Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

Pole sana mkuu mshtaki dereva mwenye gari na kampuni ya bima wote kwa pamoja.Wanasheria watakuongoza
 
Stori yako umenikumbusha siku ya ajali ya Shemeji yangu,mke wa bro..

Alipata ajali ya gari,aligongwa wakati anavuka barabara pale mwenge mida ya saa 3 usiku
Akakimbizwa hospitali ya rufaa pale karibu na makumbusho..Bila bro kuwahi kufika mkewe angekuta ameeshafariki Kwa jinsi Ile hospitali isivyojali wagonjwa mahututi

Taarifa ilipomfikia bro kwamba mkewe amepata ajali na amekimbizwa pale hospitali ya rufaa,fasta anachukua gari akafika,akauliza mgonjwa aliyepata ajali ya gari aliyeletwa km nusu saa hivi yupo ward gani? Cha ajabu akaonyeshwa alipolazwa.Alikuwa amelazwa Chini sakafuni,damu zinamvuja,taya zimevunjika,ulimi umekatika,kichwa kimeanza kuvimba na wahusika hata hawajali..so sad..bro angechelewa kidogo Tu angemkuta mkewe kwenye fridge..Akampakia kwenye gari fasta akamwaisha muhimbili

Ilikuwa ni ajali mbaya sn.Mgonjwa alipopata fahamu akawa anayakumbuka matukio ya mwaka kipindi wanatongozana na mumewe..matukio ya sasa yote hayakukumbuki Ila ya mwaka2005 kurudi nyuma ndy anayakumbuka,na anakumbuka km matukio yaliyotokea jana Tu au juzi na Sisi wengine hatujui kbs,anauliza kwani hawa ninkina Nani ..ubongo ni wa ajabu sn

Mkuu pole sn Kwa yaliyokukuta,ajali ni mbaya Sana,na km Una moyo mwepesi huwezi kutazama
 
asilimia kubwa ya vifo vya mahospitalini sababu ni uzembe wa watoa huduma na sio kwasababu ya ugonjwa au complications za magonjwa
utafiti wako umefanyia wapi ? hiyo asilimia kubwa ni ngapi ? we unafikiri ukifika tu hospitali utawekewa damu kabla hujapimwa mundi lako, damu inakaa kwenye fridge inabidi ikae ipate kwanza joto, hakuna binadamu anaefurahia binadamu mwenzie kuteseka
 
Mkuu ninakupa pole kwa kisanga kilichokupata, hata hivyo ni kudra tu ya Mungu ndiyo iliyokuponya!

Umeonesha namna gani taasisi za umma hasa zihusuzo huduma za kijamii zilivyooza!

Watu wapo kwenye ajira walizopigania kuzipata na wanalipwa mishahara lakini hawajali na rushwa zimetamalaki.

Narudia tena kusema pole!

Hii ndiyo hali halisi ya Tanzania tunayoiishi kwa sasa.
 
Pole sana Kiongozi...Mungu aendelee kutuepushia majanga
 
Sema watu wamepewa vitengo vya kuonea watu huruma lkn hawana huruma kabisa sijui ndo hawana wito na kazi


Ila bro unaonekana una vidharau flani mixer kujiona special sana Maybe wali sense ur energy..waka behave km wewe.
 
utafiti wako umefanyia wapi ? hiyo asilimia kubwa ni ngapi ? we unafikiri ukifika tu hospitali utawekewa damu kabla hujapimwa mundi lako, damu inakaa kwenye fridge inabidi ikae ipate kwanza joto, hakuna binadamu anaefurahia binadamu mwenzie kuteseka
Mkuu unaishi Tz hii?

Maana umeongea kama mtu anayeishi nchi za nje tena anayefanyia shirika la misheni.

Yaani umecomment kama vile simulizi za mtoa mada ni issue za uongo na kuwa vitendo vya namna hiyo watu hawafanyiwi!
 
Hii nchi kwenye huduma bado saaaaana tena sana, hospitali na polisi ni mtihani hasa ukiwa masikini Mungu atusaidie.Pole sana stori yako imenihuzunisha sana japo am happy u r ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…