Namna Mwekezaji Bill Ackman alivyogeuza $27m kuwa $2.6b ndani ya mwezi mmoja (almost 10,000% ROI)

Namna Mwekezaji Bill Ackman alivyogeuza $27m kuwa $2.6b ndani ya mwezi mmoja (almost 10,000% ROI)

Hivi kwanini Tanzania hatuna watu kama hawa? Carl, Auckman, Soros?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kwanza access ya markets hamna.

Bongo utanunua CDS kutokea wapi? Hata US stock tu au Stock options huwezi nunua utaishia kupata CFDs tu.

Mambo kama analysis na speculation kila mtu mwenye knowledge na ambae yuko informed anaweza fanya regardless ni mtanzania au mzungu.

Mfano issue ya $SVB nilikua informed na jamaa fln wiki kabla, cha kushangaza nacheki charts nikaona inapanda, jamaa akanitumia screenshot kwamba ka-short zaidi na akasema itablow soon. Five days later ngoma chali, the thing ni knowledge, information na access ya market
 
US stock tu au Stock options huwezi nunua utaishia kupata CFDs tu.
Unanunua sema initial capital ndio imechangamka na sio leveraged Kama hizi CFD. Ila still na hizi CFD Kama upo poa unameki 💰 💰 mbona Ila ama huwezi hold muda mrefu Mana daily swap zitamaliza faida yote ama kuongeza hasara. Huyo jamaa aliyekupa info kuwa naye karibu mno. Sie tunapata level two data najua wapo wanaopata level one dataor information faster mno
 
Jamaa alinielezea kwa nn inapanda na kwa nn yy akazidi kushort,

Ilikua kwamba $SVB walivyokua hawana cash ya kutosha na baada ya kuuza MBS zao kwa loss wakaona waissue na wauze shares zaidi, sasa mauzo ya hizo shares ndo yakasababisha ipande kdg ila kwa walokua na taarifa za kwamba SVB waliuza MBS zao toka mwisho wa mwaka jana kwa loss ndio wakawa wanacheza na charts tu. Taarifa ziliposambaa zaidi kwamba jamaa hawana cash ndipo downfall ikatokea, ila hizo taarifa kuna watu walikua nazo toka december mwaka jana
Wale wa jikoni ama unaye mshkaji anafanya kazi humo mlisoma naye ama mmekuwa naye kitaa. Mkikutana jioni mcity baada ya kazi anakupa za ndani chumbani.
Ingawa Kuna jamaa mmoja ameshawahi fungwa ama shtakiwa kwa ki trade with inside information,anamiliki hedge fund so alilipa almost $900M Kama sio bilioni hivi. Alikuwa ni Steven Cohen huyu jamaa aliotea game
 
Unanunua sema initial capital ndio imechangamka na sio leveraged Kama hizi CFD. Ila still na hizi CFD Kama upo poa unameki 💰 💰 mbona Ila ama huwezi hold muda mrefu Mana daily swap zitamaliza faida yote ama kuongeza hasara. Huyo jamaa aliyekupa info kuwa naye karibu mno. Sie tunapata level two data najua wapo wanaopata level one dataor information faster mno
Ukiachana na initial capital bado kununua haiwezekani kama ww ni mtanzania unless utumie mtu kama proxy wako anaekaa nchi inayoruhusiwa

Nmeshajaribu hadi FlowBank ya uswizi ukiachilia mbali brokers kadhaa kutoka Cyprus lkn wananambia siruhusiwi sababu TZ ni blacklisted.

CFDs nzr tu kwa hedging ili kula points za hz flactuations endapo unajua trade itapay within a day or two lkn kwa long term trader itakuumiza sana na hakuna faida nzr utapata.

Ukiwa na access ya kununua both stock na stock options, af uko informed na una knowledge ya hiz mambo basi utajiri upo wazi kabisa
 
haiwezekani kama ww ni mtanzania

NerdWallet's Best Online Stock Brokers for Beginners of March 2023​

 

NerdWallet's Best Online Stock Brokers for Beginners of March 2023​

Mkuu hapo hayupo hata mmoja anaepokea wateja kutoka TZ, yaan umeweka hadi Robinhood kweli?

