Namna elimu ya 'Balagha' inavyoingiza watu wengi kwenye Uislam

Namna elimu ya 'Balagha' inavyoingiza watu wengi kwenye Uislam

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,846
Balagha ni elimu ya maneno au Hotuba inayoathiri, na kumsogeza mtu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Ili kuielewa vyema, hebu turudi nyuma na tuangalie jinsi tunavyowasiliana,

Tuna mawazo au hisia ndani yetu, tunaita ''Maana katika nafsi''
Ili kueleza mawazo au hisia hizo, tunatumia lugha, Kwa hivyo lugha ni njia ya mawasiliano kwa kukieleza kile kilichopo kwenye nafsi.

Mchakato huu wote unajulikana kama ''Albayana' , yaani, uwezo wa kueleza maana katika lugha.

Tunaweza kuwa na msukosuko ndani yetu wenyewe lakini kueleza hisia hiyo tunaweza kusema, "Nina furaha" au "Nina Huzuni" nk.

Kutokana na hili, tunathibitisha kwamba lugha ni dhaifu kuliko maana ya kitu kilichopo kwenye nafsi. Lakini ikiwa tunaweza kuifanya lugha kuwa na nguvu zaidi kubeba zaidi ya maana ya kitu kilichopo kwenye nafsi.

Hapo ndipo utafiti wa elimu ya Balagha unapofaa. Tunajaribu kuifanya lugha kuwa na ufanisi zaidi katika kuwasilisha maana ya kitu kilichopo kwenye nafsi.

Kihistoria, Elimu ya Balagha ilianza kufundishwa katika Majazi ya kitabu cha QUR'AN إعجاز القرآن الكريم. Ambapo MWENYEZI MUNGU ametoa changamoto kwa Waarabu na wataalamu wote wa Lugha kushindana katika Bayana ya Qu'ran kwa mtindo wao wenyewe.

Waarabu wakati ule wa kuteremshwa kwa Qur'an ndio walikuwa wahodari wa lugha ya Kiarabu.

Baadhi ya washairi bora kwa mfano Ka'ab ibn Zahir na Lubayda, waliishi wakati huo.

Waarabu walipoisikia Quran, walielewa kuwa hii si kazi ya mwanadamu kutokana na mpangilio wa Balagha uliopo humo ndani. Na ndio hekima ya MUNGU kumfanya mtume Muhammad (s.a.w) asiye jua kusoma wala kuandika ili kuepuka visingizio kwa wataalamu wa lugha.

Wasije wakasema ni maneno yake ameyatunga kwakuwa ni msomi.

Hebu fikiria hali ambayo mtu alisikia ukurasa wa Qur'an au Aya kadhaa za Qur'an, na yuko tayari kuacha imani yake ya awali, mji wake, n.k.

Hiyo ndiyo ilikuwa athari ya Qur'an kwa Waarabu. Kwa mfano, Umar ibn Khattab (RA) alisikia tu Aya chache za Surah Twaha na akawa Mwislamu.

Pia Malkia Elizabeth II wa Uingereza alikuwa akisikiliza usomaji wa Qur'ani Tukufu, bila shaka amesikiliza mazingatio mengi kutoka kwenye Qur'an. Pia idadi ya waislamu wanaoishi Uingereza imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana.
Eric Abidal - Mfaransa mchezaji wa zamani wa kandanda; alichezea Lyon na Barcelona
Aminah Assilmi - mhubiri wa zamani wa Kibaptisti
Kareem Abdul-Jabbar – mchezaji wa mpira wa vikapu aliyestaafu na mfungaji bora wa muda wote wa NBA

Kwa hivyo kujibu, Namna elimu ya 'Balagha' ilivyo ingiza watu wengi kwenye Uwislamu
Kwasababu Balagha hufanya usemi kuwa mzuri ikiwemo ufasaha wa maneno, ufasaha wa hotuba, na ufasaha wa mzungumzaji.

Na hivyo ndivyo QU'RAN imepangiliwa, inaathiri ukiisoma au kuisikiliza kwa mazingatio.

d127b656e556a4e305badd895a53bf90.jpg
 
Hivi ni kwanini pamoja na watu kuhamia na kuama imani/dini tofauti kwanini watu hawaachi dhambi?
 
Mkuu una kitu lakini umeshindwa namna ya kukifikisha. Niseme tu umekosa fasaha katika ufikishaji wako.
Umetumia misamiati migumu sana, kwa mtu wa kawaida (layman) ni vigumu kukuelewa unazungumzia nini?

Balagha ni elimu ngumu sana katika lugha ya Kiarabu. Si nahaw wala swarf inayoingia kwa balagha. Ulipaswa utuelezee, balagha ni nini? Na inafanyaje kazi kwa mifano.

