Namlaumu Rais wa awamu ya kwanza

huyo mzee alikua ovyo sana, sitaki hata kumsikia. Yeye ndio alietufikisha hapa tulipo. hii mizizi mizito ya CCM na matawi yake Policcm, JWTZCCM, na Tissccm yeye ndio mfalme wao.
 
Nyerere hawezi kukwepa lawama. Maana alijua kabisa hii ni mbovu na haifai. Ila aliacha tu iendelee kutumika wakati alikuwa na uwezo wa kushawishi ibadilishwe. Chanzo cha shida zetu ni ccm. Wao ccm wanazidumisha na kuziendeleza
Ndio maana mchangiaji mmoja ameuliza ikiwa Baba yetu hakutujengea nyumba na sasa sisi wanawe tumeshafikia umri wa miaka 60 bado tunasubiri aje atujengee ?!
 
huyo mzee alikua ovyo sana, sitaki hata kumsikia. Yeye ndio alietufikisha hapa tulipo. hii mizizo mizito ya CCM na matawi yake Policcm, JWTZCCM, na Tissccm yeye ndio mfalme wao.
Swali, tutatokaje hapa?. Au tumekubali kwamba akili zetu zimedumaa. Nyerere ana hotuba nyingi sana ambazo zimechapishwa. Ukigooogle utazipata kama huna muda wa kwenda maktaba. Isitoshe, alituasa kwamba mazuri yake tuyaendeleze/tuyaboreshe kama taifa lakini mabovu tuachane nayo. Kama tunafanya hivyo tujipongeze.
 
Kijana inabidi ufe, na uzaliwe 1950, ili uelewe mambo ya nyakati.
Maana ninyi kizazi ya miaka ya Mkapa na Kikwete hamuelewi mengi.
Ufe, uzaliwe miaka ya nyuma.
 
Rubish! King hassan Wa pili wa Morocco mbona alifanya ya maana? J.j rawlings je?
 
Kumba huyu mtoa mada lumumbashi anamlaumu mzee wa watu pasimo kujua kama anachomlaumu nacho mzee wa watu ni sahihi.
 
Hii thread ya kiwango cha chini kabisa. Unamlaumu Nyerere kwa kitu gani wakati katika miaka 61 ya uhuhu kakaa miaka 25 tu.

Na kabla hajastaafu alikwisha waambia kuwa ile Katiba ni mbovu, kwa nini Marais 5 waliokuja hawajabadili?
 

hatuhitaji nasaha zake kwenye kujikomboa. alikua ni mnafiki sana, wakai huo aliokua akitoa hutuba kama hizo behind scene alikua akiendelea kutenda mabaya mengine.
1995 CCM walishararuliwa vibaya sana kwenye uchguzi mkuu kule zanzibar, ni yeye aliesamamia mpaka matokeo yakapinduliwa.
 
Hii thread ya kiwango cha chini kabisa. Unamlaumu Nyerere kwa kitu gani wakati katika miaka 61 ya uhuhu kakaa miaka 25 tu.

Na kabla hajastaafu alikwisha waambia kuwa ile Katiba ni mbovu, kwa nini Marais 5 waliokuja hawajabadili?
Miaka 25 kwahiyo ni michache? Mandela amekaa almost miaka michache but angalia South Africa
 
Nitamkosoa Nyerere overall period of my life
 
Kuendelea kulaumu haitasidia kitu. Badala yake lawama zitaendelea kusababisha uchungu mioyoni mwetu na kutudumaza akili. Jambo la msingi ni kuangalia wapi tulipoangukia au walipoangukia waliotutangulia,ili tusimame na kuchukua hatua madhubuti za kuzuia tusianguke tena.
 
Miaka 25 kwahiyo ni michache? Mandela amekaa almost miaka michache but angalia South Africa
Duh sijui uwezo wako wa kufikiri ukoje. Pengine unaelekeza lawama zako kwa wrong people. Unaweza Kuta wa kuwalaumu ni wazazi wako kwa DNA dhaifu au kwa kutokupa shule nzuri.

Mfano wa Mandela kukaa miaka 25 jela ni irrelevant na Nyerere kuwa Rais kwa same number of years
 
Huyu ni wa kupuuza tu. Tunapoteza muda kubishana na mtu asiyejitambua.

Kuna uzi mwingine kaanzisha huko anajifanya yeye ni mwajiriwa wa Usalama wa Taifa. Wanaomkosoa wote anawaporomoshea mvua ya matusi.
 
Kwenye suala la Katiba sijawahi kumuelewa Mwalimu. Aliinanga na kuikumbatia!
 
Ulivyomalizia nimecheka sana, kwamba nani vs nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…