!

Kuna dhana inajengwa eti kuwa Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi. Hakuna cha vikwavyo vya kiuchumi bali kilichoko ni ‘’competing economic interest and benefit’’ kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kimataifa hasa Marekani na Kanada. Kelele za baadhi ya wanasiasa wa Marekani ni baada ya Symbion Power Tanzania Ltd (SPTL) kupigwa ‘’kufuli’’ na serikali. Serikali ilikuwa inalipa zaidi ya Tsh bilioni 700 kwa mwaka kwa haya makampuni (Symbion, IPTL na Aggreko).

Tanzania kama nchi ingewekewa vikwazo vya kiuchumi kama tungekuwa tumewafukuza wawekezaji wa nje kama alivyofanya Rais Robert Mugabe. Yaani utawekewaje vikwazo wakati makampuni makubwa ya kimataifa ya uwindaji, gesi na madini bado yanaendelea kuvuna faida nchini huku yakisafirisha madini kwenye masoko ya nchi zinazodaiwa zitaweka vikwazo.

Hata ‘’Targeted individual sanctions’’ kwa wanasiasa wa Tanzania ni kupoteza muda tu kwa sababu wanasiasa wenyewe hata kusafiri nje ya nchi hawasafiri na pia hawana hata ‘’big asset’’ kwenye nchi inayosemekana itaweka vikwazo! Ndiyo yaleyale ya Makonda kuwekewa vikwazo huku akiendelea kudunda mitaani

Kama huzijui siasa za kidunia utaendelea kucheza mapambio ya wanasiasa ambao kwa sasa ni ''lame duck'' mpaka 2025!
 
Huyo Mazuri wa Venezuela ni dikteta na aliyejaribu maisha ya watu wake.

Mpinzani wake anataka kuitoa nchi kwenye mkwamo wa kiuchumi na kisiasa,

Unataka kutuambia JPM ni dikteta kama Maduro aliyekuja kuiharibu nchi yetu?
 
Huyo Mazuri wa Venezuela ni dikteta na mpumbavu aliyejaribu maisha ya watu wake.

Mpinzani wake anataka kuitoa nchi kwenye mkwamo wa kiuchumi na kisiasa

Unataka kutuambia JPM ni dikteta kama Maduro aliyekuja kuiharibu nchi yetu?
Mkuu;

Nani alikudanganya Maduro ni dikteta?

Maoni yako yanaonyesha huzijui siasa za Venezuela!
 
Lissu kalabata Ubelgiji alafu ghafla karudi anataka Urais.

Kashindwa uchaguzi vibaya, kwa aibu kubwa sasa anataka kusepa kwa kupitia mlango wa kutishiwa maisha.

Lissu akuna wakumtishia maisha, yeye asepa kiroho safi tu, nchi yetu ahiitaji vibaraka kama yeye.

Kazunguka nchi nzima bara na visiwani akuchomwa hata mwiba asitafute visingizio.
 
Huyo Mazuri wa Venezuela ni dikteta na mpumbavu aliyejaribu maisha ya watu wake.

Mpinzani wake anataka kuitoa nchi kwenye mkwamo wa kiuchumi na kisiasa,

Unataka kutuambia JPM ni dikteta kama Maduro aliyekuja kuiharibu nchi yetu?
Ndicho anachomaanisha huyo mjinga, anajifunga kwa maneno yake mwenyewe.
 
Lissu kalabata Ubelgiji alafu ghafla karudi anataka Urais.

Kashindwa uchaguzi vibaya, kwa aibu kubwa sasa anataka kusepa kwa kupitia mlango wa kutishiwa maisha.

Lissu akuna wakumtishia maisha, yeye asepa kiroho safi tu, nchi yetu ahiitaji vibaraka kama yeye.

Kazunguka nchi nzima bara na visiwani akichomwa hata mwiba asitafute visingizio.
Nakumbuka aliulizwa swali kama atakuwa mstari wa mbele kwenye maandamano akasema ndio.

Kesho yake akakimbilia kwenye viunga vya ofisi za balozi za nchi za Ulaya!
 
Ni kushukuru tu kuwa Russia na China ndizo zilizookoa jahazi vinginevyo Maduro angeondolewa madarakani.

Lakini hali ya uchumi ya Venezuela ikoje baada ya kuwekewa vikwazo vya uchumi na Marekani? Fuatilia vizuri.

Na huku tuzidi kumwomba Mungu mabeberu wasituwekee vikwazo! Mabeberu huwa hawashindwi.
 
Mimi namfananisha jiwe na dictator Mussolin, yeye alitumia Hadaa kwa viongozi wa RC huko Italy kujipatia nguvu kubwa ya kiutawala. Lakini dakika ya mwisho aligeuka kuwa mauaji mkubwa na dictator mashuhuri. Hayo kwa sasa tunayaona hapa nchini.
 
Back
Top Bottom