Namna nilivyonusurika kufa kwenye ajali ya gari, Bongo unakufa huku unajiona

Nilitamani niweke picha kadhaa hapa.
Mwaka huu January mwishoni..mtu wa karibu kabisa alipata ajali akavunjika vidole vinne vya mikono na pia mguu wa Kulia.
Alipofika Hospital ya Wilaya wakamwambia hapa mpaka Jtatu utapigwa Xray..unaonekana hujaumia kabisa.
Tukajiongeza..kupeleka Hospital ya jirani bila kujali Bima ..kufanya Vipimo jamaa vidole havina kazi na Mguu.

Nawaeleza..ukiwa hizi Hospital either ya Serikali or Private kama una hela tembeza hela kwa haraka.
Bima ya Afya ina masharti zaidi ya vile inavyopigiwa kelele.Muda tunaotumia kubishana na wahudumu kuhusu Bima ndio muda mgonjwa anazidi kuteseka.
 
Pol
Pole ndugu Kwa masaibu.. unashangaa ungetembea speed kubwa Wala usingpata ajali. Maisha ni fumbooo
 
pole sana mkuu, ila nimeangia samsung yangu A something pozi likaniisha ๐Ÿคฃ
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
unataka tafiti ndio mtaacha kuua watu kwa uzembe wenu ?
Ebu wapumzisheni wahudumu wa Afya wanafanya mengi kuokoa Uhai na bahati mbaya huwa hawasifiwi yaani huwezi Kuja ukakuta Uzi hapa Jf unasifia mtoa huduma wa Afya ila wakienda kinyume cha matarajio yenu hamuachi kulaumu, nakuhakikishia kama wangekuwa wabaya kwa Kadri mnavyoelezea wagonjwa mahospitalini wasingepona kabisa! ebu tuwapende na kuwasapoti wanafanya kazi kwenye Mazingira magumu Sana na lakini bado wanajitoa kutuhudumia tuweke matarajio yetu pembeni na tuheshimu professionalism.
 
Mwanzoni nilijua hosputali za mission kuna masista wenye huruma kumbe nao nyoko tu mzee niliwahi umwa aise nipo hoi nawaambia nichomeni sindano hata ya kupunguza maumivu wao wananiangalia tu na kujipitisha huduma ya afya bongo bado sanaa
 
Mkuu pole Mimi binafsi nilifiwa na baba mzazi pale reception tulifika akiwa bado mzima na anaongea wakaanza kujadiliana wampokee au raha wakafikia maamuzi yao tushakaa saa moja bila huduma na mzee aliaga dunia hapo nimemlaza mapajani mwangu kisa walihisi ni covid case. RIP father.
 
Pole sana mkuu
 
Chai. Kuna viashiria vingi kuwa hii ni chai. Kwa wale wataalam wanaojua makosa wanaofanya wasimulizi wa ''story chai'' wa Bongo watakubaliana na mimi.
 
Asante bro,
Asante bro, ulikuwa kwenye nusu comma? Je vipi family hakuna mke na watoto ? Najaribu kufikiria tu jama wapo stress waliopata ?
 
Ni chai au sio chai we inakuhusu Nini?
Mbona unakua na akili za kipumbavu?

Soma tembea
Mwenye akili za kipumbavu ni mtu anayesema habari iliyowekwa kwenye forum haihusu wana forum! Jinga kabisa! Unadhani watu wote wana ubongo wa ndezi kama wewe?
 
Aiseh mkuu pole sana.....me nakumbuka kabla ya mwaka mpya....nlikua ndani kwangu nmelala gafla nkasikia kishindo kikubwa nje me naish karibu na barabara.....basi roho inanambia toka nje nkajisogeza mdogo mdogo kufika sehem ya tukio nkaona watu kama watatu mmja ni mwanamke analia kwa uchungu sana.......kumuangalia usoni bwana we nkamjua ni Dem wa mshikaji.......nkaanza kuomba msaada tumsaidie huyo dada....hakuna anaenisikiliza.....ikabid nitafute namba ya mshikaji.... mshikaji akasema ametuma mtu aje.....hapo nishahangaika mno Sina hata mtu wa kunisaidia.....badae akaja traffic ndo kumpeleka huyo dada hospital......kumbe alipasuka figo yule dada akawa amefariki........ nakumbuka hyo siku nlikua na mia 800 ndani ...... nkasema Mungu naomba unipatie maisha mazuri niweze kuwasaidia watu kipindi Cha shida

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