Habari za saa wanachama wote.
Siku ya leo ningependa kufahamishana nanyi moja ya jambo ambalo serikali ya China katika miaka ya 1970s ilifanya ili taifa lao liweze kupata maendeleo ya kasi.
Katika miaka ya 1970s baada ya serikali ya China kuweza kurejesha ushirikiano mkubwa na mataifa ya magharibi ndipo serikali yao ilipo chukua jukumu la kuanza kupeleka wanafunzi wake bora katika mataifa ya magharibi kwa ajili ya kuweza kupata ujuzi na elimu bora katika vyuo bora vya magharibi.
Mwaka 1979 aliekuwa Rais wa China kwa wakati huo Deng Xiaoping alimpigia simu Rais wa U.S.A kwa wakati huo Jimmy Carter ili kumuomba nafasi ya vijana 5,000 wakichina kwenda kusoma U.S.A, naye Rais wa U.S.A akampatia nafasi kubwa zaidi ya vijana 100,000 wakichina kusoma U.S.A
Lengo kuu la serikali ya China kwa wakati huo ilikuwa ni kuweza kupata elimu bora sehemu mbalimbali duniani ili kuweza kulisaidia taifa lao kukua kwa kasi kutokana na kuwa nyuma na uduni mkubwa wa maendeleo walio kuwa nao kwa wakati huo.
Njia pekee walio kuwa nayo ni kupeleka wanafunzi wao bora katika mataifa yenye elimu bora na maendeleo bora kuliko wao kwa wakati huo, hii inasaidia wao kama taifa kuwa na mtaji mkubwa wa wasomi watakao rejea nchini na kuweza kutoa ile elimu bora waliopata ng'ambo na kuwa nufaisha wachina walio ndani ya nchi yao jambo linalo saidia wao kwa pamoja kupata ukuaji wa maendeleo ya kasi katika ngazi zote.
China inafanya hii mbinu hadi sasa na kwa asilimia kubwa imeleta matunda makubwa katika nchi yao kama walivyo tarajia.
Hii ni nukuu ya Rais Deng Xiaoping kuhusu hili suala.
" When our thousands of Chinese students abroad return home, you will see how China will transform itself ".View attachment 2520467View attachment 2520468
Swali:
Je Tanzania tuna yapi ya kujifunza juu ya hili jambo walilo fanya China ?
Hiyo pekee haikuisaidia China kupata maendeleo ya haraka. Ndiyo maana miaka ya 1990, ikaamua kuja na mbinu mpya, ya kubadilisha sera zake za uchumi, na kufanya ushawishi mkubwa kwa makampuni makubwa ya America na Ulaya kwenda kuwekeza nchini China.
Uwekezaji wa mataifa ya Magharibi nchini China ulibadilisha kila kitu, na kuupandisha ukuuaji wa uchumi wa China mpaka kufikia 12%. Mpaka leo, China ndiyo inayoongoza Duniani katika kuvutia wawekezaji wa nje ya nchi yao. Uwekezaji wa mataifa ya nje nchini China, kwa mwaka ni zaidi ya dola billion 80 (linganisha na uwekezaji wa dola bilioni 3 kwa mwaka, wa juu kabisa ambao Tanzania imewahi kuupata).
Makampuni ya nje yanafurahia uwekezaji wake nchini China kutokana na sera madhubuti zisizobadilikabadilika za kulinda uwekezaji.
Mpaka sasa, nchini China kuna makampuni zaidi ya milioni moja kutoka mataifa ya kigeni.
By the end of 2020, a total of 1,040,480 foreign companies were registered in Mainland China, the Official data was provided by the Ministry of Commerce (MOFCOM).2 Nov 2021.
Kwa hiyo kilichowasaidia sana China kubadilika kwa haraka, ni uwekezaji mkubwa wa makampuni ya nje. Mpaka leo, viongozi wa China, wakati wote wapo mataifa ya kigeni kutafuta wawekezaji wa kwenda kuwekeza nchini China.
Nchini China, ukihujumu uwekezaji, adhabu yako ni kifo. Mwekezaji nchini China analindwa kwa nguvu zote. Na bila hiyo China ingekuwa na shida kubwa ya unemployment.
Hapa kwetu, mkurugenzi wa kiwanda cha kusindika tumbaku pale Morogoro, RCO, kwa sababu za kijinga kabisa, alimweka ndani kwa masaa 8. Alipotoka tu, akaanza utaratibu wa kufunga kiwanda. Ndipo Rais Magufuli akaanza kuhangaika na kumtuma waziri kwenda kumbembeleza asifunge kiwanda, na akamtimua RCO wa mkoa wa Morogoro. Lakini hata hivyo, pamoja kutofunga, alipunguza sana uwekezaji wake, kiasi cha kuifanya tumbuka zaidi ya 50% mwaka ule ikose mnunuzi.
Wawekezaji ni wachache, Dunua nzima wanatafutwa. Ni yule mwenye mazingira mazuri ndiye anayewavuta wengi.