Namlaumu Rais wa awamu ya kwanza

Namlaumu Rais wa awamu ya kwanza

Unatupiga Kamba tu, wasinufaike Watoto wa kuwazaa mwenyewe ndio anufaishe ndugu za mama yako?

Hukuwahi kumjuwa Nyerere, kwake hakukuwa na deal la kupiga naye wala kutowa upendeleo maalum never.
Na huo ndio ukweli mchungu !!
 
Wakoloni walituletea maendeleo sema tu wivu na tamaa ya wapigania UHURU ndio waliwadanganya waafrika kwamba watawaletea maendeleo baada ya UHURU wakajiletea maendeleo yao na ya familia zao ndio zinazolamba asali.
Walikuja kubadilika baadaye sio wale walioudai Uhuru !!
 
Waliondoka baada ya uhuru
Na wakaahidiwa watakaribishwa tena waione Tanganyika baada ya miaka kumi jinsi itakavyokua ili walinganishe na walivyokuwepo wao kama wakoloni watawala ! Na Alitimiza hiyo ahadi !
 
Nyerere ana mapungufu ila atleast alivyoona ameshindwa alisema jqmani ngoja nipumzike. Akapumzika akatuachia nchi yetu tuamue wenyewe.
 
Tatizo ni watu na sio katiba. Hii hii iliyopo huwa haifuatwi kikamilifu na hakuna chochote kinatokea, Sasa hapo unamlaumu vipi Nyerere?
 
Kusini na Pwani ni masikini kwa sababu ya laana ya matambiko. Ukijua chimbuko la uchawi wa Mwenge utaelewa kwann kusini ni masikini.
Pamoja na hayo ila kuna changamoto kwenye utamaduni wao. Something more than uchawi na matambiko. They need to liberalize themselves first.
 
Nyerere hawezi kukwepa lawama. Maana alijua kabisa hii ni mbovu na haifai. Ila aliacha tu iendelee kutumika wakati alikuwa na uwezo wa kushawishi ibadilishwe. Chanzo cha shida zetu ni ccm. Wao ccm wanazidumisha na kuziendeleza
Hii hii mbovu inafuatwa kikamilifu?
 
Sera zake zilikuwa nzuri sema utekelezaji, hapakuwa na wasomi wa kutosha na waliokuwepo waligeuka kuwa wapiga madili, angalia mashirika ya umma yalivyokufa kifo cha mende. SU ilimaanisha "soma ule"
 
Habari,
Kwangu mwalimu Nyerere namlaumu na nitaendelea kumlaumu kabisa yeye ndio chanzo cha haya yote yanayotea hapa Tanzania.

Ilikuwaje kama yeye Rais baada ya uhuru asingeibadilisha katiba? Na bado akaendelea kutumia katiba ile ile? Hapa nahisi huyu Rais ni wa mchongo kwa maana aliwekwa na wakoloni ili kutukandamiza sisi na vizazi vyetu.

Sera ya ujamaa na Arusha Declaration, hapa Nyerere alibugi balaa sanaa nahisi ndiyo chanzo cha sie Tanzania kuwa masikini kutakana na Sera zake za hovyo kupitiliza. Hii imesababisha hata Watanzania wengi akili zao haziko sawa na wanapenda kufair fair na kupenda mteremko kupita maelezo dadeki.
Chanzo cha mikoa ya Kusini kupoteza mwelekeo hili nitamlaumu hasa na nitendelea kumlaumu mpaka basi hovyo kabisa.

Mdini na udini wa Nyerere, kwangu Nyerere ni mdini sana na chanzo cha kuisunisha maendeleo ya waislamu na hii ilipelekea kuharibika mikoa ya kusini kiuchumi.

Mods msifute hii thread kwa sababu kuna post humu za kumnanga Magufuli na bado mnazipa airtime hii post muiache.
Sifa za kijinga, anahutubia lisaa na nusu hana hata kipande cha karatasi mkononi, akaonekana ana akili nyingi, kumbe ni upuuzi wa hali ya juu leo utagundua kumbe alikuwa anatuzamisha kwenye bwawa la ujinga/umasikini, na vicheko vyake vya kulazimisha, matokeo yake ndo haya.. Elimu hakuna na hata wale waliosoma wengi wao wajinga.... angalia mataifa makubwa raisi hotuba zote zimetayarishwa na wataalamu husika, hadi vizazi wanazikuta... katunyima elimu ili atutawale matokeo yake kajikuta anatawala "MAFISI" uoga kujipendekeza, unafiki + Umajaliwa vs Precision air...
 
Elimu, elimu, elimu.

Katiba tuliyonayo ni ya mwaka 1977 na waandishi wake wapo Mwenyekiti alikuwa Pius Msekwa na Tanzania ilikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja.

Wewe ndio mdini badala ya kumlaumu Alhaji Ally Hassani Mwinyi kwa kurudisha mfumo wa vyama vingi bila kuandika katiba mpya.

Unawadharirisha waislamu wenzako kwa kuwa na akili ndogo kiasi hiki.
We ni mpuuzi sana kenge maji we
 
Rais WA kwanza alikua anaakili na upeo WA ajabu sana na ni raisi pekee alokua na Ushawishi mkubwa.
Ila sasa alikua mnafiki sana hasa aliotumia zungimzia udini kuukemea hii ilkua kama trick Kali sana.

Kwani hata kifo Cha Karume alikataa uwepo WA uchunguzi WA kifo.

Hii yote ni kutumikia wakoloni.

Anamazur mengi ila mabaya akija yaskia hutampenda hata kidogo
Kabisa
 
Unamlaumu baba kwa kuwa hakuwajengea nyumba
Leo una miaka 60 bado unalaumu si ujenge sasa

Mbona kila anaengia madarakani anakuwa na nguvu zile zile za ukandamizaji?

Bunge lipo ingawa lina uwezo wa kusema sasa basi
Ila mnatishiwa kwa kuwaleta wajeda wafagie barabara halafu mnasahau tena miaka 10

Hiyo miaka 10 itakuja na kwenda na hamtafanya lolote
Wanaoficha hela zao wazitoe zifanye kazi zizae na wapatikane hata millionaires 100 tu waswahili ndio mtajua naongelea nini hapa

La sivyo acheni mafala yaibe yahonge na yaendelee kutawaliwa yakifikiri kuendesha V8 na nyumba nzuri na watoto kwenda FEZA ndio yamefika

Ila wakumbuke potholes zitakuwepo miaka mingine 100 na malaria itawapata na kuuwa watoto wao pia
Wote ni wale wale
 
Kale ka babu kametuyumbisha sana kwenye uchumi, elimu na siasa hasa ikichagizwa na ujamaa wake. Kwangu he is no hero, japo upande wa mama yangu ni watu wa Mara na kwa kiasi fulani walinufaika kifursa wakati wa utawala wake.
Watu wa kusini wanamlalamikia sana
 
Sifa za kijinga, anahutubia lisaa na nusu hana hata kipande cha karatasi mkononi, akaonekana ana akili nyingi, kumbe ni upuuzi wa hali ya juu leo utagundua kumbe alikuwa anatuzamisha kwenye bwawa la ujinga/umasikini, na vicheko vyake vya kulazimisha, matokeo yake ndo haya.. Elimu hakuna na hata wale waliosoma wengi wao wajinga.... angalia mataifa makubwa raisi hotuba zote zimetayarishwa na wataalamu husika, hadi vizazi wanazikuta... katunyima elimu ili atutawale matokeo yake kajikuta anatawala "MAFISI" uoga kujipendekeza, unafiki + Umajaliwa vs Precision air...
Kabisa
 
Back
Top Bottom