Labda unioneshe proof, I'm in this fulltime practically, I cant wait to learn something new from u.
 
Cyprus sijui wapi huko Kama Seychelles,Bahamas,nk Mana huko hawana very strict rules za ku regulate brokers wa investment stocks or wa cfd
Na ndo maana inabidi uwatumie hao, baniani mbaya kiatu chake dawa.

Wao wanapokea hata pesa za magaidi ndo maana nikajaribu baada ya kila kona kushindikana, ila the bad news ni hawakuruhusu kutrade real Stocks
 
Mie nimekuuliza tu kuwa umewajaribu. Huyo akakubali USA tu nadhani.
Hapo nmejaribu Amertrade na robinhood tu, hao wengine nasoma terms tu naona hawatoniruhusu hata kabla ya kusignup sababu wanakua wameelezea kila kitu kwenye masharti yao, baadhi pia wana list ya nchi zinazoruhusiwa na sikuikuta Tanzania
 
Ila stocks ukisubiria ule muda ambao wawekezaji Wana wenge Mana hela zao zinashuka Kama korona hivi hapo wewe ndipo unapokuwa greedy unanunua kinyama wakati wengine wanauza wanaogopa kufilisika. So hapa Warren anasema be greedy when others are fearful and vice versa
 
Hello bosses and rosses...

Leo nmekaa mahala fln nikakumbuka pilikapilika za COVID-19. Kipindi hicho yalitokea mengi sana kwenye historia ya uchumi wa dunia, likiwemo lile ya bei ya mafuta ghafi(crude oil) kufikia zero hadi negative. Hapa nchini kwetu nakumbuka the rate Magufuli (RIP) alipeleka sampuli feki kwa mkemia mkuu zikakutwa na Covid (hahahahahahaaa)

Kilichofanya niandike huu uzi ni trade moja alofanya huyu jamaa anaitwa Bill Ackman, Bill ni bilionea mwekezaji na mfanyabiashara wa kimarekani na anamiliki Hedge fund pia.

View attachment 2562655

Huyu jamaa alipoona crisis ya COVID-19 mwanzon kabisa alibet kwamba taasisi/makampuni mengi yata-default kwenye bonds zao, hivyo yeye aliamua kununua securities fln zinaitwa CDS. Kiufupi CDS ni kama bima ila kwenye mikopo na bonds.

Kiufupi kabisa mfano mimi nikaenda kuchukua mkopo bank, bank ikanipa mkopo lkn ikaja kuona nina hatari ya kushindwa kuulipa(default) basi wanaweza kwenda kununua CDS kwenye taasisi inayouza hizo securities, ni kama BIMA fln tu. Sasa bank ikishanunua CDS kutoka kwa hio taasisi basi endapo mimi nitashindwa kulipa huo mkopo then hio taasisi itabidi kuilipa bank kiasi kilichobaki pamoja na interest. LAKINI ndani ya muda huo wa mkopo bank inakua inalipia fee fln kila mwezi/kila mwaka (ni kama premium kwenye bima) kwenda kwa hio taasisi iliowauzia CDS.

Kama umenielewa basi utaona endapo mwekezaji akinunua CDS anategemea kwamba BONDS zitadefault ili apate faida.

Sasa Bill Ackman alichofanya ni kununua CDS ambazo ilibidi awe analipia premium ya $27m kila mwezi, ambayo kwa mwaka inakua $324m. Na kinachomfanya jamaa awe legend ni kwamba aliingia at the right time, sababu baada ya kununua tu hizo CDS ndani ya mwezi mmoja zile bonds alizobet against zikadefault. Hio inamaanisha alilipia premium ya mwezi mmoja tu yaan $27m na baada ya mwezi ikageuka kuwa $2.6b. Hii trade ni kati ya trades kubwa sana kwa kizazi chetu. Na imeigizwa kwenye Season 2 ya HBO TV series INDUSTRY.


kali linux
Ivi ukitaka kununua stock za nje ni application ipi inatumika
 
Back
Top Bottom