Unaosema Qur'an ina balagha isiyo ya kawaida ya kibinaadam, yes, uko sahihi, lakini kwa mtu ambaye haijui Qur'an....anakuelewaje hapo? Qur'an ina mtindo wa lugha (balagha) very unique...... Qur'an ni mashairi...yes...lakini je yakoje?
 
Hivi ni kwanini pamoja na watu kuhamia na kuama imani/dini tofauti kwanini watu hawaachi dhambi?
Ahsante, watu hawaachi dhambi kwasababu vishawishi vya kufanya dhambi ni vingi kuliko vishawishi vya kufanya mema.

Wakristo wengine wanaamini kwamba wanadamu wote huzaliwa wakiwa na hamu ya kufanya mambo mabaya. Wanaamini kwamba dhambi ya asili inatokana na Adamu na Hawa kutomtii Mungu. Lakini sisi Waislamu tunaamini kwamba dhambi kuwa ni kitu chochote kinachokwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (Allah), ni uvunjaji wa sheria na kanuni zilizowekwa na dini.

Kusilimu ni mchakato ambapo mtu asiye Mwislamu anachukua utambulisho mpya wa kidini, kuchukua imani na desturi mpya, kujifunza kuishi kama Mwislamu na polepole anakubalika kama mmoja na wengine. Uislamu unafundisha kwamba mtu anapoukubali Uislamu kwanza, dhambi zake zote husamehewa. Mtu huwa hana dhambi kama siku aliyozaliwa. Baada ya hapo anasiku 40 za kujifunza taratibu za uwislamu.
 
Hivi ukihama dini utaenda mbinguni bil kufanya jitihada zako binafsi? Mimi naamini swala la kwenda mbinguni siyo la jumuiya ni lako mtu binafsi bila kujali uko upande gani.
Ni kweli, bila jitahada huwezi kuiyona pepo ya MUNGU, Ispokuwa kundi maalum ikiwemo vijusi vilivyoharibika kwa mimba zilizo tolewa, vifo vya uzazi, watoto walio chini ya umri wa miaka kumi, wenye matatizo ya kiakili ambao hawakuweza kujifunza, wale wanaotamka shahada ya Uislamu kwenye kitanda chao cha kufa kabla ya roho kufika kooni. Tofauti na hapo huwezi kuiyona pepo bila kufuata Amri za MUNGU
 
Dini zote zinaogopa competition ya kiimani isipokuwa Ukristo. Huwezi kuta Ukristo unazuia dini zingine maeneo yao.
Uislamu umefundisha uvumilivu kwa dini zingine, kati ya mambo ya msingi yanayo fundishwa na uwislamu ni kuvumiliana na kufundishwa kuamini uzuri na ubaya wa jambo linalotendwa na imani nyingine. Kwa hiyo, Uislamu mara nyingi huwafundisha wafuasi wake kuwa wasamehevu katika maisha ya dini nyingine, tabia ya kusamehe ya akili tukufu na ubinadamu na kuheshimu haki za wengine. Uislamu ndio dini pekee inayo amini katika mazungumzo.
 
Mkuu una kitu lakini umeshindwa namna ya kukifikisha. Niseme tu umekosa fasaha katika ufikishaji wako.
Umetumia misamiati migumu sana, kwa mtu wa kawaida (layman) ni vigumu kukuelewa unazungumzia nini?

Balagha ni elimu ngumu sana katika lugha ya Kiarabu. Si nahaw wala swarf inayoingia kwa balagha. Ulipaswa utuelezee, balagha ni nini? Na inafanyaje kazi kwa mifano.

Unaosema Qur'an ina balagha isiyo ya kawaida ya kibinaadam, yes, uko sahihi, lakini kwa mtu ambaye haijui Qur'an....anakuelewaje hapo? Qur'an ina mtindo wa lugha (balagha) very unique...... Qur'an ni mashairi...yes...lakini je yakoje?
Shukran sana ndugu. Ulisemalo ni hakika. Lakini ninatoa elimu kwa uchache walau kufikisha nadharia ya jambo.
 
Uislamu umefundisha uvumilivu kwa dini zingine, kati ya mambo ya msingi yanayo fundishwa na uwislamu ni kuvumiliana na kufundishwa kuamini uzuri na ubaya wa jambo linalotendwa na imani nyingine. Kwa hiyo, Uislamu mara nyingi huwafundisha wafuasi wake kuwa wasamehevu katika maisha ya dini nyingine, tabia ya kusamehe ya akili tukufu na ubinadamu na kuheshimu haki za wengine. Uislamu ndio dini pekee inayo amini katika mazungumzo.
Lakini kwann amruhusu imani zingine zije zishindane na uislamu.
Mfano uarabuni huwezi ukaeneza uKristo kichwa chako ni halali yako.
Lakini ulaya ni ruksa we eneza uislamu tani yako
 
Back
Top Bottom